Kuzirai kwa baadhi ya wananchi wa Igunga kutokana na kujiuzulu kwa Rostam!!

yani awa wanya-mwezi ni wa ajabu sana kujiuzuru ubunge tu wanalia,je siku za karibun tutakayomsindikiza segerea si ndio watakufa kabisa
 
kwanini isiwe ya kweli??

kumbukeni alishinda kwa kishindo na kuna watu walikua wanafaidi pesa zake kutokana na fitna za kisiasa, sasa watakula wapi??

lazima wazimie hao

Lakini ni wachache!
bora kukosa mali kuliko kukosa akili
 
Hata Pablo Escobar alipendwa sana huko kwao,na wahalifu wote ambao hutumia umasikini wa watu kujifanya wanawajali hupendwa mno hata kama unga wanaouza unawaharibu wao wenyewe,dunia ya masikini mtu makini na muadailifu huwa hapendwi.Hayo maendeleo utalinganisha na Kagoda ,EPA ,Richmond,je madhara yake kwa taifa ndio manufaa ya Igunga /tuache unafiki ,ingekuwa China jamaa angekuwa historia.Narudia tena watu wa igunga njaa zenu zitawaua.
kwanza najiuliza walijuaje kama anajiuzulu hadi watu wote waje na mabango hadi kutoka Urambo?


sijaona mabango yenyewe ila kwa walioyaona wanasema muandiko ni wa mtu mmoja na wino rangi moja.....
 
Tabora mji wa kimwinyi ule watu wavivu kazi yao kunywa gahawa tu. huyu mbunge wao si mtu wa porojo, pesa tu ilikuwa inazungumza tena vi shs alfu tano tano alfu km wale wazee wa ccm wanaridhika na ndo maana umeona wale wazee wa ccm wakizimia maana walishazoe kulilia njaa kwa fisadi
Ni kweli kabisa.
 
Mimi nipo igunga wapo wanufaika wakubwa wa ubunge wa R.A na ndo waloandaliwa kuzimia, mapema na mabango wakaandika in short kila mliloliona lilikuwa limepangwa!
 
Msiwalaumu sana wana Igunga, hayo ya kuzirai ni mambo ya kawaida ni sawa na wewe kufiwa na mjomba wako lazima chozi likutoke na pengine unazirai sababu unakuja ghafla - hata sisi wa dar na media zote wengi hatukuamini mapema sasa iweje mtu wa igunga?

Hawa wana igunga ni majeruhi wa kisiasa, ni muda muafaka wa Chadema kwenda na kuweka ngome kuu mapema, si igunga tu bali na majimbo mengine ya mkoa huu ambayo bado yapo nyuma sana ki maendeleo kwa mfano Urambo na sikonge.

Wanyamwezi ni werevu na wanyenyekevu sana, waliwaamini CCM kupita kiasi lakini sasa wamejua ndani yake kuna fitna na mizengwe, hii ni adv kwa vyama vya upinzani - chadema jimbo hilo.
 
Wakazi wa igunga wasukuma na wanyilamba ndo wengi wanyamwezi ni wa 3 kwa wingi jimboni
 
Hivi ndugu yako hata kama mwizi akifa hulii???? Mbunge wao anaiba huku anawapelekea kumbe wanakula vya Wizi!
 
Wakazi wa igunga wasukuma na wanyilamba ndo wengi wanyamwezi ni wa 3 kwa wingi jimboni
Asante kwa kuliweka hili sawa; nami nilitaka kutoa comment ya namna hiyo! Lkn sitetei wizi wa RA ila aliwekeza sana kwenye siasa za jimboni mwake kwa kuexploit, umbumbumbu na umaskini wa wananchi wake! I am sure hata kama angekuwa Moshi na angefanya equivalent (coz najua development projects/needs hazilingani) yale wanayosema kawafanyia wanaigunga Moshi, l am sure wachaga wangeumia kuondoka kwake!
 
Kwani kama kuna watu wanalipwa kwaajili ya kwenda kulia kwenye vilio kwanini hili lisiwezekane? Kwenye pesa kila kitu kinawezekana. Sisemi kwamba hilo ndilo lililotokea kwasababu sikuwepo na siwafahamu hao watu walikumbwa na nini. However, sishangai pia.
 
tunatakiwa kujua Igunga nikati ya wilaya ambayo haina maendeleo ya kutisha mimi napata ufahamu Igunga ulikuwa mji maarufu mpaka leo hii ungekuwa tunafikiria hata kuupandisha hadhi ya kuwa mkoa. elimu ndio usiseme asilimia kubwa ya wanaigunga hawana elimu niwachunga ng'ombe tu. umaskini nao nitatizo hivyo kunauwezekano walinunuliwa watu si unajua tz kila kitu kinawezekana.
 
Great thinkers, tuache ubishi na unafiki, pamoja jamaa na ufanyabiashara wake (Kupitia serikali) ila igunga kapabadilisha, tena kwa juhudi zake binafsi.
 
Back
Top Bottom