Kuzirai kwa baadhi ya wananchi wa Igunga kutokana na kujiuzulu kwa Rostam!!

Hayo ndio mazingira ya bunge letu la sasa...dhana ya kazi ya mbunge kwa sasa ni "kutoa misaada", kujenga barabara etc na sio kusimamia serikali, kutunga sheria n.k.

Ndio maana wanagombania posho eti ni kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wao!! Ndio maana hata mbunge asipochangia chochote mjengoni lakini hana wasiwasi anajua akirudi jimboni kwake na burungutu wananchi watajipanga mstari kuomba hela ya kula na nauli then kwisha kazi! Tusishangae watu kumlilia RA huko Igunga sababu aliweza kukidhi matarajio yao..MISAADA basi!

Mnakumbuka ile story ya Jambazi maarufi wa Jamaica DUDUZ? wakazi wa eleo alilokuwa anaishi yule mjamaa waligoma kutoa ushirikiano kwa polisi ili jamaa akamatwe kisa alikuwa ndio mfadhili wao, walifanya maandamano na kuweka bango moja limeandikwa "Jesus died for us, We will die for DUDUZ!"
 
Hujawahi sikia ile simulizi kuwa jambazi akienda kuwatembelea wazazi wake watampokea kwa furaha na dua tele za kubarikiwa a Mungu ili azidi kufanikiwa? Ni kwamba ukiwa unapata chochote hautajali sana kule kinapotokea
 
Wadau,
Huenda katika masuala ya kitaifa aliboronga na kuhujumu, LAKINI JIMBONI KWAKE NI LULU ISIYO KIFANI.
Tutafakari, tupime na kisha tujadili kwa mapana.

Yaah alilitendea Taifa ISIVYO,lakini huko ambako ndio anajua umuhimu wake yaani jimboni kwake ambako kwa ujumla ametumia PESA BINAFSI NA INFLUENCE,aliyoitengeneza huko juu kuweza kusababisha kutimiziwa anayoyataka kupitia POWER aliyokua nayo.

Kwa ujumla alitumia vifaa vyake binafsi kama Magrader na Katapila Bulldozer kutengeneza barabara, mabwawa na majosho ya ng'ombe ambayo alijua ni vitu muhimu kwa wakazi wa jimbo lake,kwa kuwa wengi wao ni wakulima na wafugaji.Pia alitumia PESA ZA KUTOKA MFUKONI MWAKE kugawa Pesa kwa wananchi wake kila alipoweka mguu wake,jimboni mwake.Alitoa kuanzia shilingi elfu tano mpaka kumi kila mwananchi alipoonyesha uso wake kwa huyu jamaa.Achana na shida za wapiga kula kulipia ada za watoto wao kama Tabia ambayo wabunge wengi wa bunge letu wameizalisha kwa wapiga kura ndio maana POSHO ilipoguswa Wabunge wakang'aka.

Kwa kiwango kikubwa jamaa ametumia PESA YA MFUKONI,ambayo kwa JICHO la PILI na kwa Mtu yoyote makini SIO SAWA WALA HAKI kwa UMMA kutumia PESA ya mtu binafsi kwa vigezo kuwa ni moja ya matunda ya uongozi wa mtu katika kustawisha jamii na maendeleo ya wana jamii,kama mwakilishi wa umma huo wa Wanaigunga..Kama angetoa msaada hiyo sina tatizo nalo,lakini kama moja ya bidii zake kama mwakilishi wa umma NOOOOOOOOOOOOO.
 
Kwa hiyo alikua anahamisha mali za umma ktk jimbo lake tena ambazo hakuzipata kihalali, isipokua kwa kutumia udhaifu wa viongozi wetu weusi ambao dunia mnzima inafahamu jinsi walivyo wajinga hadi inafikia wana kejeliwa kwa kupewa shahada za juu za uzuzu, na mataifa ya magharibi mbona bush hakuwahi kupewa, mm kwa mtazamo wangu hao walio zimia walipaswa kupitliza tu yani wafe yaani wana mpend muhujumu uchumi kiasi hicho, "fools die"- mario puzo
 
Jamani; Hivi mtu anaiibia nchi mabilioni ya watanzania na kujitumbukizia kwenye account zake kama message, akiona zimeshakuwa delivery ndo anatoa pesa hizohizo kiduchu anawapa igunga kupitia hao WALIOZUGA KUZIRAI. manake jamaa anatajwa kwenye dili nyingi za kudhulumu mihela ya watanzania, mtaalam huyu mwacheni aende tu, yupo kwenye bilioni 40 za kagoda zilizochotwa benki kuu ya Watanzania, Richmond, Dowans,....siasa zilikuwa sehemu za kuzugia na kukamata madili. Na nyie mliozuga kuzirai wote huko Igunga mkizinduka tu , polisi wote.
 
kibaya zaidi haya yanatutokea Tz kwenye karne ya 21 tukiwa na kumbukumbu isiyozidi karne ya utumwa na miaka with 50yrs of inDEPENDENCY!!
Hayo ndio mazingira ya bunge letu la sasa...dhana ya kazi ya mbunge kwa sasa ni "kutoa misaada", kujenga barabara etc na sio kusimamia serikali, kutunga sheria n.k.

Ndio maana wanagombania posho eti ni kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wao!! Ndio maana hata mbunge asipochangia chochote mjengoni lakini hana wasiwasi anajua akirudi jimboni kwake na burungutu wananchi watajipanga mstari kuomba hela ya kula na nauli then kwisha kazi! Tusishangae watu kumlilia RA huko Igunga sababu aliweza kukidhi matarajio yao..MISAADA basi!

Mnakumbuka ile story ya Jambazi maarufi wa Jamaica DUDUZ? wakazi wa eleo alilokuwa anaishi yule mjamaa waligoma kutoa ushirikiano kwa polisi ili jamaa akamatwe kisa alikuwa ndio mfadhili wao, walifanya maandamano na kuweka bango moja limeandikwa "Jesus died for us, We will die for DUDUZ!"
 
Nilishangaa mababa mazima yanalia dahh kumbe za EPA alikuwa anakula na wapiga kura wake
Njaa mkuu haina heshima... kuna wakubwa wengine wanapishikwa na njaa kali wanashindwa kujizuia na kuwa kama watoto, wanalia
 
Rostam alikodisha watu wa kuzimia!
Sio kweli Rostam hajamkodi mtu, ila wale walikuwa wanalia kwamba vibaruwa vyao ndio vimefikia tamati, au wewe haujui kama kuna watu wanaishi kwa kubomu? ile ni njaa inawasumbuwa.
 
Njaa mkuu haina heshima... kuna wakubwa wengine wanapishikwa na njaa kali wanashindwa kujizuia na kuwa kama watoto, wanalia

I see njaa mbaya sana mwanaume anauza utu wake kwa ajili ya njaa dah inasikitisha sana
 

Wednesday, 13 July 2011 20:57
0digg

Fidelis Butahe, Igunga
MJI wa Igunga na vitongoji vyake jana ulizizima, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz alipotangaza kuachia ubunge wa jimbo hilo.Tukio hilo liliambatana na matukio kadhaa ya wananchi kuonyesha mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti, wengine kuzirai na mara kadhaa kumvamia ili asiendelee na uamuzi wake huo.

Mbunge huyo aliwasili Igunga saa saba mchana na baada ya kufika akaingia katika ofisi za CCM wilaya na kuzungumza na Baraza la Vijana la Wilaya. Aliwambia vijana hao kwamba, halikuwa lengo lake kuingilia mkutano wao bali alitaka kuzungumza na wazee.

Wakati akiingia katika mkutano huo, alipokewa na mabango yaliyokuwa na ujumbe uliosomeka kwamba "Kama wakikufukuza na sisi tutaondoka CCM”, “Igunga bila Rostam hakuna maendeleo”, “Rostam umeboresha huduma za kijamii Igunga”, “Mbunge wetu tunakupenda sana” na “Tuna imani na wewe”.

Alitumia dakika saba kuzungumza na vijana kabla ya kukutana na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee, Kassim Ally. Akiwa na viongozi hao alizungumza nao kwa dakika 49.

Saa nane mchana aliondoka kwenda kwenye Ukumbi wa Sakao uliopo kilomita moja kutoka jengo la CCM wilaya hiyo.

Akiwa huko alipokewa na kisha kuanza kusoma hotuba yake ndefu ya kurasa takribani 10, lakini mara baada ya kutangaza kuachia nafasi zake ndani ya CCM huku akilengwa na machozi, baadhi ya wanachama walianza kulia huku wengine wakivamia meza kuu kumtaka mbunge huyo abadili uamuzi yake.

Wananchi hao walikuwa wamebeba mabango yenye maneno “ wao CCJ, sisi CCM”, huku wakilitaja jina la Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.

Kufuatia tukio hilo Rostam alilazimika kuacha kuendelea kuisoma hotuba hiyo kwa dakika 15 baada ya kuvamiwa na kundi la baadhi ya vijana waliomtaka kusitisha uamuzi wake huo na kuwasihi wasimzuie, ili amalizie hotuba hiyo na baadaye watoe maoni yao.

Baada ya wanachama hao kutulia walipewa nafasi ya kutoa maoni yao wakasema kwamba akiendelea na uamuzi huo watarudisha kadi za CCM.

"Hatukubali wewe kwetu ni muhimu sana umetufanyia mengi, yanayosemwa yavumulie nakuomba ubadili msimamo wako na kama hautabadili msimamo huo hatuoni haja wa kubakia ndani ya chama cha CCM," alisema Hamis Kanama.

Watu wazirai

Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

Mjumbe wa Barala la Utekelezaji la UVCCM, Hussein Bashe, alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio la Rostam kutangaza kung’atuka. Bashe ambaye alikuwa sambamba na Rostam tangu akiwa katika ofisi za wilaya aliliambia Mwananchi kuwa uamuzi wa Rostam ni mwiba mchungu kwa wananchi wa jimo hilo.

"Alichokifanya Rostam ni haki yake, lakini pamoja na hayo hawatendei haki wananchi wa Igunga, ila kwa kuwa ni maamuzi yake hakuna jinsi,"alisema Bashe na kusisitiza kwamba, CCM isipokuwa makini uchaguzi wa mwaka 2015 ukimalizika, utakiacha kikiwa chama cha upinzani na si chama tawala.

"Sekretarieti ya CCM itakabidhi chama kikiwa cha upinzani Watanzania wana matatizo mengi , lakini viongozi badala ya kuangalia hayo wanaendekeza siasa za chuki na kinafiki," alisema Bashe.

Rostam aondolewa na mabaunsa

Wanachama wa CCM waligoma kumruhusu Rostam kutoka katika ukumbi huo mpaka abadili uamuzi wake hali iliyosababisha vurugu na kufanya Askari wa kutuliza Ghasia(FFU) kuingilia kati.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa CCM walimtoa Rostam katika ukumbi huo kwa kuwatumia mabaunsa waliokuwa wanawazuia wananchi wasimzuie Rostam kuondoka.

Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai.

Viongozi wa CCM waliokuwapo
Viongozi wa CCM wengi kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora walihudhuria ambao ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora, wajumbe wa kamati ya siasa wa wilaya na Baraza la Wazee la Wilaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe

Alichosema Bashe ni sahihi kabisa CCM ijiandae kukabidhi chama mwaka 2015 kikiwa chama cha upinzani hakuna namna wanaweza kupona na sumu ya ufisadi ambayo imeingia mpaka kwenye mishipa ya Chama.
 
Wadau wa JF, mimi binafsi nimepigwa na bumbuwazi baada ya kusikia watu wamezirai eti kisa ni kujiuzulu kwa Mh.Rostam Aziz,hebu naombeni mnisaidie hii maana yake nini???Najua Igunga kuna wana JF itakuwa vyema mkitupa ukweli wa mambo kuhusu taarifa hizi za kuzirai kama zina ukweli wowote au la!!

Hata mimi kama wewe, lakini baada ya kutafakari sana mshangao ulikwisha kwa sababu: RA aliyekuwa msumbufu sana kwa serikali, mzigo mzito kwa chama na mwiba kwa makundi pinzani ndani ya chama, alihusika katika kuleta maendeleo ya Igunga almost singel handedly. Influence yake serikalini ilikuwa incomperable to any that I know. Hivyo ameweza kufanya makuu katika wilaya ya Igunga.

Muovu huyu kutoka Irani aliwafikia watu na kutatua shida zao binafsi. Zingatia kuwa alikuwa akizungumza na aliowaita wazee (presumably wa Chama Cha Majambazi) ambao walizoe kupokea vijisenti toka kwa huyu muwekezaji kutoka, sijui wapi, katika mfumo wa vi-asante asante kwa kuendelea kuwaaminisha wananchi kuwa yuko nao. Ni wale wazee wasio na upeo na vijana wa chama wanaofikiri bila RA maendeleo Igunga yatakoma. Ni wale wananchi ambao kila walipolia njaa, madawati, maji, umeme, sukari, dagaa, bila ya kushirikisha mtu au serikali, RA aliwasaidia. Hawa beneficiaries wa takrima toka kwa RA wanalia, wanazirai na kuugua kwa sababu walishazoea kuwa tegemezi na hawakufundishwa au kuzoea vinginevyo. Kwa nini wasilie na kusaga meno? Tena, wanajua fika kuwa sasa JK hatawaona kabisa sababu ataleta kilaza mwenzie agombee kwenye uchaguzi mdogo (na huyo kilaza atashidwa kwa kishido) na jimbo litaenda upinzani na fate yao inakuwa uncertain. Kwa nini wasilie na kusaga meno?

Wacha walie! Time is the master healer na siku moja watajiletea maendeleo yao wenyewe kwa sababu watawezeshwa na serikali makini ijayo.
 
Hii habari sioni kama inaweza kuwa na ukweli ndani yake,
kuna ukweli maana wakati jamaa katangaza tu kuwa kang'atuka, ule ukumbi ulizizima kwa simanzi na sintofahamu. Niliona (kupitia tv) wamama kwa wababa wakilia. And i ask to my self, what a wonderful world!
 
Watu wamezimia kwa sababu wana njaa halafu hotuba ndefu sana.

Rostam kaonyesha kwamba.

1. Kaweka maslahi yake ya kibiashara mbele ya dhamana aliyopewa na wananchi wa Igunga.
2. Hakuweza kupima kabla ya kujiingiza katika siasa kwamba siasa itaathiri biashara zake.
3. Ni mkata tamaa ( quitter) na kama ameshindwa kumaliza muhula wake wa ubunge, anaweza kuwa hivyo hivyo katika mengine ( Sarah Palin syndrome)

Dhamana ya ubunge ni kutoka kwa wananchi, the only ground for leaving this obligation would be leaving the party.
 
Kumbe waliozimia ni viongozi tu wa CCM, ingekuwa walala hoi wa mitaani ningesema alikuwa anapendwa! Kumbe magamba yaliokuwa yanategemea gamba kuu kuishi? Shame on them!
 
Kisaikolojia mtu mzima akilia kuna maana nyingi sana,lakini kwa mtoto kuna maana moja tu,kuwa kuna kitu kinamkera
Wadau wa JF, mimi binafsi nimepigwa na bumbuwazi baada ya kusikia watu wamezirai eti kisa ni kujiuzulu kwa Mh.Rostam Aziz,hebu naombeni mnisaidie hii maana yake nini???Najua Igunga kuna wana JF itakuwa vyema mkitupa ukweli wa mambo kuhusu taarifa hizi za kuzirai kama zina ukweli wowote au la!!
 
Back
Top Bottom