Kuzirai kwa baadhi ya wananchi wa Igunga kutokana na kujiuzulu kwa Rostam!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzirai kwa baadhi ya wananchi wa Igunga kutokana na kujiuzulu kwa Rostam!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir echa, Jul 14, 2011.

 1. s

  sir echa Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau wa JF, mimi binafsi nimepigwa na bumbuwazi baada ya kusikia watu wamezirai eti kisa ni kujiuzulu kwa Mh.Rostam Aziz,hebu naombeni mnisaidie hii maana yake nini???Najua Igunga kuna wana JF itakuwa vyema mkitupa ukweli wa mambo kuhusu taarifa hizi za kuzirai kama zina ukweli wowote au la!!
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii habari sioni kama inaweza kuwa na ukweli ndani yake,
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Nilishangaa mababa mazima yanalia dahh kumbe za EPA alikuwa anakula na wapiga kura wake
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wengi wao ama walinunua kulia ili ionekane jamaa alikuwa anakubalika au wanalia kwa kukosa marupu rupu waliyokuwa wanagawiwa kila wakimuona "mheshimiwa" au walikuwa wachawi wake hivyo kibarua kinaota majani sasa anaachia ubunge uliokuwa unamfanya awaone wamsafishie nyota yake.

  Badala ya kulilia rasilimali watawezaji kumlilia mwizi wa hizo rasilimali???
   
 5. i

  in and out Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  igunga ilikuwa wilaya haina maendeleo lakini katika uongozi wake amewafanyia makubwa
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usanii mtupu!!!!
   
 7. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  siku zote mwizi hupendwa kwao. ndio maana LOWASSA, CHENGE pia wanapendwa kwao. mzee MALECELA hakuwa mwizi ndio maana kwao sio maarufu hadi leo. TUNAHITAJI VIONGOZI KAMA MALECELA kwa ajili ya taifa la leo. kupendwa kwa rostam ni kutokana na vijisenti vya wizi ambavyo hata hivyo havifanyi mambo sustainable....tunataka list of shame..wale 10 wa mwembeyanga wote wawajibike....

  KUJIUZULU NI KLA KWANZA. KUWAJIBIKA MBELE ZA SHERIA NI JAMBO LINGINE. ROSTAM SASA APELEKWE KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YAKE.

  NB: Tukumbuke kuwa alikodi waandishiwa habari kwenda kuandika tukio lake! hashindwi kumpa hela mtu azimie!
   
 8. m

  mpweke Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Katika Igunga kafanya makubwa mno kuliko mnavyodhani. Ndio maana watu wakazimia. Ni wilaya pekee ambayo kila kaya ina Bima ya Afya. Shule za Sekondari zimezidi hadi kata zenyewe. Zahanati nyingi kuliko vijiji. Anasomesha watoto kadhaa wa kimasikini Igunga, utaacha kuzimia?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwanini isiwe ya kweli??

  kumbukeni alishinda kwa kishindo na kuna watu walikua wanafaidi pesa zake kutokana na fitna za kisiasa, sasa watakula wapi??

  lazima wazimie hao
   
 10. l

  lina Mongi Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanalia nini, walizoea kupewa vya bure na fisadi sasa wanafikiria watapataje tena kofia, Tshts ,vitenge na elfu kumi kumi. Wanaacha kuililia nchi yao iliyotekwa na wachache ( Mafisadi), walilie familia zao na jamaa zao zinazolala gizani kwa kukosa hata hela ya mafuta ya taa, mlo wa shida , matibabu ndio usiseme, wanamlilia fisadi R.A ambae amejilimbikizia mali za kutosha. POLE KWA WANA IGUNGA, Fungueni akili zenu
   
 11. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Igunga yazizima, Rostam kujiuzulu [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 13 July 2011 20:57 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Fidelis Butahe, Igunga
  MJI wa Igunga na vitongoji vyake jana ulizizima, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz alipotangaza kuachia ubunge wa jimbo hilo.Tukio hilo liliambatana na matukio kadhaa ya wananchi kuonyesha mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti, wengine kuzirai na mara kadhaa kumvamia ili asiendelee na uamuzi wake huo.

  Mbunge huyo aliwasili Igunga saa saba mchana na baada ya kufika akaingia katika ofisi za CCM wilaya na kuzungumza na Baraza la Vijana la Wilaya. Aliwambia vijana hao kwamba, halikuwa lengo lake kuingilia mkutano wao bali alitaka kuzungumza na wazee.

  Wakati akiingia katika mkutano huo, alipokewa na mabango yaliyokuwa na ujumbe uliosomeka kwamba "Kama wakikufukuza na sisi tutaondoka CCM", "Igunga bila Rostam hakuna maendeleo", "Rostam umeboresha huduma za kijamii Igunga", "Mbunge wetu tunakupenda sana" na "Tuna imani na wewe".

  Alitumia dakika saba kuzungumza na vijana kabla ya kukutana na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee, Kassim Ally. Akiwa na viongozi hao alizungumza nao kwa dakika 49.

  Saa nane mchana aliondoka kwenda kwenye Ukumbi wa Sakao uliopo kilomita moja kutoka jengo la CCM wilaya hiyo.

  Akiwa huko alipokewa na kisha kuanza kusoma hotuba yake ndefu ya kurasa takribani 10, lakini mara baada ya kutangaza kuachia nafasi zake ndani ya CCM huku akilengwa na machozi, baadhi ya wanachama walianza kulia huku wengine wakivamia meza kuu kumtaka mbunge huyo abadili uamuzi yake.

  Wananchi hao walikuwa wamebeba mabango yenye maneno " wao CCJ, sisi CCM", huku wakilitaja jina la Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.

  Kufuatia tukio hilo Rostam alilazimika kuacha kuendelea kuisoma hotuba hiyo kwa dakika 15 baada ya kuvamiwa na kundi la baadhi ya vijana waliomtaka kusitisha uamuzi wake huo na kuwasihi wasimzuie, ili amalizie hotuba hiyo na baadaye watoe maoni yao.

  Baada ya wanachama hao kutulia walipewa nafasi ya kutoa maoni yao wakasema kwamba akiendelea na uamuzi huo watarudisha kadi za CCM.

  "Hatukubali wewe kwetu ni muhimu sana umetufanyia mengi, yanayosemwa yavumulie nakuomba ubadili msimamo wako na kama hautabadili msimamo huo hatuoni haja wa kubakia ndani ya chama cha CCM," alisema Hamis Kanama.

  Watu wazirai

  Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

  Mjumbe wa Barala la Utekelezaji la UVCCM, Hussein Bashe, alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio la Rostam kutangaza kung'atuka. Bashe ambaye alikuwa sambamba na Rostam tangu akiwa katika ofisi za wilaya aliliambia Mwananchi kuwa uamuzi wa Rostam ni mwiba mchungu kwa wananchi wa jimo hilo.

  "Alichokifanya Rostam ni haki yake, lakini pamoja na hayo hawatendei haki wananchi wa Igunga, ila kwa kuwa ni maamuzi yake hakuna jinsi,"alisema Bashe na kusisitiza kwamba, CCM isipokuwa makini uchaguzi wa mwaka 2015 ukimalizika, utakiacha kikiwa chama cha upinzani na si chama tawala.

  "Sekretarieti ya CCM itakabidhi chama kikiwa cha upinzani Watanzania wana matatizo mengi , lakini viongozi badala ya kuangalia hayo wanaendekeza siasa za chuki na kinafiki," alisema Bashe.

  Rostam aondolewa na mabaunsa

  Wanachama wa CCM waligoma kumruhusu Rostam kutoka katika ukumbi huo mpaka abadili uamuzi wake hali iliyosababisha vurugu na kufanya Askari wa kutuliza Ghasia(FFU) kuingilia kati.

  Hata hivyo baadhi ya viongozi wa CCM walimtoa Rostam katika ukumbi huo kwa kuwatumia mabaunsa waliokuwa wanawazuia wananchi wasimzuie Rostam kuondoka.

  Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai.

  Viongozi wa CCM waliokuwapo
  Viongozi wa CCM wengi kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora walihudhuria ambao ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora, wajumbe wa kamati ya siasa wa wilaya na Baraza la Wazee la Wilaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 12. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna usemi usemao "Kila shetani na mbuyu wake". Siwezi kushangaa kwani hata yule unayefikiri hakufai anao marafiki wengi wampendao.
   
 13. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  nchi imekosa wazawa wa ukweli.....bila vita hakuna maendeleo hapa tz...
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,863
  Trophy Points: 280
  wamezimia mikofia na t-shirt ndio basi tena.
   
 15. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wadau,
  Huenda katika masuala ya kitaifa aliboronga na kuhujumu, LAKINI JIMBONI KWAKE NI LULU ISIYO KIFANI.
  Tutafakari, tupime na kisha tujadili kwa mapana.
   
 16. L

  Luiz JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ukosefu wa elimu unawasumbua wanainchi wa igunga.
   
 17. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Jambazi anapopigwa risasi au kuuawa katika eneo la tukio familia yake yaani wazazi, mke na watoto huuzunika na kulia sana kwani kwao huyo hakuwa jambazi bali mtoto, mume na baba. Kwa upande mwigine raia hufurahia kwani mali zao zinakuwa salama na utulivu kurudi. Mimi sishangai wananchi wa Igunga kuzirai kwani wanajua watamkosa mtoto, mume na baba yao kisiasa aliyewapa matumaini na kuwapatia walichohitaji bila kujali vilitoka wapi. Hawa ni shortsightedness kwani hawaoni hasara ambayo taifa limepata bali wanaona ktk mtazamio finyu wa vitu vichache na vya muda mfupi walivyokuwa wanapata.
  Ninachojua ni kwamba watu wachache wanalia kwa masalahi yao lakini wengi wa waTZ wanafurahi kwa sababu resource zao hazitaenda tena Igunga bali zitasambazwa kwa usawa,
   
 18. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni mijitu mivivu inayopenda vya bule,Kwani kuzimia kitu gani bana yangekufa kabisa.
   
 19. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,719
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Mh...Ingekua vice versa hapo sawa, lakini kama umeboronga kitaifa, jimbo linakuwaje afadhali!??
  Tafakari, pima kisha uje kujadili upya!
   
 20. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kaliibia Taifa na vizazi vijavyo kapeleka Igunga! Wizi ni wizi tu! Bora angekopa, huyu kaiba.... Ebo!
   
Loading...