Kuzingatia "vichwa": Wanawake sio ubaguzi huu?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzingatia "vichwa": Wanawake sio ubaguzi huu??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, May 7, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Katika stori na mdada fulani ambaye tumefahamiana mda mrefu aliniambia kuwa ana mimba, but sio ya boyfriend wake. Nilianza kumshushia lawama za u-infidelity hadi akapata mimba 'nje', yeye akasema hapana, it was planned. Anasema boyfriend aliye naye hawana mpango wa kuoana, bali kuondoleana upweke.

  Akasema kwa age aliyo nayo, hana tena mpango wa kuolewa na ameamua kuzaa akizingatia kuwa ana kipato kizuri so kujilea na kulea watoto walau wawili sio shida kwake.

  Then nikamuuliza why asizae na huyo boyfriend, akasema amemsoma akagundua kichwani sio mkali sana. Anasema huyo jamaa hata darasani hakuwa 'mzuri', na pamoja na kusoma shule nzuri matokeo yake hayakuwa ya kuridhisha.

  So, ameamua kwenda kuzaa na mtu mwingine (tena mme wa mtu), ambaye anaijua historia yake kuwa darasani zilikuwa zinachemka kisawasawa, na hata kazini alipo sasa wanamkubali.

  Eti ameamua kufanya hivyo kwani anajijua hata yeye sio kichwa sana, so anaona akizaa na mtu kama yeye tena, mtoto atakayezaliwa hata kuandika jina lake itahitajika kazi kubwa.

  Anaamini akizaa na mwanaume 'kichwa' uwezekano wa kupata 'average' au 'kakichwa' ni mkubwa!!!! na nasema siku hizi wapo wanawake wengi tu wanafanya hivyo, wengine wakichagua wacheza mpira, wanamuziki, waigizaji maarufu nk ili tu watoto ikitokea waje wafananie baba zao ...

  Ingawa alisimamia sana hoja yake, but mwishoni mi nilibaki na msimamo wangu kuwa huo ni ubaguzi kwani tukiangalia mambo kama hayo, wale 'mabongolala' tutakuwa extincted.

  Kama kuna mwanamke ana mawazo kama haya humu, naomba tu ayaache, na aache ubaguzi...
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Duh! Basi sisi ambao hatukupata divisheni wani fom foo tulie tu.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi nataka mrefu mweusi awe na mvuto maana mimi sina kuviile
  ila division ziro hapana kwa kweli......
  ziro ni noma heri lasaba wazazi wakakosa ada ......
   
 4. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mtalia sana huku mkijiliwaza kwa uhandsome na vijisent mlivyonavyo
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa we unataka watu wawaandae kabisa watoto wao kuwa wazembe?

  Alafu eti unasema ubaguzi. . .mbona nyie wanawake hua mnachagua (kwakuzingatia yale mpendayo) na sio mnachukua chukua tu?
   
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Unajua sheria ya nature inataka only the fittest to survive
  Zamani kua fit ilikua ni kukimbia, kuwinda na kulima sana
  Leo kua fit ni uwezo wa kufikiria, uwezo wa kazi nzuri etc.
  Basi dada katumia law of nature selection, only the fittest...
  But sijui kama akili nazo ni hereditary kama anavo pendekeza
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  craziness ya 'human cloning' ndipo inapoanzia...
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Sasa mie kilaza, nitafuta kilaza mwenzangu, hivi kweli huyo mwanangu mtarajiwa namtakia nini?

  Kwa weli hata mie namsapoti tu

  Mtoto kujua 'a' hadi akaombewe?

  Hivi mshaona trend za familia fulani fulani???? Wala msiseme kitu kabisa hapa.
   
 9. S

  Shaabukda Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe hii kitu ipo serious namna hii! Sasa wale wanaofaulu kwa kuiba pepa na kudesa inakuwaje hapa! Si unaweza ingia chaka!?
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,299
  Trophy Points: 280
  Kuanzia leo natembea na vyeti vyangu kabisa kumbe imefika huko.....Halafu mkuu siku hizi watu hawana aibu kuzaa nje ya ndoa ama kuzaa na mume wa mtu..Kifupi wamehalalisha style hiyo ya maisha.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Tena kweli, aliyepata wani ya 7 fomu 4 na wani ya 3 fomu six, nina yai moja mkononi nauza.
  Au leta viazi tutengeneze chips yai.
   
 12. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  sio kutembea na vyeti tu, pia personality ... how gentle, caring and nurturing you are, how think is your pocket etc.

  Poleni vijana wa leo.
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  tatizo wanaume wanatuona wajinga sana... kwanza mtu kaamua kujizalia mwenyewe ... lazima awe selective atii
  kuna genias mmoja ni dokta muhimbili ndo nammendea....
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hata iyo ni akili .... unadhani kuiba paper bila kushikwa upite form 4 upite six ..upite chuo semister 6 au zaidi .... si mchezo mkuu ... wewe ni mkali pia
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He he he he, mie natafuta roketi sayantisti

   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wabeba maboksi hatuna letu hapa. Gademu.
   
 17. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mm nimekutana na sista mmoja kama huyo ,yaan mama ameshazeeka ana watoto watatu lakin anachokiwaza yy na ameachika na wanaume wawili lakin mawazo yake kama hayo ,sasa kusema la kweli sifahamu inakuwaje ata mtu akawaza yasio wazika ,,hahaha
   
 18. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Ila ndo maana wanasayansi wanashauri kabla ya kuoa uangalie history ya familia. Mie nimeamini its true. We unaoa mwanamke kashindwa shule, kichwa ya biashara hana, unataka nini hapo? Unazaa mataahira!
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  teh mtu karisiti paper ya form foo weeee anafundisha chekechea ..... Mmmh ngoja ninyamaze wasije nipasulia server humu
   
 20. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  nimependa hiyo aidia ya dada....katumia akili sana.....
   
Loading...