Kuzidishiwa chenji au malipo: Mlipwaji kuuchuna ni baraka au ni kosa?

Habari humu!

naombeni ufafanuzi wenu, kuna mtu kanizidishia pesa niliyopaswa kulipwa, natafakari hapa je hii ni baraka au ni kosa?

maana kuna siku nilipita kanisa Fulani hivi watu walikuwa wakitoa ushuhuda,
na muumini mmoja akasema;
,"Namshukuru Mungu, konda nilipo mlipa nauli, akanirudishia kwa kunizidishia chenji, Oooh Haleluyaah!,"

Kanisa na mchungaji wakaripuka kwa ndelemo!
Sasa naleta kwenu wadau mnifahamishe, Je; Kuzidishiwa chenji au malipo ni baraka au ni kosa?

Maana nataka kuwa mtu mwema !!

Hiyo ni laana umechukua. Mrudishie kwa usalama wako.
 
Wakristo wanasema "Mungu hutenda kwa njia za ajabu" unajuaje kama hiyo ndiyo njia ya ajabu?
Huwa na assume jamaa kanpunguzia ... Sinaga mbwe mbwe ... Hafu roho haijawah nisuta
Basi mwenzenu ni muoga balaa!! Kwanza roho inaniuma sana. Hata nikiokota hela, sawa, ninaichukua lakini navaa viatu vya yule aliyepoteza hela yake jinsi anavyohangaika.
Kuna wakati nilikuwa huko kwenu Tanzania (Dar), jamaa mmoja hivi akanipigia simu, "Njoo hapa NBC/Jojis Club tunywe bia nina hela" basi nikaenda, kufika akanisumulia, " yaani nilikuwa ferry nakula, nimetoa 1,000/= lakini yule mama kajichanganya akanirudishia change kubwa akidhani nimetoa 10,000/=, tuinywe pombe" Kusema kweli nilisinyaa wala zile pombe sikunywa, japo ni mroho wa pombe. Nilimwambia kabisa umefanya vibaya kubanisha hiyo change!!!
In short mimi siwezi.
 
Hahaa kuna watu ni makauzu balaa.
Juzi tu hapo mida ya jioni nimeenda dukani na elfu 2 nataka vocha ya jero kanirudishia 9,500.. Nikamwambia wew hunijuie... Haya maisha ya Magu yalivyo kuwa hayaeleweki nikaikunja vizuri kabisa kwenye waleti..

Mambo mengine ni rizki tu
 
Mkuu wewe kama mimi siwezi zurumu ata mia ya mtu iwe umenizidishia au lah nitakurudishia ila Uzinzi kwa kweli utanisamehe ukisahau papuchi yako gheto kwangu ni lazima iliwe hapa tu ndio ninapojijua kwamba siwezi kwenda mbinguni ila mengine mbona simple tu.
Kwenye Papuchi kiukweli uaminifu sina ila pesa hata uache Mil 30 nitakurudishia.
 
Kwa swali lako jibu lipo kwenye kwenye suala la Star Times. Wao wamezidishiwa chenji/malipo kwa channel walizostahili kuzitoa bure lakini watu tulikuwa tukizilipia na ukiishiwa kifurushi na channels za bure zilizotakiwa kuendelea kuonekana zinakatwa. Hivyo hiyo siyo baraka bali ni kosa na dhuruma kubwa sana. Jibu ndilo hilo.
 
Basi mwenzenu ni muoga balaa!! Kwanza roho inaniuma sana. Hata nikiokota hela, sawa, ninaichukua lakini navaa viatu vya yule aliyepoteza hela yake jinsi anavyohangaika.
Kuna wakati nilikuwa huko kwenu Tanzania (Dar), jamaa mmoja hivi akanipigia simu, "Njoo hapa NBC/Jojis Club tunywe bia nina hela" basi nikaenda, kufika akanisumulia, " yaani nilikuwa ferry nakula, nimetoa 1,000/= lakini yule mama kajichanganya akanirudishia change kubwa akidhani nimetoa 10,000/=, tuinywe pombe" Kusema kweli nilisinyaa wala zile pombe sikunywa, japo ni mroho wa pombe. Nilimwambia kabisa umefanya vibaya kubanisha hiyo change!!!
In short mimi siwezi.
Sinywi pombe. Wala sikai dar ... Ila .. Nkizidishiwa chenji nachek nature ya mtu aliyezidisha ... Kama ni mmama namrudshia ... Kama ni mbaba namwacha accoton na his condition aszd kuwa mzembe ... Kama ni konda maweeee yaaan huyu. .. Hata angenizidishia na gari ... Yaan huyu hata sifikirii ... Kama ni kijana mwenzangu ... Ile hela ... Nanunua kitu chapu hapo hapo hafu ... Tunagawana .... Ila kama ni binti ... Uwiii hapo ... Namrudishia ... Na nnamwongezea ... Hafu tunakutana ... Hafu ananrudishia ... Kwa njia ya kipekee zaid .. # life hacks
 
Good. Nilikua supermarket fulani ya ndugu yangu last saturday kuna wazungu watatu wakaja mmoja ni regular costamer wengine nadhani walikua ni wageni wake.

Sasa katika kulipa mmoja wa wale wageni wakati anaondoka akasahau baku baku lake ambalo ndani tulihesabu tukakuta kuna dollar 2255 kamili.

Ndugu yangu akamrudishia for the sake of tht regular costumer.
Kwenye situation kama hii ww ungefanyaje mkuu.
Alifanya jambo la busara sana, faida yake ina weza isiwe ya hapo kwa hapo, ila matunda atayaona tu soon
 
Ni afadhali umzulumu tajiri kama bakhressa au mengi au dewji shillingi millioni 10, kuliko kumzulumu maskini elf 10 yake.... Impact za hawa watu wawili tajiri na maskini nitofauti kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom