Kuzidishiwa chenji au malipo: Mlipwaji kuuchuna ni baraka au ni kosa?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,217
2,000
Habari humu!

naombeni ufafanuzi wenu, kuna mtu kanizidishia pesa niliyopaswa kulipwa, natafakari hapa je hii ni baraka au ni kosa?

maana kuna siku nilipita kanisa Fulani hivi watu walikuwa wakitoa ushuhuda,
na muumini mmoja akasema;
,"Namshukuru Mungu, konda nilipo mlipa nauli, akanirudishia kwa kunizidishia chenji, Oooh Haleluyaah!,"

Kanisa na mchungaji wakaripuka kwa ndelemo!
Sasa naleta kwenu wadau mnifahamishe, Je; Kuzidishiwa chenji au malipo ni baraka au ni kosa?

Maana nataka kuwa mtu mwema !!
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,231
2,000
Sio kosa Bali ni wizi Mimi siwezi Fanya hivyo kunasehemu tulienda kula mi narafiki yangu msosi kama wa buku 14 yeye akakata buku 7 kwa one plate tukashangaa Yukawa tumeshatembea kama mita 200 tukagundua ametuzidishia tukamrudishia jamaa hakuamini kabisa..
 

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
9,964
2,000
Sio kosa Bali ni wizi Mimi siwezi Fanya hivyo kunasehemu tulienda kula mi narafiki yangu msosi kama wa buku 14 yeye akakata buku 7 kwa one plate tukashangaa Yukawa tumeshatembea kama mita 200 tukagundua ametuzidishia tukamrudishia jamaa hakuamini kabisa..
Safi mlifanya jambo jema sana.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
20,317
2,000
Kuna duka moja lilikua na wauzaji wawili, hawakua wakijua hesabu vizuri mara ya kwanza rafiki yangu ukuwi akaniambia kuhusu kuzidishiwa chenji. Nikaenda kuprove nikakuta ni kweli.

So tunafanyaje? Tunaenda kumpa taarifa mwenye duka au tufaidike na hiyo hali?

Tukachagua kufaidika na hiyo hali. So ikawa kila tunapokua broke tunaenda na elfu mbili tunanunua mkate mmoja.

Chenji atakayorudisha unaenda kuhesabia nyumbani.
 

majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,180
2,000
Dhamira yako inasemaje! Ungejisikiaje kama utamzidishia chenji mtu akurudishie?

Ni vema kurudisha, Mungu atakupa riziki yako kwa njia nyingine nyingi tu na sio kwa kukauka na chenji iliyozidi.

Mtu anauza maandazi, kamtaji kenyewe shilingi elf tano, anakuzidishia chenji unafurahia???? nooo!
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,228
2,000
Nilishawahi kumrudishia Mdada m.1 alinizidishia kwenye Kamati ya Harusi, alikuwa Mhasibu wetu, akiwa katingwa mie nikamrejeshea ile m. Hakika hakuamini jinsi ilivyotokea. Alishapotea kwa hofu ya kuathiri Ndoa ya mdau wetu. Tatizo likaja baadae, ule wema niliomtendea ukasababisha nimgegede kirahisi sana .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom