Kuzaliwa kwa CCM kulienda sambamba na mmomonyoko wa maadili ya uongozi hapa nchini.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Takribani mwaka mmoja na nusu baada ya kuzaliwa kwa CCM, nchi yetu ililazimika kupigana vita dhidi ya nduri Amini. Vita hiyo ilididimiza sana uchumi wa nchi kiasi kwamba kulianza kujitokeza uhaba mkubwa wa bidhaa za aina yote. Katika kukabiliana na tatizo hilo bidhaa muimu zilianza kuuzwa kwa mgaho; na hivyo ziliundwa kamati za kusimamia mgaho huo kuanzia ngazi ya mtaa/kijiji hadi taifa. Tofauti na ilivyokuwa katika enzi za TANU, ambapo chama hicho kilikuwa akijishughulishi na kazi za utendaji, kamati hizo za kusimamia mgaho wa bidhaa muimu, zilijumuisha viongozi wa CCM. Kwa ujumla utendaji wa kamati hizo haukuwa mzuri, kwani zilikuwa zinakula njama na watendaji kuuza bidhaa nyingi kwa bei kubwa kwa kupitia mlango wa nyuma. Mbegu ya ufisadi iliyopandwa wakati huo ndiyo ambayo imegeuka na kuwa donda ndugu. Matokeo yake, mafanikio yote yaliyopatikana chini ya uongozi wa TANU yametelekezwa; hii ni pamoja na elimu na matibabu bure, viwanda na makampuni mbali mbali, na hata uhuru wetu. Katika enzi za TANU maamuzi yote yalikuwa yakifanyika hapa nchini, lakini katika zama hizi maamuzi muimu yanayogusa mstakabali wa nchi yetu yanatolewa na wafadhili. Katika hali hiyo CCM haina cha kujivunia leo hii inapotimiza miaka 34
 
Back
Top Bottom