Kuzaa na mtu haikupi uhalali wa kuolewa naye

Joao de Matos

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
334
267
Kuzaa na mtu sio ndoa, unaweza ukazaa na mtu na asikuoe pia na hata ukalalamika kwa wazee wake kama hata taka kukuoa hatakuoa tuu.

Wasichana ujitunzi usizae tuu, na hata wazazi wako wakisema na kulalamika kwa familia ya mwanaume huyo mwanaume anaweza akakubali mtoto na asikuoe.

Kuna kijana mmoja alikuwa mchungaji mtarajiwa, akatengeneza mahusiano na binti wa mchungaji, wakaendela na mahusiano hadi wakafanya UZINZI na binti kupata ujauzito.

Shida ni yule mchungaji mtarajiwa kumbe alikuwa na binti mwingine ambaye alimtolea mahari, na ndoa ikatangazwa kanisani. Familia ya mchungaji hawakukubali jamaa aoe binti mwingine wakaenda kuweka kipingamizi kanisani kwamba asifunge ndoa.

Mahamuzi ya kanisa walisema kuzaa na mtu sio ndoa na haiwezekani kuweka pingamizi kwa sababu ya kuzaa na mtu, Hilo pingamizi likatupiliwa mbali na ndoa ikafungwa. Binti wa mchungaji kabaki single mother.

Akinadada muwe makini.
 
Kupinga ndoa isifungwe ni Kama sababu zifuatazo

1. Kama wamewahi kufanya uzinzi na kuishi pamoja Kama mme na mke, na unapopeleka kipingamizi lazima uwe na ushihidi wa kueleweka.

2.Kama mwanaume au mwanamke wamewahi kuoa au kuolewa na mtu Fulani ukapeleka ushahidi mbele ya kanisa Basi watazuia kufunga hio ndoa.

Sijajua Kama Kuna sababu nyingine Kama zipo Unaweza kuweka tukaona.
 
sasa sio wote wataolewa bana itoshe tu kukubaliana na kila kitu ila akili kichwani
 
Ni kweli kutegesha mimba au kutokuwa makini kwa mwanamke ni risk in many terms including hiyo ya mimba ambayo Mwanaume anakuwa hajatarajia wala kuridhia na kupanga hivyo hata yatakayofuata baada ya mimba hiyo dhamiri yake inamshuhudia kutohusika.

Risk Mojawapo ni ya u-single parent.
 
Wanawake wengi hutegeshea ili iwe chambo kumfanya mtoto kama kitega uchumi kupitia ruzuku ya malezi ya mimba na mtoto.

Lakini wanaume nao huwa wanawastukia kuchomekewa Kwa makusudi na kuona yeye hakushirikishwa na kuridhia kubebwa kwa mimba na kuzaliwa kwa mtoto huyo hivyo aloitaka hiyo mimba awajibike yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom