Kuzaa kila mtoto na baba yake ni kudhihirisha ukahaba

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
379
465
Thamani ya ndoa itabaki palepale sababu ndoa ni mpango wa Mungu ndoa ni kielelezo cha utu na heshima ya mwanadamu ndoa ni kilele cha malengo na matarajio ya mwili wa mwanadamu.Ndoa ni jambo muhimu kwa maisha ya binadamu na kizazi chake.

Moja ya dalili mbaya ya mmonyoko wa maadili na kukithiri kwa ujinga ni wanawake kufikia hatua ya kujivunia uzinzi na kuzaa watoto wazinaa.

Kuzaa zaa hovyo tena na mababa tofauti tofauti ni kuharibu future ya watoto wako sio ujanja bali ni ujinga. Itakupelekea kupata tabu ya malezi sababu siku zote malezi bora ya watoto yanatokana familia ya wazazi wawili.

Nikuchangaya damu na na kuvuruga kizazi chako unakuwa umepanda mbegu aina nyingi katika shamba moja hapo kila mtoto atakuwa na tabia yake kila mtoto ana ukoo wake unaleta mseto wa hovyo ambao utakucost wewe mwenyewe baadaye.

Unajidhalilisha na kudhihirisha ukahaba wako katika jamii na na hata kwa watoto wako kuna asilimia kubwa watoto wako kuja kuathirika na hiyo tabia yako na wapo watakao kuja kurithi huo mfumo wako wa maisha usishangae na wao kujakuzaa bila ndoa na wapo watakao kuja kujutia kuzaliwa na mama kama wewe usiye na maadili.

Kupandikiza mbegu ya chuki baina ya watoto wenyewe kwa wenyewe ikitokea katika hao watoto wale watoto ambao mababa zao wanahudumia vizuri watajiona wao ni bora kuliko wenzao ambao hawahudumiwi na baba zao tayari mpasuko unaanzia hapo.

Kutengeneza visasi na uhasama baina ya watoto na mababa zao ,kuna baadhi ya mababa watamalizana na wewe baada ya kujua kuwa unageuza watoto wao kuwa mtaji hiyo itapelekea kususia kutoa huduma na kuwatelekeza watoto tayari itakuwa ni bifu la baadae hilo kati ya baba na mwanae.

Unajipa mizigo na majukumu ambayo yatakufanya upate tabu na shida mpaka ujione unamikosi sababu hutoolewa hakuna mwanaume ambaye yuko tayari kuoa mwanamke mwenye msururu wa watoto tena kila mmoja na baba yake wanaume wenyewe hawa wa leo wanavyojua kukwepa majukumu yao.

Kupata tabu katika kupata huduma za watoto ,lazima utapata shida katika kuwafuatilia hao wazazi wenzio watoe huduma kama ikitokea wakawa na utata katika kutoa huduma za watoto bado utafeli hivi utaweza kuwapeleka mababa wanne au watatu wote ustawi wa jamii?

Ushauri wa bure kwa wanawake wote ikitokea umepata mtoto na baba hasomeki basi iwe ni funzo na mazingatio ujitathmini wapi ulikosea na nini cha kufanya sio kukurupuka kujizalisha hovyo tena ,ukitegemea utapata huduma kwa mababa hao ndugu yangu wanaume wengi huwa hawatahamini watoto wao wa nje ya ndoa unajitia katika mtihani mzito katika maisha yako fikiria kwanza kabla ya kutenda na muonee huruma huyo kiumbe asiye na hatia utakayemzaa.
 
Mke ni tofauti na Hawara,na kama wewe umezalisha wanawake tofautitofauti jukumu lako kuwahudumia .
Najua ni jukumu langu kuwahudumia watoto wangu wote.

Unazungumziaje mimi kuwazalisha wanawake wanne (wote ni wake zangu kwa mujibu wa imani yangu) ama vinginevyo. Katika dhana hiyo ya mwanamke kuonekana ni kahaba kwa mwanaume sio hivyo hivyo pia?
 
Kudhaa kila mtoto na baba yake si ukahaba, mwanamke ni mtu wa kudanganyika sana kama alivyodanganywa Hawa, lakini wanaume pia tunakimbia majukumu, na mwanamke akizaa mtoto mmoja ni rais sana kudhaa watoto wengine mana huwa wanaona aibu kadhaa nje ya ndoa na wanaanza kuingia kwenye ndoa za ovyo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua ni jukumu langu kuwahudumia watoto wangu wote.

Unazungumziaje mimi kuwazalisha wanawake wanne (wote ni wake zangu kwa mujibu wa imani yangu) ama vinginevyo. Katika dhana hiyo ya mwanamke kuonekana ni kahaba kwa mwanaume sio hivyo hivyo pia?

Hapa tunafarijiana tu, kama mwanaume imekutokea ukawa na watoto kwa wamama tofauti tofauti ndio mbaya zaidi kuliko hata kwa mwanamke.
 
Hapa tunafarijiana tu, kama mwanaume imekutokea ikawa na watoto kwa wamama tofauti tofauti ndio mbaya zaidi kuliko hata kwa mwanamke.
Nakubaliana na wewe na natafsiri kama kwa mwanaume kuzaa watoto kwa wanawake tofauti tofauti ni UMALAYA na ushetani wa kupindukia kuzidi hata mwanamke aliyezaa watoto na wanaume tofauti tofauti.
 
Ila wanaume nyie mfyuu si mnasema hamtaki kuoa single mom. Acha tuzae am plann niongezee watto 5 kila mmoja na baba yakr
Kinachonishangaza hawa wanaume wanasema hawataki kuoa single mother; halafu wanazaa nao haohao single mother, na lawama wanawatupia single mother ,na wanakuja kulalamika hapa na kutoa vijembe kwamba kuzaa watoto na baba tofauti ni ukahaba!

Yaani mwanaume ulimuona kabisa mwanamke ana mtoto wa baba mwingine,na wewe umeenda kumzalisha,halafu eti unaanza kulalamika!

Inashangaza Sana.
 
Back
Top Bottom