Kuyumba maadili chanzo cha gulio la kura - Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuyumba maadili chanzo cha gulio la kura - Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 24, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, amesema kuyumba kwa maadili nchini kumesababisha kuwepo na gulio la kununua kura za wananchi ili kupata nafasi za kuongoza.

  Mbowe alisema hayo mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye mikutano ya kuwashukuru wananchi wa jimbo la Hai kwa kumchagua kuwa mbunge wao pamoja na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.

  Alisema jambo hilo ndilo linalochangia watu wasio na sifa wala uwezo kuchaguliwa kuongoza hali inayosababisha viongozi kutowajibika kwa wapiga kura wao kutokana na ukweli kuwa kilichowaweka madarakani ni fedha zao walizotumia kununua kura.
  “Uongozi ni dhamana unayopewa na wenzako lakini leo umeingia sumu umegeuka mnada wa kura; mwenye fedha za kugawa na kununua pombe, chakula na vitu vidogovidogo visivyo na maana yoyote na kugawa kwa wananchi anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa.

  “Lakini athari yake ni kubwa kwa sababu kiongozi aliyenunua uongozi anasema ‘si ni hela yangu imeniweka hapa!’ hivyo hana haja ya kurudi kwa waliomchagua, lakini mimi kwa kuwa sikuwapa chochote ili mnichague ila mmenichagua kwa mapenzi na imani yenu kwangu na kwa tulikubaliana kushirikiana kwenye kutatua kwa pamoja changamoto zinazotukabili hivyo ninatekeleza wajibu kwa kuja kuwashukuru kwa kunichagua na tukae tuweke mikakati ya kusonga mbele.

  “Nawashukuru kwa kuniamini na kunichagua na kwa wale walioninyima kura nawaombea Mungu awape maisha mazuri na marefu ili waniangalie nikipiga mzigo kwa miaka mitano halafu wanipime kama walininyima kura kihalali au walinionea; natumaini baada ya hapo nao watanipigia kura,” alisema Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
  Akizungumzia tukio lake la kukamatwa na kushtakiwa jijini Arusha, Mbowe aliwataka wapiga kura wake kutompa pole bali wazidi kumuombea kwa Mungu ampe nguvu za kuendelea kupambana na udhalimu na ufisadi nchini mpaka hatimaye haki ipatikane na kila mwananchi anufaike na rasilimali za

  Source: Tanzania daima
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni aibu kuruhusu kuwa na gulio la kura!
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ziko njia tatu tu ambazo ccm inatumia kupata kura - na zote si halali.
  1. Kununua kura (gulio la kura)
  2. Wizi wa kura (kubaka demokrasia)
  3. Vitisho kwa wananchi kuwa wakichagua upinzani watauwana (hoja ya nguvu)
   
Loading...