Kuyumba kwa sasa kwa nchi yetu baba wa taifa hawezi kukwepa lawama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuyumba kwa sasa kwa nchi yetu baba wa taifa hawezi kukwepa lawama.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Jan 14, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa nchi yetu inapitia katika kipindi kigumu; kundi dogo la watu linaonekana limefanikiwa kukiteka nyara chama tawala na serikali yake, kiasi kwamba vyombo hivyo muimu kwa uhai wa nchi yetu, hivi sasa vinajishughulisha zaidi kuendeleza na kulinda maslahi ya ako kakundi kadogo badala ya wananchi wote. Mtu anaweza akauliza kwamba kama hivyo ndivyo, kwanini basi uongozi uliopo wa chama na serikali husiondolewe madarakani ili kuepusha balaha? Jibu ni kwamba kwa katiba ya sasa hilo haliwezekani, kwasababu hayati nyerere aliamini ya kuwa ili kuwepo mshikamano wa kitaifa, palihitajika kuwa na rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala, ambaye mamlaka yake hayawezi kuhojiwa na chombo chochote nchini. Na hivyo alihakikisha katiba yetu inampa rais wa jamhuri madaraka makubwa sana kiasi kwamba anaweza kuitwa mungu mtu. Jambo hilo linaweza kuwa na manufaa kama rais aliyoko madarakani ni kiongozi mwenye wito wa kuwatumikia wananchi kama alivyokuwa Baba wa taifa mwenyewe. Lakini akipatikana rais mchumia tumboni nchi inatumbukia kwenye maafa, na hakuna wa kuiokoa. Ndiyo yameipata nchi yetu kuanzia utawala wa Mkapa. Kwa kutumia madaraka ya kimungu mtu aliyokuwa amepewa na katiba Mkapa aliweza kuuza mashirika na nyumba za umma kwa bei poa huku wananchi wakilalama bila kujua la kufanya. Vivyo hivyo, hivi sasa wananchi karibu nchi nzima wanaonekana kutoridhishwa na mwenendo wa serikali yao lakini hawana la kufanya zaidi ya kukaa wakinungunika. Hivyo bila ya kuwa na katiba mpya, itakayopunguza sana madaraka ya rais nchi yetu itazidi kudidimia.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  I would say partly yes partly no!Is like mtoto wako umfundishe vizuri lakini akajifanya mdadisi akafanya ambayo hakutakiwa kuyafanya! Lakini kama mzazi ulitakiwa ku oversee his/her tracks.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  When are we as Tanzanians going to take responsibility of our own destiny? Baba taifa was there and has gone. Ametuachia nchi yenye amani.
  Viongozi tuliowachagua wametuangusha. Tuna vyama vingi vya siasa unlike wakati wa Nyerere. Kwa nini hatutumii fursa iliyopo kupata viongozi bora tunakubali kuhongwa tu na vi tisheti, kanga na sahani ya wali kuwachagua mafisadi. Let us take responsibility of our own future.
   
Loading...