Kuyapokea matoekeo ya Uchaguzi kwa amani ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuyapokea matoekeo ya Uchaguzi kwa amani ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Oct 28, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jamani kama mmesikiliza tokea juzi na jana na hapa tulipofikia kuna vyombo mbalimbali vimesikika vikionya kuwa matokeo yapokewe kwa amani na utulivu ?

  Je mnakubaliana na mavuvuzela hao ? Nakumbuka miaka yote iliyopita matokeo yalikuwa yakitolewa na yakipokewa kwa amani ,sasa hili au haya makelele yanayozuka safari hii ,hivi kuna jambo gani lilojificha hata pakatolewa onyo na vyombo kutishia amani ya wananchi ??

  Kama ni wizi wa kura watu wafanyeje ? Kama kuna kuchakachua wananchi wafanye nini ,hao wanaotoa onyo hawajawaeleza wananchi ikiwa matukio ya kura au tuseme ya uchaguzi yatapindishwa wafanye nini ? Sheria hairuhusu kuhoji matokeo yakishatangazwa haswa ya uraisi ,akishatangazwa ndio imetoka.

  Je kwa mikiki na makeke haya ya kuwambia wananchi watulie chali na kuridhia kila kinachotangaza ,hapaonekani kama hapa pana mgawo unataka kufanywa na kitakachogaiwa ndio hicho hicho uridhike ???
   
 2. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mkuu nami hii naitafakari bila mwafaka. Kuna ninini mbona siku zote matangazo na tahadhari hizi hazikuwepo?

  Kwa taarifa zao, wakileta usanii tutabanana mafunzo ya JKT waliyatoa bure hivo huo ujuzi tunao wala sisi sio makondoo. Tutakubali matokeo yanayo onesha ukweli. Usanii watajuta.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hilo litakua kosa, maana utapambana na vyombo vya dola vilivyokwisha jazwa kasumba ,kuwa atakaeleta au kupinga mat5okeo ni msaliti wa azimio lao la kupokea matokeo kwa amani na utulivu ukijumlisha na kuyakubali ,sasa utakaa vipi wakati mawakala weshaweka saini ,na kukubali. Hivyo ndivyo tutakavyotangaziwa kuwa kura zeshahisabiwa na mawakala weshaweka gumba ,mabo redioni ,kwa maana hiyo hakuna wa kupinga na tutaona ,we tulia
   
 4. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwiba, peoples power inahitaji ignator kidogo tu, ngoja wafanye ujinga wao, ya Kenya yatakuwa historia tu ila hapa kwetu itakuwa live show!! watu wameshachoka mkuu, mi naona watu wako tayari tena bahati nzuri wale wote wenye nguvu wanadai mabadiliko. Mimi nawewe tunataka changes, lakini hata siku moja hayo mabadiliko twajua hayatakuja kirahisi tena kutoka kwa hawa FISADI's ila kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tusubiri tuone.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kweli peoples power lakini sio Tz ,yaani WaTz hawawezi hata siku moja kukusajika Ikulu kwa mida ya siku zaidi ya moja ,jengine ni woga na kama haitoshi watu huwa tunachekana baada ya kupigwa marungu na mabomu ,hivyo risasi ya mwanzo tu humuoni mtu ,nakumbuka maandamano ya CUF jangwani ,wanaCUF na ungangari wao wakikamatwa kirahisi na kwekwa kwenye karandika ,ikiwa wakati ule waliachiwa CUF peke yao je umoja huo leo hii utatoka wapi ?? Mkuu usicheze na vyombo vya dola haswa hivi vinavyolipwa hela ndogo ,huwa wana hasira sana.
   
 6. Pacemaker

  Pacemaker Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Panapofuka moshi....?Tahadhari kabla ya hatari. Sivema kukataa kuhoji juu ya hali ya tashwiswhi iliyotanda wkt huu. Endapo tutafanya hivyo tutakuwa tumeingia chaka ambalo logic huita "Fallacy of denying the hypothesis" maana wapo ambao wanajihami kwa kuthubutu kudai ushindi ni lazima, nyingine hiyo fallacy of affirming the conlusion.

  Binafsi naamini Amani ya nchi hii ipo kwa sababu ya rehema za mwenyezi Mungu. Naamini ndiye aliyetujalia Wtz uvimilivu katika masahibu yote ambayo tumekutanana nayo. Imefika wkt uwazi na ukweli uliohubiriwa enzi za Mkapa uonekane hasa ktk mchakato huu wa uchaguzi. Mamlaka husika ziwajibike kuzingatia kuwa mchakato una kuwa wa haki pasipo utata kwa vyovyote vile.

  Sina hakika sana kuwa uvumilivu huu utaendelea iwapo haki ya Wtz ya kidemokrasia ya kupata uongozi bora kwa kupitia kura halali ktk masnduku ya kura.

  Kwa kuwa wengi wetu tunaamini sauti ya watu sauti ya Mungu basi wito wangu ni kuwa heshima stahiki itolewe kwa sauti ya watu. Nafikiri watu wazima vijana kwa wazee wenye akili timamu hawatokataa matokeo ambayo yanaakisi sauti ya watu kwa haki.

  Angalizo Mungu hadhihakiwi. Mungu si mwandamu hata aseme uongo. Chonde chonde wakuu wote wenye nyadhifa ktk taasisi husika wasiingie majaribuni kuvuruga uchaguzi. Kiukweli sote tuna madhaifu kama wanadamu, Tumeshuhudia rafu hapa na pale ktk kampeni nawasihi wadau wote, rafu zisipewe nafasi ktk upigaji kuhesabu kujumlisha au kutangaza matokeo/mshindi.

  Ikiwa haki itanzingatiwa basi wahusika hawapaswi kuwa na hofu kuhusu kukubalika kwa matokeo kwa kuwa Mungu muweza wa yotealiye juu sana husimama na wanaozingatia haki kwa hivyo hata kwa uchache wao atawalinda.
   
 7. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  do not underestimate the power of people!
   
Loading...