Kuwepo utaratibu wa kuwaadhibu viongozi wanaotumia madaraka vibaya au wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Moja wa kauli za Rais Magufuli kuhusu uwajibikaji aliwahi kusema kwamba “Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwasababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza”.

Uwajibikaji ni kitu muhimu sana kwa nchi yoyote ile inayotaka maendeleo na ustawi wa kiuchumi. Kila mtendaji au kiongozi katika eneo lake la kazi anatakiwa awe na dhamana ya yale yote yanayotokea katika eneo lake.

Kuna njia mbalimbali ambazo huchukuliwa kama mojawapo ya sehemu za uwajibikaji. Mfano;

1. Kujiuzulu kwa viongozi walioko madarakani,
Mfano; George Simbachawene alijiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia agizo la Rais la kuwataka watu waliotajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na Almasi kupisha.

Mwaka 2013 aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa naye alijiuzuru katika nafasi hiyo kutokana na kashfa ya ufisadi na kusema kwamba alifanya hivyo ili kuonyesha uwajibikaji.

“( Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.)”

2. Wafanyakazi kufukuzwa kazini au kuondolewa kutoka kwenye nafasi zao,
Mfano; Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo.

Ndugu Wilson Kabwe, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar alisimamishwa kazi mwanzoni mwa mwezi Mei, hivi sasa ni marehemu.

Rais Dk John Pombe Magufuli alitengua uteuzi wa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga kutokana na waziri huyo kuingia Bungeni kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

3. Wananchi kutomchagua kwa mara nyingine kiongozi ambaye hakuleta maendeleo katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi.
1. Wasira alipoteza jimbo la bunda
2. Wenje alipoteza jimbo la Nyamagana
3. Machemli alipoteza jimbo la ukerewe
4. Aggrey Mwanri alipoteza jimbo la Siha
5. Sirili Chami alipoteza jimbo la Moshi vijijini
6. David Kafulila alipoteza jimbo la Kigoma kusini
7. Moses Machali alipoteza jimbo la kasulu

Kuwepo mfumo wa udhibiti wa matumizi ya madaraka;
Kuwepo utaratibu wa kuwalazimisha viongozi kutekeleza wajibu wao na kutokiuka wajibu wao, Kuwepo utaratibu wa kuwaadhibu viongozi wanaotumia madaraka vibaya au wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao
 
Kuwepo mfumo wa udhibiti wa matumizi ya madaraka;
Kuwepo utaratibu wa kuwalazimisha viongozi kutekeleza wajibu wao na kutokiuka wajibu wao, Kuwepo utaratibu wa kuwaadhibu viongozi wanaotumia madaraka vibaya au wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao

Hapa nakubalina na wewe, ila ugumu utakuja tunaweza kupata tume au taasis ambayo ipo huru isimamie haya?
 
Tatizo ni mfumo. Atawajibishwa na nani ilhali hayo madudu wanafanya wote huko juu?
 
Back
Top Bottom