Kuwepo na alama itakayoonyesha trafic aongozapo magari kwenye mataa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
175
Salam wapendwa,

Kama kuna wataalam watakaonisoma, napendekeza kuwepo na alama au ishara katika mataa ya barabarani itakayomwonyesha dereva kuwa sasa anayeongoza magari ni trafic na si taa.

Nashauri hivi kwasababu nimeshuhudia kiasi kama mara 2 ajali zikitokea eneo la mataa, sababu kubwa ni kukosa mawasiliano. Trafic kaongoza magari ya upande mmoja na wa upande wa pili bila ya kujua wakaingia kwa kuwa taa zinamewaruhusu ikasababisha ajali, bahati nzuri nilizoziona hazikuwa serious sana. Ila kuna uwezekano kabisa wa kuwa na ajali za kutisha kutokana na kosa hili.

Ni vigumu kutambua ni nani anayeongoza magari kwenye taa wakati wote, maana trafic anaingia wakati wowote na kuacha wakati wowote.

Nawakilisha!
 
Back
Top Bottom