Kuwepo mdahalo kati ya CCM na upinzani. Je ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwepo mdahalo kati ya CCM na upinzani. Je ni sawa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by CAIN, Oct 26, 2010.

 1. C

  CAIN Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenu wanaJF.

  Je ni sawa kuwepo kwa mdahalo kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani???

  Nimependa niweke mada hii kwa mambo mawili.. matatu yafuatayo:

  - Kwanza:
  Kuweka mdahalo kati ya chama tawala CCM kilichotawala kwa zaidi ya miaka 40 na vyama vya upinzani (Chadema, CUF, UDP, NCCR-Mageuzi,... nk) ambavyo havijawahi kutawala kabisa si sawa. Kuweka mdahalo huu ni sawa na kumpima mtoto aliyesoma darasa la kwanza na mwingine ambaye hakusoma kabisa kisha ukawapa mtihani mmoja, ni wazi kwamba yule ambaye hakusoma kabisa atakuwa na la kujitetea.
  Hapa ni rahisi kuikosoa CCM kwa kuwa tayari imeshakaa madarakani na kutoukosoa upinzani ambao haujawahi kuongoza nchi.

  Pili:
  Kuweza kufikia maendeleo makubwa kama ilivyo kwa nchi za Ulaya na Marekani inahitaji muda wa kutosha ikichukuliwa kwamba jamii yetu (Tanzania) bado haijaelimika vya kutosha hivyo kuwezesha nchi kuwa na maendeleo hayo.

  Lakini tujiulize ni mambo mangapi ambayo Serikali chini ya CCM imeyafanya na kuendelea kuyafanya ilihali watu wakiendelea kufaidika nayo??

  Kwa upinzani/Chadema kuweza kujibu maswali yote katika mdahalo ni rahisi sana kwa kuwa wakati wote watajibu wataweza na wakati huohuo huwezi kuwasahihisha ama kuwakosoa kwa kuwa hawakuwahi kuongoza nchi, ambapo tungeweza kupima na kujua ni lipi walilitekeleza na lipi hawakulitekeleza.

  Hivyo sioni tatizo kwa Makamba kuwataka wagombea wa CCM kutoshiriki midahalo.

  Kupima ubora wa pande mbili ni lazima pande zote ziwe zimeshiriki katika jambo tena kwa muda ulio sawa.
   
 2. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Umemaliza?
   
 3. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni sawa, lakini ccm hawatakubali hata kidogo
   
 4. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Ndio maana Chadema wanaingia kwa miaka mitano kwa kuanzia kisha Uchaguzi ujao kutakua na mdahalo mtupime, umeelewa?
  safi sana mwalimu wako haupatashida kukufundisha.
   
 5. m

  mosesk Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndugu yangu kama ni hivyo basi CCM wasingekuwa wanafanya kampeni kwa sababu wao wako madarakani na mambo yao mazuri watu wanayaona na kuyafaidi. Kwanza kabla ya kutoa majibu rahisi namna hiyo inabidi tujiulize nini maudhui ya mdahalo. Mdahalo unawahusisha watu gani kwa nia gani, ukipata jibu ndiyo tuseme je ni haki kwa CCM kukimbia Mdahalo?

  Kimsingi mdahalo unawahusisha wanaogombea na pia wanaoongozswa kwa maana ya wananchi, ni katika mdahalo huu ndipo ahadi tata za wagombea zinajadiliwa na wagombea wenyewe na pia wananchi. Ni furusa pia ya wagombea kuulizana maswali na kutoa ufafanuzi pale ambapo kuna jambo ambalo halieleweki.

  Kwa hiyo kimtazamo CCM wanakimbia kutokana na kuogopa maswali magumu kuhusiana Ilani na ahadi zao. Katika kampeni CCM imetoa ahadi nyingi nafikiri imevunja record kwa wingi wa ahadi toka CCM na kabla TANU vilopanzishwa.

  Kinacholeta hofu ni kuwa kwa mfano mgombea anaahidi mfano Kununua meli tena kubwa kuliko ile iliyozama ziwa Victoria. Watu wana maswali iweje iwe leo, kwani meli iliizama karibia miaka 10 iliyopita kwa nini haikununuliwa kabla? na maswali mengi zaidi ya ahadi za kigoma - (Meli), Mbeya - ( Meli) kama ndivyo hivyo i kwa kipindi gani zitakuwa tayari? maswali haya yote yanatakiwa ufafanuzi wa ana kwa ana.

  Tumemsikia Mgombea wa CHADEMA kuwa Elimu itatolewa bure, kivipi kwa uchumi upi, zinahitajika shilingi ngapi?. Ni furusa pia ya wagombea kulizana maswali juu ya ahadi zao na kupata ufanunuzi wa kina.

  Sioni maantiki kwa CCM kukimbia mdahalo halafu kujibu mitaani kuwa CHADEMA wanadanganya, hakuna uwezekano wa vifaa vya ujenzi kupuguzwa gharama wala Elimu kutolewa bure.

  Ninashindwa kuelewa kwanini wamefanya hivyo sasa? mbona CCM iliwahifanya mdahalo mwaka 1995 tena kwa mafanikio makubwa? Sababu hizo zote hazikuwepo na mazingira ni yaleyale.

  Kimsingi ni rahisi kukubali kuwa CCM inadanganya kwenye ahadi na Ilani yake ndiyo maana wanakimbia Mdahalo kama sivyo naomba wafanye mdahalo ili kuondoa wingu hili vinginevyo tutaamini hivyo.
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu,
  BTW - say whatever you want kuhusu Mkapa (I too have a lot to say) BUT... Mkapa wa 1995 alikuwa si mchezo. Nakumbuka jinsi alivyomgaragaza mgombea wangu (mzee wa kiraracha) kwenye ile debate hadi ikatia huruma.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Chadema hawajashika madaraka ya kuongoza nchi, lakini majimbo wanayo, majimbo yanayongozwa na Chadema ndiyo yenye maendeleo ya kutukuka, kodi za unyanyasaji zimefutwa, watoto wanalipiwa ada ya shule na halmashauri, miradi ya maji, dispensari siyo tatizo tena, kulinganisha na halmashauri zinazoongozwa na ccm.

  Sasa wapeni Tanzania watuonyeshe maana ya maendeleo ya taifa na jamii.
   
Loading...