Kuwepo damu mpya bungeni, tutazamie nini bunge lijalo?

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Bunge la safari hii kwa kweli limevunja rekodi. Nadhani hatujawahi kuona Bunge lenye mchanganyiko wa watu wenye uwezo wa kuchanga hoja kama hawa. Sio tu kwamba wana uwezo wa kuchanga hoja, ila pia wanawakilisha mawazo mbadala na hivyo kunogesha zaidi vikao. Lakini lililo kuu zaidi ni ule uwezo wa kuiweka serikali "kiti moto" na kuilekeza kufanya yale wananchi waliyoituma.

Katika hali hii tutazamie nini katika Bunge hili? Nadhani kwanza tutazamie ushindani wa hoja utakaotokana na makundi mawili; lile la wabunge vijana na wenye mawazo ya kimapinduzi na la wale mahafidhina (conservatives) Kundi la vijana wanatarajiwa pamoja na mambo mengine ku-introduce chachu ya mabadiliko ambayo watazania tunatamani sana kuyaona na kuyafikia. Ushindani huu utasababisha ama upande mmoja ku-give in, na kukubaliana na angalau baadhi ya mambo ya upande mwingine katika mambo ambayo yataleta mabadiliko makubwa ya kimtazamo na utendaji serikalini na machoni mwa jamii. Mfano ni hoja ya ufisadi iliyotambulishwa na Dr. Slaa katika Bunge lililopita jambo ambalo lilileta mtazamo mpya katika jamii nzima juu ya kitu ufisadi hata kusababisha mtikisiko serikalini.

Pili tutazamie kutikiswa kwa ccm na serikali yake. Huku kutatokea kwa sababu bila shaka wapo wabunge wa ccm watakoungana na wale wa upinzani at least katika baadhi ya hoja nzito kama ilivyokuwa ya Richmond na nyingine iliyoleta "earth quake" ndani ya ccm mpaka kamati ya mzee "ruksa" ikaundwa.

Hii yote mimi inanipa meseji hii: Tanzania inapitia mchakato wa mabadiliko ya kimtazamo, na kifalsafa. Ni ukuaji wa demokrasia, na faida ya upinzani nchini. Spika anayetakiwa kuongoza bunge la aina hii ni muhimu sana akawa mpevu na mwelewa wa mambo, la sivyo cheche zitawaka bungeni. Ndiyo maana nadhani wabunge wanahitaji kuwa makini sana wanapochagua Spika safari hii. Nawaombea hekima ya Mungu katika hili.
 
well said, lakini hayo yote yatawezekana iwapo tu ccm hawataendekeza siasa zao za majitaka na kuacha bunge lipate spika anayekubalika, si na wabunge tu bali pia na wadau wengine hasahasa wananchi wote. Nadhani umeona reaction ya watu baada ya mzee wa vijifedha vya yatima kutangaza kuwania uspika. Tukiweza kuvuka salama huo mtihani, basi matarajio ni makubwa sana.
 
Yatawezekana kweli yote hayo Mbele ya CHENGE!???? tunaweza kupata bunge la KIBABE SANA never seen!
 
Back
Top Bottom