Nundu_Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 811
- 349
Huyu aliyepo hii leo ndiye asiye kuwepo badae na asiye kuwepo ndiye aliyepo. Hiki unachokiona leo siyo hicho walichokiona waliokuwepo, lakini ndiyo hicho kilichopo, ambacho kila aliyekuwepo, anayekuwepo na atakaye kuwepo anacho.
Wewe upo kwasababu wao walikuwepo na kwasababu walikuwepo na wewe upo na hivyo wote mpo.
Ukisema kwa sababu walikuwepo hivyo hawapo sasa maana yake na wewe haukuwepo na haupo sasa. Kama unasema walikuwepo, lakini sasa hawapo maana yake wewe pia hukuwepo ndiyo sababu unaona hawapo.
Ukiwa mwanadamu tayari umekuwepo na hivyo haiwezekani kwamba hautakuwepo.
Mtu aliyepo anawezaje kusema hayupo angali yupo? Vivyohivyo kwa aliyekuwepo atawezaje kutokuwepo? Aliyekuwepo ndiye aliyepo nae atakuwepo. Vivyohivyo kwa aliyepo ndiye yupo na atakuwepo.
Kama huyo hayupo maana yake na wewe haupo, lakini kama wewe upo na yeye yupo. Unawezaje kusema, yeye hayupo, lakini wewe upo?
Kama mtu huzaliwa na aliye kuwepo na yeye huyo anaezaliwa huwapo nae akisha kuwapo huzaa atakae kuwepo. Sasa ni nani kati hawa anaeweza kudai huyu hayupo?
Hivyo hakuna awezae kuwepo kama aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuwepo hajaweza kuwepo na hivyo aliyekuwepo yupo, atakuwepo na kwasababu yupo nasi tupo.