Kuweni makini na wanaowaahidi ajira humu kwa kuweka namba za simu

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
19,739
10,067
Wadau kutokana na kuwa na tatizo kubwa sana la ajira, vijana tumekuwa tukimnyenyekea yeyote tu anaetangaza kuweza kukupa ajira..

Humu jukwaani kuna jamaa mmoja anaweka sana namba yake ya simu na kusema atafutwe, nimejaribu kumpigia simu ili nijue hasa ana deal na nini!

Kwa haraka haraka nilijua yupo Dar tuu!

Jamaa kapokea, baada ya salam na utambulisho siku hiyo hiyo kaniambia tukutane ukumbi wa JK Nyerere posta kuna semina tena na elfu tano kiingilio! Dah! Nikamuuliza ni biashara/kazi gani hiyo ina kiingilio?? Jamaa kaongea vitu vingi mnoo nikajua tu ni forever living.

Kanitumia video whatsapp ya dk 30 akiniambia jinsi watu wanavyoingiza mil 20 kwa mwezi kupitia forever living. Kuweni makini.

Biashara ya kuzungusha alovera mjini na kuunganisha watu si rahisi hivyo. Huyu jamaa ID yake inaanza na herufi W.
 
Kuweni makini
Mwingine yupo wa kike... ID yake inaanza na herufi C...
Jaman hakuna ajira rahisi rahisi labda uamkie bahati
 
Kuweni makini
Mwingine yupo wa kike... ID yake inaanza na herufi C...
Jaman hakuna ajira rahisi rahisi labda uamkie bahati

Wataje mkuu,
Maana kuna wengine ni watu wema tu,
Ila wataogopwa kwa kuwa tu majina yao yanaanzia na "C."
 
Wataje mkuu,
Maana kuna wengine ni watu wema tu,
Ila wataogopwa kwa kuwa tu majina yao yanaanzia na "C."

Huyo wa W anajiita Wealthier basi pia mshukuruni kama huyu ni agent kweli wa forever living maana wengine ni vibaka hawana imani hata kidogo. huyo wa C..... SIJAKUTANA NAYE KTK POST LABDA MDAU ATAJE KWA MANUFAA YA WADAU
WHAAT???....Mother Fanta!! its a last word your mom provoked in my Bed :cheer2::bathbaby:
 
Nashukuru sanaaa umemtambulisha vizuriii. Hii inamaanisha huyu jamaa si tapeli.

Umechukua namba yake umempigia yy akakwambia sababu ya yeye kutaka atafutwe na evidence ni hiyo video aliyokutumia sasa hapo ana ubaya gani mpaka unatangaza eti watu wawe makini kwani nn maana ya kuwa makini?

Ww ungesema tu kuwa nimeona mm binafsi siiwezi hii biashara. Ondoa kabisa hiyo imani ya kudhani kitu usichokiweza wewe bac wooooote hawakiwezi.

Wewe unaweza usiwe na shida nayo kwa sababu mbalimbali labda mtoto wa mama au una kazi nzuri kiasi kuwa huna shidaaa.
Wallet yako si sawa na ya wenzio.

Labda utuambie kwenye video umeona kipi kibayaaa? hebu itupie hapa na ss tuioneee.
Maana naona unafurahishwa na hizi kelele za watu kutafuta ajira. Binadamu tuna vipaji tofauti cha kwako ni tofauti na cha fulani hii inamaanisha kile usichoweza wewe mwingine anakiwezaaaa. Ndio maana wapo wanaoifanya hii biashara ndio maana wanaingiza hizo 5mil ulizosema.

Imeandikwa maskini hawatakoma katika nchiii. Ili hili andiko litimie lazima watu wa aina yako muwe.

Wallet yako na ya mwenzio nina amount tofauti so unavyowashawishi wasifanye kazi waoneshe njia mbadala ya kuwaingizia kipato kama kweli wewe una nia njema la sivyo acha kila mtu atumie kipaji chake alichopewa na Mungu!
 
muwe mnasema manataka kazi gani.. kuzungusha alovera mjini ni kazi kama kazi nyingine mkuu,...
 
Imeandikwa maskini hawatakoma katika nchiii. Ili hili andiko litimie lazima watu wa aina yako muwe.
Mkuu nimeyaelewa sana maelezo yako na mizuka yako ya utafutaji, nimewaelewa pia wanaojaribu kuwakatisha tamaa watafutaji kwenye ulimwengu huu mgumu wenye watu wagumu.

Ila maandiko mengine ni upuuzi wa mchana kweupe, kumbuka kitabu hiki ndicho kilidai kuwa dunia ni bapa na sio duara na baadae ikagundulika ni urongo mtupu. Kwa vile umeanzisha session ya maandiko, Mtakatifu Marx aliandika kwenye Manifesto ya Chama cha Kikomunisti kuwa inawezekana kumaliza umasikini kama kila mtu atafanya kazi na tutakomesha unyonyaji... Nasikia Kuba wanakaribia kuumaliza umasikini, ujinga walishafanikiwa.

Mtakatifu Nyerere nae akasema kuwa utajiri wa watu sio maendeleo, ni matokeo ya mgawanyo usio sawa wa rasilimali na mapato... Ndio maana hata taifa masikini lina matajiri wenye akaunti nje na taifa tajiri lina masikini wasio hata na pa kuengesha mbavu.

Tuendelee kuimarishana kifikra!
 
Back
Top Bottom