Kuweni makini: Kondomu hazizuii maradhi na mimba kwa 100%

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Naandika uzi huu kuwafanya mchukue tahadhari zaidi ktk maisha. mara nyingi watu wanatumia kondomu wakitumaini sana wataepuka maradhi hasa gonjwa la ukimwi na pia kuepuka mimba isiyotarajiwa.

Kihistoria kondomu zilitengenezwa kwa ajili ya kuzuia mimba na baadae wakazifanya kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi ya maradhi. hata hivyo kondomu zimeonyesha kufeli kukidhi haja ya malengo hayo kwa asilimia kubwa.

Najua zina mchango hasa kuzuia mimba na kidogo kuzuia maradhi.wapo watu wengi wanaotoa ushahidi kuwa wameambukizwa maradhi na daima walikuwa waamini wazuri wa kondomu. we jiulize kama zinazuia maradhi kwa 100%, mbona ukimwi hauishi?hata mimba nyingi zinazotolewa leo ukiwahoji wahusika utasikia 'kondomu tulitumia lakini tunashangaa kuna mimba'. kumbe hizi kondomu sio za kuziamini kwa 100%.

USHAURI:
1. Kuwa mwaminifu kwa mwenzio wa ndoa ili kuepa maradhi

2. Kuwa na mke/mume mmoja ni nzuri zaidi kuliko wengi

3. Tumia njia asili za uzazi wa mpango(NFP) ambazo ni za uhakika zaidi

4. kabla ya kuoana, wachumba wapime afya zao na hasa maambukizi yanayoletwa kwa njia ya ngono.

5. acha maisha ya upekee kama sio wito wako. kaoe/kaolewe.
 
Acha kukurupuka na mabandiko yasiyo na reference wewe, huo uchunguzi wako umeufanyia maabara ipi?

Kama hujui kuvaa condom uliza watu wazima tukuelekeze na sio kusema condom haizuii mimba, au unavaa mfuko laini unachanganya mambo wewe?
 
Hapana kondom kwa 100% inazuwia mimba, hao wanaosema walipata mimba wasiwadanganye wenziwao, usishangae anaenda kubemendwa na mtu bila kinga halafu anakuja kusema alitumia na kupata mimba.
 
"Walioamini kuwa UKIMWI upo, ndiyo hao leo wanaishi kwa hisia za Babu" - Young Killer
 
Acha kukurupuka na mabandiko yasiyo na reference wewe, huo uchunguzi wako umeufanyia maabara ipi?

Kama hujui kuvaa condom uliza watu wazima tukuelekeze na sio kusema condom haizuii mimba, au unavaa mfuko laini unachanganya mambo wewe?
sijasema hazizuii kabisa bali sio kwa 100%. soma uzi wote kwa kuelewa na usiishie kwenye heading tu. asante na kuwa mwangalifu na hizo kondom.
 
575196efa61e2c8878efeeb33b9ce6fa.jpg
 
Acha kukurupuka na mabandiko yasiyo na reference wewe, huo uchunguzi wako umeufanyia maabara ipi?

Kama hujui kuvaa condom uliza watu wazima tukuelekeze na sio kusema condom haizuii mimba, au unavaa mfuko laini unachanganya mambo wewe?
Hahaa mweleze huyo... naona mkuu umemshukia!!! Na id yako vinafanana na ulichocoment
 
Back
Top Bottom