maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,277
- 15,522
Hali ya Serikali ya sasa si rafiki kwa uwekezaji Tanzania kutokana na mazingira yaliyoonekana kuwa mazuri awamu iliyopita kutoweka ghafla na kuacha wawekezaji wengi njia panda huku wengi wakishindwa kuendesha biashara na hata kuamua kuzifunga. Tayari Hotel tano zimeshafungwa mpaka sasa na taarifa zinadai kuna hotel nyingine 150 kufungwa siku za mbeleni. Akiongea na The Citizen mmiliki wa Hotel ya Kifahari iliyopo Bagamoyo ijulikanayo kama Green Park Village Bwana Slim Slim alisema anajuta kuja kuwekeza nyumbani maana mazingira ambayo wao kama Diaspora waliahidiwa na Serikali iliyopita hayapo tena. Mtanzania huyo mzaliwa wa Bagamoyo alieishi Norway kwa zaidi ya miaka 20 alisema alishawishika kuja kuwekeza nyumbani kutokana na juhudi za Serikali iliyopita kuonesha nia njema ya kuwataka warudi kuwekeza nyumbani. Kwa sasa hali imekua tofauti kabisa na serikali haifanyi juhudi yoyote kuonesha nia ya kusaidia wawekezaji na kuacha wengi wa wawekezaji wakihaha nini cha kufanya. Kwa sasa mmiliki wa hotel hiyo yupo katika wakati mgumu baada ya kuuza kila alichokuwa nacho Norway na kuja kuwekeza Tanzania na badala yake kushindwa kabisa kufanya biashara hali iliyopelekea hotel yake kutangazwa kupigwa mnada jumamosi hii. Inasikitisha kuona mkopo wa milioni 900 tu unapelekea kuuzwa kwa hotel ya shilingi Bilioni 5 tena kuuzwa kwa bei ya kutupa kitu kinachoonekana kuwa hujuma kwa kuwa hakuna chombo chochote cha serikali kinachoonesha kuingilia kati. Hali ni mbaya kwa mabenki yote kwani kwa sasa hakuna benki hata moja iliyokubali kununua mkopo huo licha ya kuzunguka kwenye mabenki yote nchini.
http://www.thecitizen.co.tz/News/Ag...llion-hotel/1840340-3895014-8oj5mo/index.html
http://www.thecitizen.co.tz/News/Ag...llion-hotel/1840340-3895014-8oj5mo/index.html