Kuweka na kutoa shilingi kwenye Mshahara wa Waziri

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,598
2,000
Wakuu, hakuna mtu anayejua kila kitu,

Katika bunge letu, kuna kitu mimi nimekuwa nikikiona mara kwa mara hasa wakati wa upitishaji bajeti na sijakielewa vizuri hadi sasa lakini bila shaka kutakuwa na wanaokielewa vyema.Ni kuhusu "Kutoa shilingi na kurudisha kwenye mshahara wa waziri".
Ninaomba kwa anayejua atujuze nasi tupate kuelewa juu ya mambo yafuatayo:

(a) Kutoa shilingi kwenye mshahara wa waziri maana yake kiuhalisia ni nini hasa?

(b)Ni nani anayepanga mshahara wa waziri? na je mshahara wa waziri unapitishwa na bajeti, au unapitishwa kivyake? yaani bajeti inaweza kupita bila mshahara wa waziri?

(c) Ni madhara gani yanayotokana na kutoa shilingi kwenye mshahara wa waziri na madhara hayo huwakumba kina nani hasa?

(d) Ili kutoa shilingi kwenye mshahara wa waziri kuweze kuwa na madhara yaliyokusudiwa; ni wabunge wangapi wanatakiwa kutoa shilingi?

(e) ni sababu zipi kimsingi zinamfanya mbunge awe na haki ya kutoa hiyo shilingi?

(e)Katika historia ya bunge letu;Huu "Utoaji shilingi" huu ushawahi kuleta madhara fulani? kama hapana, tunaweza kuwa na mfano wa bunge lolote duniani ambalo jambo hili lilishawahi kuleta madhara/matokeo yaliyokusudiwa?

Nadhani tukipata elimu juu ya haya, tunaweza pia kupata na majibu ya maswali mengine, au kuwa na maswali mengine ya nyongeza.

Kwa kila mwenye kujua, anakaribishwa!.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Ninadhani kama tungekuwa na BUNGE lenye sauti na wabunge wote wakawa wanajua nafasi yao ya kuingia BUNGENI,basi inamaana kwamba ukishika shilingi ya mshahara wa waziri basi na wote mkawa na malengo ya kitaifa basi bajeti ya waziri husika haipiti mpaka mambo yanayohitajika kubadilika yapewe kipaumbele na kuirekebisha bajeti husika.Hii ni kwa mtazamo wangu.
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
597
250
Siku hizi kila mbunge akisimama 'natoa shilingi.' Ukitoa shilingi tafsiri yake ni kuwa fungu la mshahara wa waziri litapitishwa bila shilingi moja. Ni sharti mtoa hoja atoe hoja mahususi ambayo itajadiliwa ndipo bunge litaamua kwa kupiga kura kama kawaida. Kwa kawaida ni fedheha kwa waziri bajeti yake kupita bila sh moja hvyo ni vema akatetea ili irudi. Zamani ukisikia mbunge anatoa sh waziri alikuwa anahangaika kujiokoa!
 
Mkya

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
668
0
Mbona mnaleta porojo hapa

Nini maana ya kutoa sh. Kwenye bajeti ndiyo swali Kama huna jibu pita kushoto Kama mm maana sijui
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
597
250
Mbona mnaleta porojo hapa

Nini maana ya kutoa sh. Kwenye bajeti ndiyo swali Kama huna jibu pita kushoto Kama mm maana sijui

Acha ukali soma sentensi yangu ya pili imetoa maana ya kutoa shilingi. Mengine yalihusu namna ya kutoa shilingi rejea maswali ya mtoa mada.
 
Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,417
2,000
Siku hizi kila mbunge akisimama 'natoa shilingi.' Ukitoa shilingi tafsiri yake ni kuwa fungu la mshahara wa waziri litapitishwa bila shilingi moja. Ni sharti mtoa hoja atoe hoja mahususi ambayo itajadiliwa ndipo bunge litaamua kwa kupiga kura kama kawaida. Kwa kawaida ni fedheha kwa waziri bajeti yake kupita bila sh moja hvyo ni vema akatetea ili irudi. Zamani ukisikia mbunge anatoa sh waziri alikuwa anahangaika kujiokoa!

Ni kweli kaka maana nimeona kwa sasa kila mbunge anashika shilingi na kuachia lkn nadhani sbb ni kwa sbb ya kura maana hata ukiwa mpinzani ukishikilia shiringi kwenye kura chama tawala watakuangusha tu
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
597
250
Ni kweli kaka maana nimeona kwa sasa kila mbunge anashika shilingi na kuachia lkn nadhani sbb ni kwa sbb ya kura maana hata ukiwa mpinzani ukishikilia shiringi kwenye kura chama tawala watakuangusha tu

Ni kweli mkuu.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,598
2,000
Ni kweli kaka maana nimeona kwa sasa kila mbunge anashika shilingi na kuachia lkn nadhani sbb ni kwa sbb ya kura maana hata ukiwa mpinzani ukishikilia shiringi kwenye kura chama tawala watakuangusha tu
sasa kama hilo linajulikana, kuna haja gani ya kushikilia halafu baadae unaachia, sio kwamba wala hapakuwa na haja ya kushikilia? yaani bado kuna maswali ya kujiuliza hapa!
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,049
2,000
HUWA wanabana baadae wanaachia,cheazea wazee wa ndioooooooooooii
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,656
2,000
Suala la kutoa ama kurudisha shilingi ni kiini macho na mchezo wa kuigiza...
Wonders shall never end in Tanzania.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,699
2,000
Kwa Mtazamo wangu kutoa shilling ni kutokubaliana na baadhi ya vifungu vya fedha vilivyopo kwenye bajeti ya wizara husika...opposite is the same.(Kurudisha-kukubali)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom