Kuweka mikono mbele ya Kiongozi ni dalili ya busara, unafiki au uwoga?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Nimekuwa nikiwaona Watu wengi sana pale wanapokuwa wamesimama na Kiongozi yoyote wa nchi hasa Marais katika nchi nyingi sana hapa duniani wakiwa wameweka mikono yao mbele tena wakiwa ' wapole ' na wana ' adabu ' zote kiasi kwamba hata ikitokea kuna ' Siafu ' anamng'ata ' au kaona ' Nyoka ' hawezi kushtuka na kuiondoa hiyo mikono.

Sasa naomba kuuliza je kuweka mikono mbele ni dalili ya nini kati ya haya yafuatayo?

  1. Je ni busara iliyotukuka?
  2. Je ni Unafiki uliotukuka?
  3. Je ni Uwoga uliotukuka?
Uwanja ni wenu wana ' Jamvi ' na karibuni ' mtiririke '.

Nawasilisha.
 
0aad8ac99bed9df93a926ccba4c65b6f.jpg


Nafikiri ni kuonyesha kuheshimiana tu
 
Hiyo ni heshima na sio woga viongoz hasa Wa kisiasa wana namna wanakaa mbele za watu siyo kusimama kama unakojoa mbele ya raisi,kitumbua kitaingia mchanga yaan ndiyo kaliba za viongoz kwa ufupi..
 
Masikini mleta mada kawa banned(anatumikia adhabu japo sjui ni kwa sababu ya hii thread au nyingine!!..)
skuhzi ban zipo nje nje..
 
Ni aina ya body gesture inayoashiri utii.hii hata unaposali unaeza kufanya hivyo.ishara hizi hata wanya wengine wanazo kwa mfano mbwaa hufyataa mkia kuonesha utii au uoga au kutojiamin mahala alipo.

Lakini sio kuwa ni unaafiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom