Kuweka anwani za makazi kwenye makazi holela ni kupoteza fedha

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Ukienda jijini Mwanza ukipita kwenye makazi holela unakuta vibao vimewekwa eti anwani za makazi, huku ni kupoteza pesa yetu bure. Unapita kwenye njia zilizochangamana mara umeibuka junction moja kimewekwa kibao cha anwani ya makazi.

Ushauri
Anzeni kwa kutuwekea mitaa inayoeleweka tumieni hizo gharama za sasa kuchonga barabara mitaani, mkiweka majina kwenye mitaa inayoeleweka sasa inakuwa rahisi na vibao vinakuwa anwani inayoeleweka. Kwamba mtu anaweza kuelezea mtaa wake kuwa ni barabara fulani, mtaa fulani na fulani.

Kwa sasa kinachofanyika kwenye makazi holela wala huwezi kutoa anwani yoyote labda wale tu wa barabara kubwa tu.
 
Akili ya Mabula na Lukuvi hiyo.
Wamebuni dili wote mmoja kaondoka mwingine kapanda. Kufa kufaana
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Maeneo yaliyojengwa bila mpangilio kama Manzese, nyumba zithamanishwe wenyewe walipwe chao kisha waondoke kwa muda kupisha ujenzi wa maghorofa.

Ujenzi ufanywe kwa mpangilio kulingana na mipango miji, yatakapokamilika wakazi wa awali wapewe kipaumbele, kwa kuuziwa au kupangishwa nyumba mpya kama ilivyofanyika kwenye kota za Magomeni.
 
Back
Top Bottom