Kuwe na Ukomo wa Ubunge Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwe na Ukomo wa Ubunge Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ubungoubungo, Jul 30, 2009.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ubunge mwisho miaka 10, as it's for the president!

  Ninasajesti mtz yoyote anayetaka kugombea ubunge, afanye hivyo, akishinda mara moja abakiwe na mara yake moja kama ilivyo kwa rais kuwa na term mbili tu.

  NAFIKIRI HII ITASAIDIA sana watz kuangalia nini mtu amefanya kwa miaka hiyo kumi, na kama ameboronga, basi akamatwe.

  Nasema hivi, kwasababu nahukia sana kuona mbunge tangu nimezaliwa miaka ya sabini hadi leo nina miaka 30 yeye bado tu ni mbunge, akiboronga bado tu anachaguliwa, wananikera.

  Mnasemaje wajameni?
   
 2. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wakuu hili suala la kuwa na wawakilishi wa majimbo (Wabunge) wa kudumu ni lini litapata tiba?

  Kwanini tusiwe na ukomo wa ubunge Tanzania?

  Nawakaribisha wadau tutoe maoni na pia tushauri ni nini kifanyike katika hili, tuendelee kutokuwa na ukomo wa hawa wawakilishi au tuwe na ukomo?

  Nawasilisha.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe kabisa kwamba badala ya kuwa na Wabunge wanaoufanya Ubunge wa jimbo kama mali yao ya kurithi (juzi nilisoma mahali mbunge mmoja amekuwa mbunge kwa miaka 25 sasa) kuna umuhimu mkubwa wa kuwema ukomo kwa Wabunge wa kuchaguliwa na Wabunge wa kuteuliwa usiwe zaidi ya awamu mbili kama ilivyo kwa Rais wa Tanzania. ZiiZiiM hawatalikubali hili liwekwe kwenye katiba maana wanajua fika kwamba, kwa mfano hili likiwekwa kwenye katiba ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa na Wabunge wengi ndani ya Bunge kama chaguzi zitakuwa halali, maana sasa hivi ZiiZiiM (Chama cha mafisadi) wanadai wana "mbinu" zao zinazowasaidia kushinda chaguzi nyingi lakini ukweli ni wa kwamba wanatumia vyombo vya dola kuwanyanyasa Viongozi wa upinzani, wanachama wao na hata kuiba kura ili kuhakikikisha wanashinda chaguzi nyingi.

  Pamoja na hayo bado kuna umuhimu mkubwa wa kubadilisha katiba ili Bunge letu lipate Wabunge wapya kila baada ya awamu mbili badala ya Wabunge wenye mawazo mgando ambayo kwa kiasi kikubwa wamechangia katika kuvuruga sana maendeleo ya Tanzania.
   
  Last edited: Sep 12, 2009
 4. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapa kwenye katiba naona ndo pana utata kwani wanaotakiwa kufanyia mabadiliko si ndo hao waliogeuza ubunge kama ajira yao ya kudumu? Nadhani haitakuwa rahisi kwa wao kulikubali hili.Je,hakuna njia nyingine ambayo wa Tanzania tunaweza tumia kujikwamua na hili?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280

  Mvina, labda kingine ni vyama vya upinzani kususia chaguzi zote na kuiomba jumuiya ya Kimataifa na mashirika mbali mbali ya maendeleo duniani kuishinikiza serikali kwa kuinyima misaada na mikopo mbali mbali mpaka hapo katiba ambayo inakubalika na vyama vya upinzani na ambayo itakuwa inatoa kwa vyama vyote nafasi sawa za kuweza kushinda chaguzi na hatimaye kuingia madarakani, hii katiba iliyopo inatoa advantage kubwa kwa Ziizzim na pia hukiukwa, kwa mfano pale vyombo vya dola kama polisi, FFU n.k. wanapotumiwa na Serikali kama kitengo cha chama tawala kwa kuwanyanyasa kwa aina moja au nyingine Viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani.

  Naamini shinikizo la jumuiya ya kimataifa linaweza kuharakisha nchi yetu kupata Katiba mpya.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wazo ni zuri la ukomo wa wabunge lakini kuishirikisha Jumuiya ya Kimataifa inaweza isizae matunda. CUF walijaribu mbinu hii hasa kuhusu muafaka baada ya uchaguzi lakini bila mafanikio. Kwa nini wabunge wa upinzani wasitoe muswada binafsi?
   
 7. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii pia inawezekana lakini naona kama hata wabunge wetu wa upinzani hawapo tayari kwa haya mabadiliko au wenzangu mnaonaje? Kama waliweza ufisadi wa richie..kwanini lisiwe hili?
  Pia naona hili liendane na mada ya kuwa baraza la mawaziri liundwe nje ya bunge ni kimanisha mtu akiwa mbunge hawezi kuwa waziri at the same time.
   
 8. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Babu ataka kusema!

  Nakushukuru kwa mchango wako wa dhati kwa muda wote sijapata hapa jF umeonyesha ukomavu. Katika kuchangia ili kuondoa rushwa na kuleta dynamics katika ubunge napendekeza ubunge akishatumikia vipindi viwili kama ilivyo Rais anapaswa kuachia ngazi. Jimbo litarajie sura mpya after every 10 years

  Wabunge hawapaswi kufanya marathon as if wanaleta maendeleo but wamekuwa ni moja ya chanzo cha kukua kwa rushwa na imbalance distribution of the National Cake. Let have a balanced mix. Wanapita chini kujimegea pesa kutoka Hazina in the most uncivilized manner.

  Na kwa sababu Watz wengi elimu ni kwa kijiti they virtualy know nothing ndio maana kuna mpumbavu mmoja alimshukuru Mkwere for a certain development project uliofanyika huko kwao Sengerema kwani anatoa ahadi when he thiks of kuwa Matonya.

  We did not choose the president to travel looking for peanuts wakati anawaachia akina RA, MENGI na Subash Patel kufanya real estate busness NA biashara lukuki pasipo kulipa kodi . In the whole world gvt's survive only on Tax payers money na sio kufanya utalii wa kifuska kwenda kuomba while Tanzania is much much reacher than the states he usually visits kutembeza bakuli.

  Babu hivi kwa akili yako kuna mbunge anayeweza leta maendeleo kama people are not willing or ready for development? He can't of course sasa hiyo dhana ya mbunge kuleta maendeleo kwenye jimbo inatoka wapi?
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hili jambo tulishalipendekeza kuanzia BCS hadi sasa JF........kama sikosei kuna mheshimiwa mmoja aliwahi kutaka hiyo hoja iongelewe.......aisee alipigwa vita kama mpira wa kona.......bado nazidi kusisitiza...........inabidi tufikie mahali tuweke ukomo kwenye ubunge, na pia turuhusu Rais aweze kuchagua watu wenye uwezo kwenye baraza la mawaziri hata kama sio wabunge.........we can still debate on this........
   
 10. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Hapa nitakuwa na wazo tofauti. Infact kwa Rais kuwa na miaka kumi (two terms); ni sawa kabisa; kwa sababu Rais wa Tanzania ana madaraka makubwa sana kumuondoa kwa kura ni ngumu sana.

  Kwenye ubunge tuendeleze ushindani. Ukiona kuwa mbunge anakaa sana kwenye kiti cha bunge lake basi lazima ujiulize wananchi wengine wa jimbo hilo wana mwamko upi. Kumpata mwakilishi mzuri wa Bunge lazima atoe tactics mpya kumpita yule incumbent. At least kila jimbo lina vijana, wazee, wanawake kwa wanume wasomi; kama hawa watu hawana mwamko na hawa-fight for their constituents, wasitegemee tu constution ifanye ubunge uwe na ukomo?

  Kuna mifano: Kuna Mbuge wa Mtera, kuna mbunge wa Njombe (Makweta), Sumbawanga (Mzindakaya) hawa huwa hawana upinzani mkubwa, simply kwa kuwa watu aidha hawajitokezi, wavivu kufikiri, au waoga. Je Kwa nini turuhusu tu mteremko. To get at the top we should compete on what we will deliver, tusiwekeane ukomo; hapo ndipo tutawapata the best! Akitokea mtu apambane na Malecela au Makweta au Mzindkaya na kuwabwaga, basi mbunge kama huwa analeta confidence ya kwake na hata ya wale anaowawakilisha.
   
 11. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbona hujataja majina yao? Ni akina nani hao?
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mh ningependa kupingana na wewe kwenye hii point. Wabunge ni chaguo la wananchi, hivyo kama wananchi wa jimbo wanampenda mbunge fulani, nadhani iwe haki yao kuamua kama wanataka awe mbunge wao kwa miaka 5,10,20 au hata 50. Ubunge ni ofisi yenye direct accountability to wananchi, hivyo sidhani kama ni sawa kuingiliwa na katiba. Kama mnataka ni kupunguza election cycle to 4yrs/3yrs, kwa kusudi kuongeza uwajibikaji. Lakini ubunge ubaki choice ya wananchi. Kama mnaona wamekosea, basi ni haki yako kwenda kugombea na huyu mbunge na kusambaza sera zako mbadala. Hiyo ndo njia ya demokrasia. Msipende kila solution itoke kwenye katiba.

  Pia sidhani kama kuweka limit ya muda wa mbunge kutupunguza nguvu ya CCM. Kwani jambo hili litazuiaje kurithishana? Litazuiaje rushwa kutembea? Kwani incumbent anashindwa kuamua nani achukue ubunge pale muda wake unapoisha na hivyo kutoa rushwa na kumsaidia kuchaguliwa? Swala la ubunge nadhani ni wananchi wenyewe kuamka na kujua umuhimu wa hii nafasi katika utawala wa nchi.

  Wakishaelewa hili, basi watafanya maamuzi yao kwa busara. Lakini kusema kuwanyima haki ya kuchagua mbunge kwa muda na vipindi wapendavyo wao ni kuwanyima haki yao.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  Chagua la Wananchi baada kupewa pilau, beer, soda na vijisenti vichache na wakishapigiwa KULA na wananchi wanahama majimbo yao ya uchaguzi mpaka karibu na uchaguzi mwingine ndiyo wanaonekana tena jimboni kwenda kuomba KULA (isomeke KURA) kwa awamu nyingine. Na majimbo hayo hayana maendeleo yoyote miaka nenda miaka rudi na bado mbunge akae kwenye Ubunge miaka 25 au zaidi eti kwa sababu ni "chaguo la wananchi". :confused:
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  This is not possible for now kwa sababu kwa siasa za Tanzania zilivyo mtu kuwa waziri ni lazima au mbunge na kama mtu ana aspire kufikia zile ofisi tatu kuu za nchi basi ni lazima apitie ubunge. Sasa ukiweka kikomo kwenye ubunge it means wale wabunge kwenye there 20's au 30's career zao zita isha hata kabla hawa jiandaa vizuri kuwa maraisi. Unless some things change hii kikomo ya ubunge ni ndoto.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  MwanaFalsafa1, hili la Waziri ni lazima awe Mbunge nalo ni tatizo lingine hili ambalo inabidi lirekebishwe. Hakuna ulazima wowote wa Waziri kuwa ni lazima awe Mbunge. Miaka yangu mingi ya kufuatilia vikao vya Bunge utakuta Wabunge ambao waliwahi kuwa mawaziri na baadaye kupoteza uwaziri wanakuwa waongeaji wazuri sana bungeni katika kuikosoa serikali katika maamuzi yake mengi, lakini mara wanapoutwaa Uwaziri basi wanakuwa Kimyaaaa na kufuata mstari wa Serikali.

  Nakumbuka hata miaka ya nyuma wale Wabunge ambao walikuwa wanaichachafya Serikali bungeni wengi waliishia kupewa Uwaziri ili kupunguza makali yao ya kuikosoa Serikali. Hivyo kwa maoni yangu hili nalo la Waziri ni lazima kuwa Mbunge linastahili kabisa kurekebishwa haraka sana.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I agree with you 100% mkuu. There is no need for a MP to be a minister. It causes a conflict of interest. Maana kazi ya mbunge ni kukosoa serikali na kazi ya waziri ni kuitetea serikali. Sasa where does one drw a line between being a minister and being a MP? Na je mtu akisha kuwa waziri na baadae akawa tu mbunge wa kawaida will he have the moral authority to say anything negative about the government?
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  Thank you Mkuu MF1!
   
 18. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeupenda mchango wako lakini bado ukumbuke kuwa kuna baadhi ya majimbo watu wanaogopa kupambana na hawa wazee ambao wengi wao wana hata zaidi ya miaka 25 bungeni kwasababu tu watu wanaogopa kupoteza nadhani umenielewa.Kwa kuweka ukomo nadhani hata mambo ya kishirikina yanaweza pungua kidogo 'cause mtu si rahisi akampoteza mwenzake kwa kitu cha 10yrs.
  Pia si wote wanawakilisha haya majimbo kwa miaka mingi wanashinda kihalali wengi ni rushwa kwavile tayari wamejilimbikizia mali so kijana ambaye labda ndo ametoka chuoni hawezi kupambana nao kwavile atategemea sera zake wakati mwenzake ni sera pamoja na rushwa.
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  either waruhusu Mgombea BINAFSI au waweke Ukomo wa Ubunge........

  Mkuu IO i really feel/understand what you are trying to say........unajua hizi demokrasia inafikia mahala zinatakiwa ziwe generic in a way ku-suit mazingira yetu...........hizi demokrasia tulizochukua jumla jumla toka huko west.....lets review them thoroughly na kuona jambo lipi latufaa....ili mradi tusiharibu maana ya demokrasia.........

  hili pendekezo linaweza kuboreshwa hata kwa kusema "say" ukishamaliza vipindi vyako viwili vya ubunge waweza kurudi tena kugombea baada ya vipindi viwili kupita........intermittently way.....kwa nini nasema hivyo

  ..........Kazi ya ubunge yapaswa kuwa ya kujitolea kuwatumikia wananchi kufikia malengo ya maendeleo yao..........hali ilivyo sasa wabunge wanatumia nafasi hizo kujinufaisha badala ya kufanikisha malengo ya wananchi..............

  ............. siku moja JK aliwaambia wananchi wa Mbeya (wakati ule alipolaumiwa kuwa hajawatembelea toka uchaguzi uishe na kuwa hawajali)......kuwa kama ningekuwa siwajali nisingewapa Mawaziri wawili Senior!!!....can you imagine such a statement!!!!.......kama alivosema Mwanfalsafa1...tuchague moja uwe mbunge au Waziri.....otherwise ni kujidanganya linapokuja jambo la checks and balances..........

  .......unakuta hata tumepoteza walimu wa vyuo na wataalamu wazuri tu kisa.......kupigania ubunge (kwani ubunge unalipa kuliko kufundisha) na siku moja who knows "my friend" anaweza kunipa uwaziri........

  Kuimarisha jimbo lako si lazima uwe Mbunge au Waziri, hizi nafasi ni pure kwa ajili ya kujitolea.....kitu ambacho ni tofauti sana na hali ilivyo sasa.........HIYO NI EXPERIENCE AMBAYO KILA MMOJA WETU HAPA JF ANAWEZA KUWA SHAHIDI........

  Don't get me wrong.........kuna wabunge ambao kweli nia yao ni kujitolea kuleta maendeleo na kazi zao zinaonekana...........tena sio zile za "FAVOUR" kama za akina Chenge na Meghji.........

  ........watu wapo tayari kupigania constitutents zao.......ispokuwa hii mambo ya kupitishwa na chama ina ukiritimba ambao kina "Mzindakaya" ndio wenye final say........na ndio maana KUNA UMUHIMU WA KUWA NA MGOMBEA BINAFSI...angalau ikitimizwa hiyo basi.....hii hoja ya UKOMO wa UBUNGE itakuwa haina uzito sana.........

  IO jaribu ku-imagine mwananchi wa kawaida unamletea achague CCM/CUF/CHADEMA/TLP/NCCR.....halafu wagombea waliopitishwa ndio kama akian "Guninita/Komba"..........unafikiri kwanini akina siye tusikate tamaa ya kuingia ulingoni

  .......trust me wakiruhusiwa wagombea binafsi utaona jinsi watu watakavyojitokeza........
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa tatizo ni mbunge au wananchi? Wape wananchi elimu ya kujua kiongozi bora, na kujua haki na majukumu yao. Nakumbuka nilipokuwa shule ya msingi tukijifunza lile somo la uraia. Nadhani lile somo lingeweza kuelekezwa zaidi katika kujenga misingi bora ya uraia, badala ya kujifunza waziri wa michezo, nk ni kina nani! Wananchi wengi hawajui hata ofisi mbalimbali za serikalii za mitaa na kazi zake. Mnategemea serikali kuu ifanye kila kitu wakati mna serikali za mitaa za kuwaletea maendeleo katika level ya karibu zaidi na wananchi? anyway - this is beside the point. Tukirudi kwenye ishu, ni kwamba i dont see how ku-limit ubunge kutaleta ufanyaji kazi mzuri. Ubunge ni nafasi yenye umuhimu sana katika mfumo wa katiba, yenye direct link na wananchi. Na nadhani ibaki kuwa choice ya wananchi juu ya kipindi cha wabunge wao.
  Ukiwa Minister, lazima ukubaliane na serikali yako. the constitutional convention of cabinet collective responsibility hiyo. Kama hapendi maamuzi ya serikali yake, jiuzulu kama Mrema alivyofanya.

  mh, kazi ya waziri ni ku-impliment government policy katika department aliyo-incharge. Kwa hiyo yeye ana-act kama agent wa serikali. Tofautisha public service na government policy. Kwa mfano, CCM i-campaign on kupunguza bei za umeme. Basi wakishinda, yule anayechaguliwa kuwa Minister of Energy, kazi yake itakuwa ku-implement hizo campaign promises through that department. Sijui umenipata? Tatizo kwa Tanzania, yani civil services zimeunganika sana na Chama na Serikali. Utakuta Katibu Mkuu wa Wizara (a civil servant) na yeye ana-support CCM, au anahofia serikali na chama tawala. Hapa ndipo hali inakuwa ngumu. Watu kama kina Balali, nk, waliokuwa Benki Kuu walishindwa kusimamia kazi zao against serikali na kuruhusu Serikali ku-squander pesa za umma (EPA). Hivyo basi, kwa waziri kutoka bungeni, hii isiwe taabu. La muhimu ni kuelewa kwa undani how the whole mechanism works. Na hichi ndicho kitu watu wengi hawaelewi.
   
  Last edited: Sep 14, 2009
Loading...