Maria Nyedetse
JF-Expert Member
- Apr 24, 2021
- 657
- 1,485
Wanajamvi habari za usiku,
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari nyumbani kwangu na rafiki ambaye amenitembelea, nikaona taarifa ya walimu kuandamana kutoka jijini Mwanza wakimlalamikia mkurugenzi juu wa malipo yao ya kazi ya kukusanya taarifa za anwani za makazi. Nikashangaa inawezekanaje mlishakubaliana na kusainiana mkataba halafu baadala terms na malipo yanabadilishwa? Kwa nini Mwanza na si nchi nzima?
Hapa ndipo rafiki yangu ambaye anafanya kazi LGA [halmashauri moja hapa nchini] alipoanza kunisimulia madudu ya hawa watu wanaoitwa wakurugenzi na jinsi walivyo na power without check and balance.
Wakurugenzi wanateuliwa na Rais na wanafanya kazi chini ya baraza la madiwani lakini mkurugenzi huyu ndiye msimamizi wa uchaguzi uliowaingiza madiwani, ndiye anawalipa posho za vikao, ndiye mwenye maamuzi wapi mradi uende na wapi usiende. Technically yeye ni basi wa madiwani na sii kinyume chake.
Sasa story za jinsi wanavyozisasambua fedha za LGA ndiyo zilizonishangaza mimi.
Nikawa nawaza; kwanini wakurugenzi wasiwekewe targets to achieve kama zilivyo taasisi binafsi kama mapato, uwekezaji, transforming kilimo, mifugo na afya, elimu etc.
Namna wanavyo-motivate wafanyakazi badala ya kuwazuia wafanyakazi kuhama hata kama wanafanyiwa madhila.
Ikiwezekana nafasi hizi ziwe zitangazwa na watu kuomba na kusailiwa kulingana na uwezo wao na siyo kuteuliwa na rais pekee au wajadiliwe bungeni jina kwa jina.
Ni ngumu sana Rais kusimamia wakurugenzi wote nchini. Lakini pia waziri hana nguvu kwao kwa sababu mamlaka ya uteuzi ya waziri na mkurugenzi ni moja.
Maoni: Kuwe na namna nzuri ya kuwapata, kuwapima na kuwasimamia hawa watu!
Wenye uzoefu na LGA [halmashauri] leteni uzoefu wenu hapa, isijekuwa nimedanganywa.