Kuwe na mpango wa kuwezesha makundi haya

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Wale watumiaji wa daladala haswa maeneo ya mijini kama dare s salaam tunashuhudia vijana wengi kwenye vituo vya daladala wakiuza chenji kwa makondakta wa daladala na watu wengine wanaopenda kununua chenji hizo kwa ajili ya kazi zao za kila siku .

Mfano ukiwa na shilingi alfu 1 basi chenji yake atakuuzia kwa shilimi mia 9 au mia 8 hamsini vijana hawa wanaongezeka kila siku na kila kituo inaonyesha biashara hii inawalipa sana sijapata kujua kama biashara hizi zinasimamiwa na mtu au vikundi vyao wenyewe na kama vikundi hivyo vimesajiliwa au kama serikali za mitaa hiyo zina mpango wa kuwasaidia watu hawa .

Hata hivyo inaonyesha vikundi hivi vinafadhiliwa na kulindwa sana na wababe wa vituo au vikundi vingine ambavyo vinawatoza pesa wafanyabiashara wengine ambao wanafanya kazi kwenye vituo hivyo bila serikali za mitaa hiyo kujua au viongozi wake kuogopa kuwauliza chochote kutokana na kuhofia usalama wao na wa watu wao wa karibu .

Kama inaonyesha wanafanya kazi kwa kupata faida kama ninavyofikiria mimi , kwanini vikundi hivi visisajiliwe na kupatiwa mazingira mazuri zaidi ya kufanya kazi yao kuliko ilivyo sasa hivi ? tena hata benki zinaweza kuwakopesha watu hawa wakuwa kwenye vikundi vyao naamini wataweza kupata faida zaidi ya wanavyofanya sasa hivi .

Ni muhimu kwa wahusika kwenye mitaa hii wafikirie kuhusu vijana hawa isije ikawa wanahifadhiwa na wahalifu huko mbeleni ije kuwa balaa ,pia kuna wamachinga ambao wanafukuzana na mgambo wa jiji mara kwa mara hawa nao wawekewe mazingira mazuri ya kufanya kazi zao lakini sio kwa style ya machinga complex

Mfano hawa wamachinga kutokana na aina ya biashara walizonazo wanalazimika kutembeza mitaani , kwanini kusifanyike utaratibu mzuri wa kuhakikisha wamachinga hawa wanawekewa mazingira hayo ya kufanya kazi mbona wanaouza vocha za simu wanazunguka mitaani bila shida yoyote hakuna anayewasumbua ?

Ukiacha wauza vocha kuna wanaoshugulika na kusafisha viatu , kuna wauza magazeti , kuna wauza maji na biashara zingine ndogo ndogo hawa wote wanaweza kuwezeshwa kuhakikisha biashara zao zinafanyika katika mazingira bora zaidi kuliko kufukuzana na askari wa jiji kama ilivyo sasa .

Huwa nafarikija ninapoona vikundi vya wakina mama mitaani wanavyofanya kazi na biashara zao kwa njia za amani kwa kukopeshwa hela na benki mbalimbali au saccos humo mitaani , sasa hivi ni ngumu sana kukutana na wakina mama wanaokaa vibarazani wengi wapo kwenye shuguli zao wamewezeshwa na benki hizi au saccoss zao .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom