Kuwe na mjadala wa wazi kuhusu Katiba kati ya Chadema(Bara) na CUF (BLW)Znz

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Wana Ukumbi.

Nafikiri ni vizuri sana kuweka mjadala wa wazi kuhusu uundwaji wa katiba mpya na ufahamu wa katiba kati ya Chadema na CUF zanzibar. Na ningeshauri wahusika wawe Mh Abubakar Bakari na Mh Juma Duni Hadji (hawa kutoka Baraza la wawakilishi CUF Zanzibar na Tindu Lissu na Zitto au Mnyika au hata Prof Safari au Mabere marando au wote hawa.

Hapa nafikiri mtaona wazi kuchambuliwa kwa Katiba iliyopo na ile inayotakikana. Kwani kuna mengi ambayo naona Tindu Lisu anatumia kuinyonyoa Zanzibar bila kukutana na wachambuzi wazuri na mahiri wa siasa na sheria hususan mambo ya katiba.

WaTz mjaribu kushawishi kukutanisha watu hao muone uzuri na udhaifu wa vyama na taaluna zinavyotumiwa vibaya kwa jamii.

Andaeni mjadala huo.
 
Tatizo ni kwamba Wazanzibari wanaogopwa sana na magamba! Just imagine Katiba ya Muungano mpaka sasa inamtambua Waziri Kiongozi wa SMZ!
 
Tatizo ni kwamba Wazanzibari wanaogopwa sana na magamba! Just imagine Katiba ya Muungano mpaka sasa inamtambua Waziri Kiongozi wa SMZ!

Ndio maana nasema ni vizuri Chadema mbao ndio vinara wa kuichambua katiba napendekeza wapambanishwe na baraza la wawakilishu hususan wawakilishi wa CUF ambao ni Mh Abubakar Khamis Bakar na Mh Juma Dini Hadji na Chadema waweke watu wao hata wakiwa sita au sabaa ili kuuchambua kwa kina sana Muungano na nini cha kuweka katika katiba.

Kwani kwa sasa inaonekana Tindu Lisu amatamba pekee katika kuuchambua muungano kwa upande wa Bara. Na hivyo inakuwa waTz hawatendewi haki hata kidogo pasi na kusikia kutoka upande wa Pili.

Kama walivoweza kuwapambanisha Mbowe na Hamad rashid. sasa wawapambanishe hao hapo juu ili wananchi wajue mbivu na mbichi.
 
Ingependeza mjadala uwe na chama kilichopo madarakani yaani CUF na CCM na CCM na CDM.
Hiyo unayopendekza wewe ya CDM na CUF lengo na dhumuni lake ni nini hasa?
 
haki ya nani TUNDU LISSU anasumbua vichwa vya midebwedo zenji vibaya mno. walilokuwa wanalitaka ndilo lissu analowaambia, ajabu wanamgeuka kuwa anawatusi. mmmh!
 
haki ya nani TUNDU LISSU anasumbua vichwa vya midebwedo zenji vibaya mno. walilokuwa wanalitaka ndilo lissu analowaambia, ajabu wanamgeuka kuwa anawatusi. mmmh!

Zumbemkuu= Zumbukuku. Hivi wewe umeona Wazanzibari ni midebwedo sio. Chunga ulimi wako.
 
Zumbemkuu= Zumbukuku. Hivi wewe umeona Wazanzibari ni midebwedo sio. Chunga ulimi wako.

unajua maana ya midebwedo? midebwedo ni wale wote wasiopenda haki, kama wewe ni mmoja wapo u'mdebwedo tu, simaanishi znz hakuna watu wenye akili, wapo wengi tu na nawaheshimu sana. otherwise zumbukuku is also my name.
:tongue:
 
Wana Ukumbi.

Nafikiri ni vizuri sana kuweka mjadala wa wazi kuhusu uundwaji wa katiba mpya na ufahamu wa katiba kati ya Chadema na CUF zanzibar. Na ningeshauri wahusika wawe Mh Abubakar Bakari na Mh Juma Duni Hadji (hawa kutoka Baraza la wawakilishi CUF Zanzibar na Tindu Lissu na Zitto au Mnyika au hata Prof Safari au Mabere marando au wote hawa.

Hapa nafikiri mtaona wazi kuchambuliwa kwa Katiba iliyopo na ile inayotakikana. Kwani kuna mengi ambayo naona Tindu Lisu anatumia kuinyonyoa Zanzibar bila kukutana na wachambuzi wazuri na mahiri wa siasa na sheria hususan mambo ya katiba.

WaTz mjaribu kushawishi kukutanisha watu hao muone uzuri na udhaifu wa vyama na taaluna zinavyotumiwa vibaya kwa jamii.

Andaeni mjadala huo.
Nina wasiwasi na uwezo wa kuchambua mambo wa Juma Duni Hadji maana badala ya kuchambua mambo yeye hushambulia watu. Rejea dakika 45 alizozichezea kule ITV jumatatu!
 
Back
Top Bottom