Kuwe na kiwango kimoja cha utambulisho (titles) k wa wanasiasa wa kuchaguliwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwe na kiwango kimoja cha utambulisho (titles) k wa wanasiasa wa kuchaguliwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jun 28, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nina hoja ndogo sana ambayo nadhani si vibaya viongozi wetu wakaiangalia.

  Siku hizi wanasiasa wetu wanachaguliwa kutoka katika nyanja mbalimbali za maisha. Kuna waganga wa kienyeji, kuna waalimu wa shule za msingi, wakuu wa vyuo, wanajeshi watsaafu, polisi wastaafu, wapelelez wastaafu, mahakimu wastaafu, majaji wastaafu, wachungaji wastaafu, mapadri, maprofesa, manesi, madaktari, maimamu, madereva na nyanja mbalimbali.

  Hii imesababisha bungeni kuwe kama ni sehemu ya kuwatambua wabunge kwa walikotokea badala ya kuwatamabua kama wanasiasa wa kuchaguliwa. Utashangaa kusikia wabunge wakijulikana kama Kapteni Mkuchika (mstaafu), Kanali Kichuguu (mstaafu) Brigedia Ngwirizi (mstaafu), Professor Msola, Mwalimu Mkuu Lukuvi, Jaji Werema, Mganga wa Kinyeji Maji Marefu, Dakta wa Bandia Nchimbi, Dr. Kigwangalla (MD), Mchungaji Natse, Mr.2 Mbilinyi, Imam Kichuguu, Askofu Getrude Rwakatale n.k..

  Kwa vile wote pale bungeni wana kazi moja bila kujali walikotokea, ni vizuri tukawa na title moja kwa wabunge wote pamoja na mawaziri. Kwa utaratibu huo huo, tuwe pia na title rasmi kwa rais na makamu wake bila kuangalia walikotoka. Wabunge na mawaziri wote wajulikane kama Mbunge ABC au Waziri XYZ, na wala tusisikie tena titles na vyeo vya walikotokea. Hivyo tuwe na Mbunge Mkuchika, Mbunge Kichuguu, Mbunge Nwgirizi,Mbunge Msola, Mbunge Lukuvi, Mbunge Werema, Mbunge Maji Marefu, Mbunge Nchimbi, Mbunge Kigwangalla, Mbunge Natse, Mbunge Mbilinyi, Waziri Kichuguu, Mbunge Getrude Rwakatale n.k....

  Kwa upande rais nako tuondokane na ushamba wa kuwa matitles ya ajabu ajabu kama ilivyo sasa kutoka Rais Dr. Col Kikwete au Makamu wa Rais Dr. Bilal tuwatambue kwa urahisi tu kuwa ni Rais Kikwete, na Makamu wa Rais Bilal.

  Kuwa na title standard zitaondoa kasumba ya kuamini kuwa kapteni hawezi kumbishia General, na vile vile mwalimu wa msingi atafyata mkia kwa profesa au Mganga wa kinyeji ataogopwa kutokana na nguvu zake za gizani zaidi ya nguvu za hoja.

  Uwepo wa uniformity za titles katika viongozi wa kuchaguliwa itasaidia sana kupunguza ulazima wa watu kujitafutia titles za haramu.
   
 2. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Tena napenda kuongezea kwa mkuu hapa kwamba hata huo uheshimiwa ukome, waitwe ndugu fulani. kwakuwa huu uheshimiwa unawalemaza wanajiona miungu watu!
   
 3. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja zote mbili kwa 100%
  hasa hiyo ya nyongeza MUHESHIMIWA SPIKA, kwani hawezi kuwa spika tu, makinda ni mwananchi gani anayemuheshimu
  wanatumia kama vitisho najua hii kama ikipelekwa bungeni watapinga kama wanalivyofanya posho

  hata neno chama cha upinzania kwenye uchaguzi likome wakati wa uchaguzi hakuna chama cha upindani kila
  mtu anatafuta post kwa nini kuna chama cha upinzania tena

  hapo ni kuwapoteza wananchi neno upinzania lina maana mbaya katika fikra za wananchi
   
Loading...