Kuwawajibisha maafisa wa Serikali ni kitovu cha Demokrasia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kuwawajibisha maafisa wa serikali ni kitovu cha demokrasia. Uwajibikaji wa kidemokrasia unawapa wananchi na wawakilishi wao nafasi na njia ya kutoa maoni yao na kupatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa maafisa wa kuchaguliwa na wale wasio wa kuchaguliwa, na inapobidi wanashauri hatua za kuchukua kwa maafisa walioshindwa kutekeleza majukumu yao.

Dhana ya uwajibikaji wa kidemokrasia inajumuisha vyote viwili uwajibikaji wa kisiasa na ule wa kijamii—iwe moja kwa moja au kinyume chake, kwa wima, kwa ulalo au kimshazali au kwa namna yoyote ile iliyo katika msingi mkuu wa kidemokrasia wa nguvu ya wengi katika maamuzi yanayohusu umma.

Uwajibikaji wa kidemokrasia unajumuisha uwezo wa wananchi wa kuelezea matakwa yao ili kushawishi maamuzi, kwa mfano, kupitia michakato ya uchaguzi. Njia nyingine za kidemokrasia ni pamoja na maandamano, habari za kiuchunguzi, mikakati ya kibunge, midahalo ya umma au kura za maoni.

Uwajibikaji wa kidemokrasia pia unahusu mbinu ambazo sio za moja kwa moja, kama vile mfumo wa kuchunguzana na kurekebishana pamoja na taratibu nyingine zinazotumika kwenye taasisi moja moja ili kushawishi uendeshaji wa nchi.

Mifano ya mbinu hizo ni usikilizaji wa kesi katika kamati za kibunge, maswali yanayoulizwa na vyama vya siasa vya upinzani pamoja na mapitio au uchunguzi unaofanywa na ofisi ya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi au taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu za seikali, n.k.

Uwajibikaji siyo sifa inayoishia kwenye demokrasia tu bali uwajibikaji unapokuwa wa kidemokrasia, unasaidia sana kuboresha utendaji wa serikali. Hivyo, kwa kutumia istilahi uwajibikaji wa kidemokrasia, mwongozo huu unalenga kujenga dhana iliyojumuisha yote, pana na ya msingi kabisa badala ya dhana baguzi, finyu na yenye mipaka.
 
Najua mnapiga na nilishasema kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, tatizo ninyi mnakula sana…. MTAVIMBIWA.
 
Ofisi za umma sio mali ya mtu binafsi wala kijiwe cha kula bure bila kufanya kazi
 
Back
Top Bottom