Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Mhe Rais jana amesema mambo mawili kuhusiana na uhitaji wake wa msaada toka Rwanda.
Jambo la kwanza aliomba Kagame amsaidie watalaam watakao msaidia kununua ndege Q400 kwa ajili ya Air Tanzania.
Jambo la pili ameomba Kagame amsaidie watalaam watakao tengeneza system ya kutrack mapato ya TRA on realtime ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali
Maswali ya kujiuliza
1. Je ni kweli Tanzania hakuna watalaam wa kumsaidia kazi hiyo?
2. Je ni kweli Tanzania hakuna vijana watalaam wa IT wenye uwezo wa kufanyia kazi hizo requirements za Rais.
Kwangu mimi naona mheshimiwa amepitiliza ktk kulifanyia kazi swala hili. Na uhakika Tanzania ina watalaam wazuri sana ila serikali haijaamua kuwatumia.
Mfano kuna DG wa pale Costech kitengo kinachojihusisha na ICT kwa vijana anaitwa Mulamula. Huyu jamaa aliwahi kuchukuliwa na Kagame na ndiye inawezekana aliyeset na kushape mambo yote ya ICT Rwanda, lakini baada ya kurudi Tanzania hajapewa nafasi kama alivyo pewa na Kagame.
Ninacho jua kuwa watanzania wengi sana wanaotumiwa na serikali ya Rwanda kimya kimya na yamkini hao watakaokuja kumsaidia Magufuli wakawa ni wabongo.
Serikali ikubali kuwa tatizo la watalaam kutumia elimu zao linatokana na upendeleo ambao umekua ukifanyika kwa makusudi . Vijana wenye ujuzi wapo na wanao uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya taifa lao ili serikali kwa makusudi imewafungia nje.
Zamani usalama wa taifa walikua kazi yao ni kutafuta vijana talented na kuwashawishi kwa ajili ya kuchukua nafasi nyeti za serikali. Lakini leo ukiwa na kadi ya CCM hata kama hujasoma IT utashangaa unachukua kitengo cha IT.
Magufuli naomba ufikirie upya juu ya hili pia serikali iwe makini kuruhusu mgeni tena jirani aingilie mfumo wako wa IT ni hatari, vijana wapo jaribuni kuwatumia.