Kuwatumia "Mafundi" badala ya Wahandisi kwenye Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule ni dharau

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,427
85,872
Hongera kwa kukusanya TOZO ya dhuluma, mnataka kujenga vituo vya Afya ambavyo "vilianza kujengwa" tangu enzi za JK....sina tatizo!

Tatizo langu ni lile sharti kwamba "Ujenzi" ufanywe na wale mafundi wetu a.k.a Fundi Maikoz kwa kisingizio cha kupunguza gharama.

Majengo ya serikali sio nyumba binafsi, yana standard zake, yana aina yake ya ujenzi kwa ajili ya kuruhusu vitu mbali mbali ikiwemo wakati was majanga.

Ujenzi huu huwezi kumpa Fundi Maiko akujengee, ujenzi sio kuweka cement na tofali na kuchukua kamba au "pima-maji" kuona kama ukuta umenyooka. Hivyo kwa hili sikubaliani kwanza na Kitu hiki.

Pili, tuna Vyuo Vikuu mbali mbali lakini tunacho Chuo Kikuu cha ARDHI ambacho kimezakisha Mainjinia wazuri (labda leo tuwakane). Hawa Vijana wetu, Kaka na Dada zetu wana kampuni za Ujenzi, wana taaluma husika, wanalipa kodi, wameajiri. Leo hutaki kuwatumia then at the same time unataka Makampuni yao yalipe Kodi na Wao waendelee kulipa mikopo ya Bodi ya Elimu. Fursa umewapa Fundis kwa kigezo cha "kurudisha" fedha kwenye jamii.... Kwani hao mafundi wanaishi wapi na Contractors wanaishi jamii IPI?

Hivi Fundi anaweza kulipa bima ikitokea tatizo? Anaweza kufidia/kurudia ujenzi akitokea kajenga chini ya kiwango?

Je, in sahihi Fundi awajabishwe/akaguliwe na Mwenyekiti wa Kijiji/Daktari/Mwalimu etc ambao hawapo kwenye fani husika??

Kuna faida kubwa ya kuwatumia Wakandarasi ambao tena wako registered kabisa na Board yao, wanatambulika kisheria, wanalipa kodi, wana quarantee ila pia ni nafasi ya kuonyesha ubora wa elimu yetu kuwa sio ya makaratasi.....

Kinyume na hio tutakua tunadharau sana Elimu ya Vyuo vyetu kwa kigezo cha kukwepa gharama!

Unaweza kusoma barua hio hapo na sababu zilizotolewa.

I stand to be corrected

IMG-20210820-WA0096.jpg
 
Kipengele cha 3 cha barua nimekipenda, mashaka ni pale wakurugenzi na viongozi katika tarafa, kata, kijiji na kitongoji watajipa tender na kuwajili hao vibarua. Tunarudi haraka sana
Hahaahaha hatujawahi kusogea, tunazungukia hapo hapo. Magu ndio muasisi wa hizi mambo then anakwambia JENGO LA 500M TUMEJENGA KWA 50M TUMEIBIWA SANA
 
Naamini hawajapewa hio nafasi ila kama wepewa nafasi na wakashindwa basi mfumo wetu wa elimu ni wa hovyo ambao muasisi wake ni CCM. Kwahio tuchague moja kati ya hayo mawili
Nafasi ipi wahandisi ni nursery kids au kuna sababu ingine. Si wanaitwa mainjinia what are they engineering all these years since independence.
 
Mkuu asante kwa kulisemea hili. Tena hawa mafundi wanadhulumiwa sana na hao wasimamizi wa serikali
Eti ili alipwe inabidi muhtasari uandaliwe kwanza, dah hapo fundi anapewa asaini tu
 
Back
Top Bottom