Kuwashwa sehemu ya haja kubwa

Napenda kufaham je mtu kuwashwa sehemu ya haja kubwa ni ugonjwa Je inasababishwa na minyooo? Ili kuzuia huo muwasho mhusika anaweza kutumua dawa gani?

Huu muwasho ni kwa ndani au kwa nje na unawashwaje? By the way nimekupa tip za kufanya.....
Kama kwa ndani hao ni minyoo wanaitwa entorobius vermicularis dawa yake nenda phamacy uombe albendazone au mebendazone

Kumbuka
Nawa mikono mara na baada ya kutoka chooni. Nawa mikono kabla ya kula kitu chochote. Hakikisha chakula unachokula kina moto
 
Ahsante nimeuliza kwa kutaka kujua kama mgojwa atakuwa anawashwa kwa nje pia but nimekuelewa
 
Owky thanks na je kama ni muwasho wa nje

muwasho wa nje unaweza kutokea kama matokea ya uchafu au dalili ya ugonjwa hiyo sehemu, hivyo ukihisi hivyo we usitumie dawa yoyote zaidi ya kusafisha tu hiyo seheme kwa maji kisha pakaushe na taulo, usivae nguo nyingi ili kupunguza joto na unyevunyevu... usipaguseguse sana na mikono wala kujikunakuna, muwasho utaisha wenyewe.
 
Owky thanks na je kama ni muwasho wa nje

angalia aina ya toilet paper utumiayo, tumia zaidi maji na unawe mikono na sabuni kila baada ya kukata gogo

Usiache dawa ya minyoo, tumia at least twice a year

zaidi ya hapo labda ni aina ya meal au tu labda kiu mbadala:biggrin1:
 
Napenda kufaham je mtu kuwashwa sehemu ya haja kubwa ni ugonjwa Je inasababishwa na minyooo? Ili kuzuia huo muwasho mhusika anaweza kutumua dawa gani?
Inawezekana hao ni fungus, hivyo inabidi akamuone daktari ampe vidonge vya kuingiza sehemu ya siri au cream ya kupaka.
-Vile vile inawezekana anapenda kuvaa chupi wakati sehemu ya siri sio kukavu, anapomaliza kuoga ahakikishe ajifute vizuri ndipo avae chupi, unyevu nyevu sehemu za siri unaweza kusababisha kuwashwa.
-Ahakikishe anajisafisha vizuri sehemu za siri, wanawake wana utoko sehemu zao za siri, hivyo ahakikishe kila siku kujisafisha hadi ndani ili utoko wote utoke. Kama akiwa na utoko nao unaweza kusababisha kuwashwa.
- Azingatie usafi wa hayo niliyotaja hapo juu, kama muwasho unaendelea akamuone daktari na achukuliwe kipimo cha mkojo.
 
Napenda kufaham je mtu kuwashwa sehemu ya haja kubwa ni ugonjwa Je inasababishwa na minyooo? Ili kuzuia huo muwasho mhusika anaweza kutumua dawa gani?

Usafi wa kutosha unatakiwa - oga walau mara mbili kwa siku, tumia dodoki kusafisha rim ya bottom yako, kila baada ya haja kubwa tumia maji kujisafisha, fanya sitz bath/ sit bath mara kwa mara, kunywa dawa za minyoo walau mara mbili kwa mwaka, kata kucha zako, kula vyakula vyenye fibre kama brown bread, nuts, mboga za majani, kunywa maji kwa wingi, usibane choo kwa muda mrefu unapojisikia kwenda haja kubwa. Halafu punguza maharage. Pia muone daktari kama hali itazidi kuwa mbaya.
 
Zingatia Usafi, ukavu sehemu za siri, tumia Albendazole na/au Anusol. Ongea na daktari kwa ushauri zaidi.
 
Tumia tangawizi mbichi mara kwa mara hizo ni dalili ya kupata nyama za njia ya haja kuwa pia tumia fawa za minyoo nayo ni dalili mojawapo maumivu yakizidi muone daktari
 
Ahsanteni kwa ushauri naufanyia kazi kwani nimepata mwanga kuhusu hili tatizo.God bless you kwa wote mliokuwa positive katika ushaur wenu
 
Hiyo itakuwa minyoo nenda hospital upime kipimo cha haja kubwa ujue tatizo. Lakini mara nyingi kuwashwa kwenye mata.ko ni sababu ya minyoo wanaotaga mayai kwenye anus
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom