Kuwasaidia ndugu wa mkeo ni limbwata?

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Ndungu wana Jamvi nimeleta kwenu uzi huu ili tuweze kuuchambua, natumai humu wamo walioowa na wanaotarajia kuoa. Hapa utajifunza

Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.

Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!

NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatulia

Sijui ndugu huwa mnamatatizo gani hasa wadada
 
Hiki ulichokisema nimewahi kukishuhudia somewhere....A man alikua ni mtu wa ofisin na mke wake darasa la saba..lakini yule mwanamke alikua ana akili sana ya miradi ya biashara...jamaa yule alifanikiwa sana kimaisha...kufika utu uzima mke wake aliuacha ulimwengu....since there jamaa hajakua vzuri sana kimaisha isitoshe alishastaafu...so be careful na mke unayeishi nae..Mungu anaweza kumfanya amana na milango ya baraka ya maisha yako despite of elimu yake au status yake ya maisha ya nyuma.
 
Mkuu lazima wanaume tutumie akili sana yani
 
Promo ..... Kama ni kweli una tatizo mkuu.....Yaani mama yako aombe fedha kwa mkeo? Kisa, misimamo yako?

Anyway ni kawaida sana vijana walioanza mapenzi utu uzimani na wanaotoka kwenye makabila yenye wanawake wasio na mvuto kulowea kiasi hicho.
 
Ndungu wana Jamvi nimeleta kwenu uzi huu ili tuweze kuuchambua, natumai humu wamo walioowa na wanaotarajia kuoa. Hapa utajifunza

Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.

Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!

NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatulia

Sijui ndugu huwa mnamatatizo gani hasa wadada
Please give a kiss to ur wife for me
 
Hongera sana.
Mimi mwenyewe nipo kwenye hatua za mwisho mwisho kummilikisha kila kitu mke wangu.
Kwenye ndoa, ili kupata mafanikio na amani lazima mmoja awe bwege, mimi nikajichagulia (sitaki shida) ubwege,tumefika mbali tofauti na hapo zamani.
Tubaki na undugu wetu ila tusipokee kila ushauri kutoka kwa ndugu zetu kuhusiana na uendeshaji wa familia zetu.
 
Na siku ukimuacha mkeo unafilisika baraka zako ziko kwa mke wako mpende daima nyie wanaume mkifanikiwa tu huwa shida, halafu acha tabia ya kushirikisha ndugu zako mambo ya maendeleo yako, kulikuwa kuna haja ya wao kujua kuwa mkeo anajenga kwao kweli, jifunzeni kuwa na siri pia wewe ni mwanaume unayejielewa endelea kuwa na mkeo ingekuwa wanaume vichwa panzi wangeshavunja ndoa kisa eti mchagga
 
Ni wanaume wachache sana wenye msimamo kama wako.

Sumu ya ndoa ni ndugu, tena wa pande zote mbili. Mmoja akiwasikiliza ndugu ndoa haina tena uhai.

Hongera sana kwa kuonyesha msimamo thabiti
Nilitukuza ndugu wa mke wangu walipotamka kuwa nyumba hii amejenga ndugu yao mbele ya mama yangu. Ndugu hatari sana kwa ndoa
 
Sasa ulitaka aombe nani na wewe jamaa ndo mwanaume sasa sio kusikiliza ndugu kuua ndoa yake
Promo ..... Kama ni kweli una tatizo mkuu.....Yaani mama yako aombe fedha kwa mkeo? Kisa, misimamo yako?

Anyway ni kawaida sana vijana walioanza mapenzi utu uzimani na wanaotoka kwenye makabila yenye wanawake wasio na mvuto kulowea kiasi hicho.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom