Kuwapo kwa uongozi wa jiji la Dar-es-salaam ni namna nyingine ya ufujaji wa fedha za umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwapo kwa uongozi wa jiji la Dar-es-salaam ni namna nyingine ya ufujaji wa fedha za umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jul 13, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napata shida sana kusikia na kuona kuwa serikali yangu inaridhia muunda wa kiutawala Jijini Dar ambao unatuonyesha kukosa umakini katika kupunguza matumizi ya fedha za umma yasiyo ya Lazima. Tumetengeneza mianya mingi mno ya kutolea fedha ndio maana mwisho wa siku kidogo tulicho nacho hakitoshi. Jiji la Dar lina Manispaa tatu ambazo kimuundo wa utawala zinajitosheleza sasa kuna haja gani kuwa na uongozi wa wa jiji na mayor? na mkurugenzi? pengine na wasaidizi wengine wengi? Wakati huo huo kuwe na uongozi wa mkoa Katibu Tawala na Mkuu wa mkoa. Ni nini ambacho kinafanya shughuli za jiji zisitawanywe kwenye manispaa zake? kwa nini soko la karikoo na stand ya ubongo zisiwe mamlaka huru zenye kuendesha mambo yake na kwamba kwa kufanya hivyo uongozi wa taasisi hizi utakuwa karibu na wateja wao na kutatua kwa karibu kero za kila siku kuliko ilivyo sasa ambapo baadhi ya maamuzi lazima yatolewa na uongozi wa JIJI? hivi ni thamani ipi uongozi wa jiji unaongeza katika soko la kariakoo? au ubongo? sana sana ni masilahi binafsi ya kwao na rafiki zao.
   
Loading...