Kuwapigia magoti viongozi wa CCM, je ni sawa?

Sep 13, 2011
11
5
http://4.bp.blogspot.com/-jMW2c5L7I...NI+WA+VITI+MAALUMU+KATA+YA+NGOHELANGA+CCM.JPG

DIWANI+WA+VITI+MAALUMU+KATA+YA+NGOHELANGA+CCM.JPG

Huyu mama ni diwani wa CCM akiwapigia magoti mawaziri kuombea wananchi wake waruhusiwe kuendelea kulima katika bonde la Kilombero. Je imefikia hatua ya viongozi wetu kuabudiwa kama miungu? Na je dunia ilipoumbwa si kila mtu mahali alipolizaliwa ndio eneo lake la kujipatia riziki na kuishi? Cha ajabu tanzania watu wanafukuzwa maeneo yao ya asili na kupewa wageni. Kilichobaki ni kupigia watu magoti hata kile ulichopiwa na Mungu.

Mwisho wa ubaya aibu,nahisi waTZ tumerogwa huyu diwani ana matatizo haki hataufutwi hivyo vipo vyombo vingi vya kudaia haki.Kingozi kama huyu hatufai, na si mfano wa kuigwa.
 
Mkuu wananchi wengi hawajui haki na stahili zao kutoka serekalini. Ndio maana serekali ikijenga barara inajisifu kuwa serekali ya ccm imefanya vizuri,ni wajibu wa serekali kuhudumia raia wake kwa huduma za kijamii kama, shule,zahanati na ujenzi wa barabara. Kwani hata mkoloni alijenga vitu hivyo. Tatizo hapa sisi tujaribu kuelimisha umma nini wajibu na haki zao kwa serekali isiwe kama inatufadhili!
 
Mimi naona ni "usanii" mtupu hawa sisiemu wanatufanyia!
 
Inasikitisha sana kuona kuwa wananchi hawana haki na mali zao. Haiwezekani kuwa wawapigie magoti viongozi ili waweze kujipatia riziki zao. Wananchi tuanaonekana kabisa hatuna haki zetu au hatuzijui kabisa; kwani viongozi tuliowachagua wanatakiwa kuwatimizia wananchi mahitaji yao. Na wala si kuwapigia magoti, binadamu mwenzio eti kuwaomba wao ni nani???
 
Poor me. Nimeliangalia suala hili kwa mtizamo mwingine kabisa. Sio kwamba amepiga magoti kama heshma tu ambayo wanawake wengi wanafunzwa tangu wakiwa wadogo?? Angepiga mwanaume ningeshangaa. Na je inawezekana kuwa asingepiga hayo magoti kama madiwani hao wasingekuwa wa CCM?

Ah haya makitu ni magumu kuyaelewa.
 
Huenda huyo dada ni msukuma hivyo anadumisha mila!
 
Back
Top Bottom