Kuwalinganisha Marais kufanywe na watu walio nje ya mfumo tu

Bushesha jr

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
677
690
Hii tabia ya kuanza kufanya uchambuzi wa kuwalinganisha viongozi wetu wakuu naona ingali bado inaendelea, binafsi nilimsikia Mhe. Rais mara kadhaa akikemea jambo hili lakini bado kuna watu tena wateule wa rais wanaendelea na hii tabia

Uwaziri ni cheo cha heshima sana sasa inakuwaje mtu anaacha kazi za uwaziri na kuanza kuzungumzia vitu visivyohusika?

Tumesikitishwa sana na kitendo cha Waziri Fedha tena kwenye hotuba nyeti ya bajeti anaacha kufafanua Mambo muhimu ya kibajeti ili wananchi waelewe anaanza kudemka

Kwa mtu unayefikiri kwa kina huwezi kuanza kuwachambua Marais viongozi wako waliokuamini kwa muda mrefu na huku wew ukiwa mteule wao hayo siyo maadili kabisa. Waziri Mwigulu kama anataka kuwachambua Marais wetu aachie ngazi Kwanza

Ni afadhali angeishie kwenye vibwagizo vya yanga tu japo hata hivyo navyo havifai kwa sababu tukio hilo lilikuwa nyeti mno likifuatiliwa na mamilioni ya watu walioko ndani na nje ya nchi sasa kwanini mtu unashindwa kuwa serious na kazi

Inasikitisha sana labda atajirejebisha lakini ametukosea sana

Mungu ibariki Tanzania
 
Tatizo ni kwamba hawapo pale kutumikia wananchi, bali wapo pale kulinda ajira. Mwanasiasa anapolinda ajira yupo tayari kufanya lolote kwa usalama wa ajira yake. Kwa ujumla kuwa mwanasiasa ni kuwa mna*ki.
 
Waliowaita Mabeberu walikuwa wanasikiliza malumbano ya hoja badala ya bajeti
 
Back
Top Bottom