Kuwakamata wamiliki wa Tashrif kuwe somo kwa wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwakamata wamiliki wa Tashrif kuwe somo kwa wengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,884
  Likes Received: 83,366
  Trophy Points: 280
  Kuwakamatwa wamiliki wa Tashrif kuwe somo kwa wengine
  Gloria Tesha
  Daily News; Wednesday,January 14, 2009 @20:00​

  Ajali za barabarani hapa nchini si jambo jipya au geni masikioni mwako msomaji, bila shaka umesikia matukio hayo katika maeneo unakoishi au hata katika mikoa mbalimbali.

  Matukio ya ajali yamekuwa yakisababisha vifo vya watu wengi hasa nikikumbuka ile iliyotokea majuzi tu, katika Kijiji cha Hale, wilayani Korogwe, Tanga na kuhusisha basi la kampuni ya Tashrif linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tanga. Katika ajali hiyo watu 28 walikufa na wengine 22 walijeruhiwa.

  Ajali hiyo ni miongoni mwa ajali nyingi mbaya kuwahi kutokea nchini ikijumlishwa pia ile iliyotokea takriban wiki mbili zilizopita katika eneo la Uchira, Kilimanjaro na kusababisha vifo vya watu 11, ndugu wa familia moja. Ajali nyingine mbaya kutokea mkoani Tanga ni iliyohusisha basi la No Challenge iliyotokea mwaka 1998 na kusababisha vifo vya abiria karibu 70.

  Si lengo langu kueleza historia ya ajali zilizowahi kutokea kipindi cha nyuma au hata hivi karibuni, bali ni kukupa taswira ya namna ndugu, jamaa na marafiki zetu walivyopoteza maisha, viungo na kupata ulemavu wa maisha kutokana na ajali hizo ambazo nyingi zinaweza kuepukika.

  Kikubwa zaidi ni hatua iliyochukuliwa na polisi wa mkoa huo ya kuwakamata wamiliki wa kampuni inayoendesha mabasi hayo. Sifurahii kukamatwa kwao, kwa kuwa anayejua kuwa wana kosa au hawana ni vyombo vya dola (mahakama) lakini kwa mujibu wa Kamanda wa Tanga, Simon Sirro katika mahojiano na gazeti hili katika habari iliyoandikwa jana, inasemekana kuwa wamiliki hao wanadaiwa kuruhusu gari kufanya safari ya kubeba abiria huku wakijua kuwa ni bovu.

  Madai mengine ni kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wao aliyetoroka mara baada ya ajali kutokea Januari 10 mwaka huu, hivyo polisi kushindwa kujua kama alikuwa ni dereva kweli ama la.


  Madai hayo kama ni kweli yanadhihirisha wazi kuwa kuna udhaifu mkubwa kwa wamiliki wa mabasi kutokuwa na muda wa kufuatilia hali ya magari yao badala yake wamekuwa wakifurahia kukusanya fedha zitokanazo na mapato bila kuhoji uzima wa magari yao.

  Inakuwaje mmiliki wa kampuni ya magari ya kubeba abiria (mabasi) kama huyu wa Tashrif anakosa kuwa na kumbukumbu za dereva wake?
  Sitaki kuamini suala hilo pengine mpaka baada ya uchunguzi wa polisi ukamilike, lakini pia ni madai ambayo yamebainika baada ya kuhojiwa na polisi.

  Eti mmiliki wa gari hana hata nakala ya leseni ya dereva wake! Hata hana maelezo binafsi yanayomhusu dereva huyo. Hii inadhihirisha wazi kuwa baadhi ya wamikili huajiri madereva wa uchochoroni, wasiokuwa na sifa wala vigezo bila shaka kwa kuwa labda ni mjomba au shangazi.

  Hali hii isipodhibitiwa, itatumaliza. Pamoja na Mkuu wa Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema jana kupitia gazeti hili kukiri kuwa bado kuna udhaifu wa kuhimili ajali za barabarani kwa polisi nchini kutokana na kukosa umahiri katika kazi, pia tukubali kuwa wamiliki, madereva na hata abiria wamekuwa wakichangia kutokea kwa ajali kama tunavyoshuhudia kwa ajali hii ya Tanga.

  Mara nyingi tumesikia na kushuhudia abiria wakimlazimisha dereva kufanya jambo la hatari, mfano; kumlazimisha dereva aongeze mwendo au kumpita mwenzake, ushabiki huu umesababisha maisha ya wengi kupotea.

  Ndiyo maana nasema wamiliki kama hawa wanapaswa kuwa mfano kwa wengine, si kwamba nawahukumu kwa tukio hilo la ajali lakini iwe njia mojawapo kuwapa angalizo wamiliki wenye tabia ya kupuuza ubovu wa magari yao au kuhifadhi kumbukumbu ya madereva.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Huu ni uonevu kwa wamiliki wa mabasi, tatizo liko kwa dereva, kama basi lilikuwa bovu kwanini aliliendesha?
   
 3. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa isitoshe ni jukumu la trafic kufanya ukaguzi ya mabasi ya abiria mara kwa mara.upana mdogo wa barara zetu wakati kuna ongezeko la magari.kutowajibika kwa trafic kuhusu mwendo wa kasi yote hayo huchangia ajali.hapo seriakali inajivua lawama kwa kumkamata mmiliki
   
 4. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Ubovu na wembamba wa barabara,huchangia sana ajali ili hali kuna ongezeko la magari
   
 5. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele ndugu zangu. Kabla ya yote nadhani tuchunguze sababu zote zinazoleta karaha katika usafiri wetu. Tukianza na mabarabara, driver education, ufuatiliaji wa polisi wa traffic na kuhakikisha kuwa watumia barabara wanawajibika. ( kama una traffic offense ufuatiliwe ipasavyo ili ufikirie mara mbili kabla hujarudia hilo kosa), uthibiti wa mabasi na magari yote kwa jumla. Including regular inspection kuhakikisha kuwa mabasi na magari ni road worth all the time.

  This can be done if we are serious about our safety.

  Peace
   
 6. e

  eddy JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,406
  Likes Received: 3,783
  Trophy Points: 280
  Kwanini tusiige Holland ambapo ukaguzi wa magari hufanywa na makampuni maalum. hawa trafik wanaangalia rangi ya gari tu.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Barabara sio nyembamba kiasi hicho. Barabara hiyo ipo katika viwango vinavyotakiwa kabisa. Kwa uendeshaji wa staili ya Tashrif na ubovu wa basi lenyewe hata barabara ingekuwa pana kiasi gani ajali ile ingetokea tu
   
 8. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Huo utakuwa uonevu kwa dreva.Anayekagua gari/basi na kutoa kibali cha kufanya biashara si dreva.What if dreva hajui mambo ya ufundi???Hivi kazi ya dreva ni ipi hasa kwa hili???ingekuwa chanzo ni speed kali basi hapo dreva angehusika.
   
 9. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nadhani hapa kuna nidhamu ya woga, kamanda anashindwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yake na badala ya anatafutwa mchawi.
   
 10. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Mbona ubovu wenyewe haujatajwi kwenye hii story? nauliza hivi kwa kuwa hata kuchanika kwa seat ni ubovu! Ni huo ubovu unaosemwa ndio umesababisha hii ajali?
  Ajali nyingi za barabarabi Bongo husababishwa na madereva- mwendo wa kasi,uzoefu mdogo,kutojua sheria, uchovu, utumiaji vilevi, etc.
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hii ni siasa tu, wanataka waonekane wanafanya kitu, wakatika wa kukagua magari walikuwepo wapi matrafic? Au hakuna sheria kama hiyo? Na kwani owner wa kampuni lazima ahusike kwenye daily operations za hiyo kampuni?
  Ukweli ni kwamba barabara zetu ndogo (narrow) sana.
   
 12. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #12
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza nianze kwa kuwapa pole ndugu na jamaa wa marehemu woote na Taifa kwa ujumla. Pili naomba kuchangia kidogo kuhusu hii maada.

  Mi mimi ninaona tatizo halipo kwa mmiliki/wamiliki wa vyombo vya usafiri wala /dereva/madereva peke yao baali ni governement kwa kushindwa kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti/kuratibu huduma ya usafiri(abiria) nchini. Serikali sasa inakimbia jukumu lake na kuanza kutuhumu wamiliki wa uzembe ambao wao ki msingi wanatumia huo mwanya/uhuru kufanya kama wafanyavyo, kuua na kuua miaka nenda rudi na kuchange tu majina ya makampuni yao huku serikali ikijigamba kuwa imewafungia leseni za kutoa huduma.

  Utengenezaji wa mabasi, asilimia kubwa ya mabasi Tanzania hayana sifa ya kubeba abiria. Kutumia Engines za magari ya mizigo na kuyafanya ya abiria mi sina tatizo nalo, tatizo lina kuja kwenye utengenezaji/usukaji wa mabodi. Mabodi mengi sana yanatengenezwa bila kuzingatia utaalamu na viwango vinavyo takiwa. Utakuta basi lina uzito mkubwa (hapo halija pakia hata abiria) na ndo maana yaliyo mengi kila yakifika kwenye mezani utaona abiria wanashushwa hata kama halijapakia mizigo mingi. Uzito huu unasabanishwa na kutokutumia materials zinazotakiwa. Chukua mfano wa viti vya mabasi yetu haya, sehemu kubwa ni vyuma halafu viko karibu karibu sana, na kwajinsi vilivyo tengenezwa huwezi kuweka mkanda maana haiwezekani....kwa nini? Jibi ni rahisi tu mfumo ule hauruhusu mambo hayo. Sasa basi likipata msukosuko wa hatari lazima watu wengi watapata majeraha makubwa sana pengine inaweza hata vifo vikawa vingi si kwa sababu ya mwendo kasi wa basi baali ni vyuma/mabati waliyokuwa wamekalia yamewachinja. Kuna basi lilikuwa linajilikana kwa a.k.a "mende" nadhani ni kati ya 2005/2006 lilikuwa linafanya safari zake kati ya Arusha na Dar, huwezi amini mkifika salama bila tairi moja (kushoto nyuma) kupasuka basi siku hiyo mnabahati kubwa sana. Utaona hapo hakuna uwiano kati ya uzito wa basi lenyewe na uwezo wa matairi.

  Sasa basi, mwenye uwezo wa kuleta changes kwenye huu mfumo mmbovu ni government peke yake kwa kuweka sheria/utaratibu/viwango vya vyombo vya usafiri. Pia iwapeleke wale vehicle inspectors wasomee hayo mambo ya mechanics wala sio hizo course za miezi mitatu mitatu na kuishia kujua tu matatizo madogo madogo ya magari.

  Natoa wito kwa wamiliki wa mabasi wajitahidi kuboresha huduma zao wasisubiri wachina washike biashara ya usafirishaji halafu waanze tena kulalamikia governement haiwapendelei kama wazawa.

  Mwisho, matatizo yapo mengi sana kwenye mfumo mzima huu wa usafirishaji, cha msingi kila mtu akitimiza wajibu wake kwa haki tutapiga hatua na kupunguza hivi vifo visivyo vya lazima.

  Asante.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Baada ya kusogezwa mara mbili tokea kwenye siti yangu ambayo ilikuwa karibu na ya mwisho, ilibidi nimuulize konda kuhusu usumbufu huu ambapo basi lenyewe lilikuwa tupu. Nae akatupa lawama kwenye bodi la basi kuwa ni zito sana. Bodi la basi hilo limetengenezwa Kenya
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mzee. Hauko serious!
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Vyanzo vya ajali vinajulikana. Hii hatua ni kama Zimamoto, sababu ajali zimetokea siku za karibuni na kupotoza ndugu zetu kibao. Lazima uwatafute mabangusilo ili uhamisha lawama.
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Kwenye Majira leo kuna headline kuwa majamaa wameepuka kwenda jela, sijasoma zaidi ya hapo lakini.
   
 17. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Owner anahitajika kujua sifa za madereva wake, pamoja na kuwakatia bima etc. Vile vile anahitajika kujua jinsi ya kuwapata endapo watapotea kama inavyosadikika katika habari hii. Kwa ujumla anahitajika kujua operations za shughuli nzima pamoja na ubora wa magari etc. Ndiyo maana utakuta katika mashirika ya mabasi kama vile zamani Kamata na railways wakati mwingine basi linasimamishwa na wakaguzi wa kampuni kufuatilia mwenendo wa dereva na konda wakiwa njiani. Wakati mwingine shirika linakuwa na watu wasiofahamiana na dereva na konda wanaosafiri njia nzima ili tu waje waripoti utendaji wa hao operators ( konda na dereva) Kwa kujibu hoja yako, ndiyo; owner anapaswa kujua daily operations za mabasi yake yote. Kama anayo mengi basi huajiri watu kufanya kazi kwenye department ya traffic operations.
   
 18. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tabia ya madereva ku-overtake hata sehemu zisizo muafaka mfano milimani, kwenye kona n.k. husababisha ajali kwa asilimia kubwa sana. Pamoja na hilo pia speed za mabasi ni kubwa mno, hawa jamaa huwa wanaenda mpaka 160-180kph na barabara zetu hazijakaa sawa kwenda kwa speed kama hizi.
   
Loading...