Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Serikali ya Kuwait imeahidi kutumia Sh84 bilioni kwa ajili ya kuifanyia ukarabati Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo katika ofisi za wizara hiyo mjini Unguja jana, Balozi wa Kuwait nchini, Jasim Al-Najim alisema Serikali yake imechukua hatua hiyo ili kudumisha umoja uliopo kati ya pande mbili hizo.
Balozi huyo alisema timu ya wataalamu kutoka Kuwait inatarajia kuwasili Zanzibar Agosti kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu juu ya utekelezaji wa msaada huo.
Alisema matengenezo yataanza baada ya wataalamu hao kumaliza kazi hiyo na kutoa maelekezo yakinifu juu ya utafiti wao katika majengo hayo.
Balozi Al-Najim alisema watakapokamilisha ujenzi huo mashirika mbalimbali yatajitokeza kwa ajili ya kusaidia miradi mingine.
"Mradi huu mkubwa utafungua milango kwa Serikali ya Kuwait kupitia mashirika ya misaada ya nchi hiyo kusaidia miradi mingine ya maendeleo ya uchumi na kijamii,"alisema.
Waziri Kombo aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kukubali kutekeleza mradi huo mkubwa utakaowasaidia wananchi wa Zanzibar.
Source: Mwananchi