Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Wana JF,
Mara nyingi nashindwa kabisa kuwaelewa hawa wanasiasa wetu, na hasa hawa wanaohusika na uongozi wa Bunge. Hivi, huwa wanajipa muda wa kutafakari na kutambua kwamba wanapotoa adhabu za kuwafungia Wabunge kuhudhuria vikao vya Bunge, zaidi ya kumi au vikao vyote, kimsingi wanaadhibu wananchi wanaowakilishwa na hao Wabunge na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa katika Bunge?
Hivi kweli hii kamati hii ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayopaswa kuwa ya maadili na haki, inaona ni maadili yanayokubalika kuwaadhibu wananchi kwa kosa alilofanya mbunge mwakilishi wao, huenda kosa ambalo wala wao haliwahusu? Na katika kipindi chote ambacho kamati hii inamfungia mbunge kuhudhuria vikao, nani anakuwa muwakilishi wa hao wananchi katika Bunge kulingana na haki yao ya kikatiba?
Kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge inaweza kudhani inawakomoa wabunge kwa kuwafungia kuhudhuria vikao, lakini kimsingi anayeadhibiwa na kukomolewa hapa ni mwananchi, ambaye ana haki ya kuwakilishwa katika vikao vyote vya Bunge. Kamati hii haina mamlaka yeyote ya kikatiba kuzuia sehemu fulani ya nchi hii Tanzania kutowakilishwa Bungeni kwa kipindi fulani. Hii si haki wala maadili kwa mwananchi.
Kama kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge ina uwezo wa kutafakari mambo basi itafute adhabu mbadala kwa wabunge, adhabu ambazo haziwanyimi wananchi haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa katika vikao vyote vya Bunge. Sio kuadhibu waliokuwamo na wasiokuwamo kwa sababu tu mnataka kuwalenga watu fulani.
Nadhani suala hili la adhabu za kuwafungia wabunge kuhudhuria vikao vingi linapaswa kupelekwa Mahakama ya Katiba ili kieleweke.