Kuwafukuza njiwa

julisa

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
209
49
Habari wana jf

Hapa nyumbani nina banda la uwani ambalo natumia kama stoo sasa njiwa wanaweka makazi yao sehemu ya juu ndani ya fisher board..naombeni njia ya kuwafukuza kwani sijui wametokea wapi na wanachafua mazingira na uchafu wao..
 
Njiwa ni kitoweo tafuta mtu awatege, aisee ningekuwa hapo!!!!
 
hao ni ndege wazuri saana, mimi binafsi nawapenda saana ndege hao, na nina mpango kabambe wa kuwafuga,tatizo nahofia hawa kunguru weusi, maana ni waharibifu saana na serikali inaleta usanii ktk kupambana nao eti wanaita mpango wa kuwaangamiza, mara utasikia zoezi letu limefanikiwa tumewaangamiza ,mmhh wakati bado wapo kibao na wanazaana ile mbaya. kuhusu hao njiwa nakushauri tengeneza banda mahususi kwa ajili yao , kisha liweke vzr njee, na wakishaa zoea kuingia kwenye banda basi ziba dari lako kusiwe na sehemu ya wao kuweza kuingia kisha wahudumie kwa kuwapa maji na chakula, kila unapowapa chakula piga mluzi wakizoea utafurahi kuwa nao.
 
mh... huwa nasikia njiwa wa dar es salaam wengine wana kazi maalum ila sijui ni kazi gani hiyo!!!!
 
Jaman nataman kama wahamie kwangu maana ninavyowapenda ni balaa ni ndege wapenda amani hao kama nyumba ina magomvi zinakimbia
 
Back
Top Bottom