Kuwafanyia watoto DNA test | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwafanyia watoto DNA test

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TIMING, Dec 14, 2009.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu, juzi katika vikao vyetu vya pombe tulikumbana na hoja moja iliyokuwa moto sana hasa kwa akina mamsapu!!!

  Hoja yenyewe inahusu kupima DNA watoto wetu wanapozaliwa; mimi nilitetea kwa hoja kwamba inasaidia watu kuwa makini wanapomega au kumegwa nje, na pia inaleta faida kwa mtoto kwa kumjua baba halisi

  Pia nilitetea hoja kwamba hakuja ubaya kutumia utaalam wa kisayansi uliopo kwenye maisha ya kila siku

  Cha kushngaza, wanawake woote waliokuwa pale (including tibaigana wangu) walipinga DNA tena kwa hasira kabisa na hasa wakisisitizia kwamba kupima DNA ni kumfanya mkeo kuwa si muaminifu

  sasa wadau, naombeni mawazo yenu kwani bado naamimi DNA ni ,uhimu!! akina dada mnasemaje?
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Juzi juzi hapa walipima akina baba DNA na watoto wao ilionekana idadi kubwa ya wababa wamebambikiziwa watoto yaani sio wa kwao aidha mama alidungwa na lijamaa jingine au hausi boy alijipendelea yaani taabu tupu unaweza kufa kwa kiholo.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nikileta hoja hizo wanasema nawaona malaya... sasa nataka kutafuta njia nyingine ilimradi kupigania DNA test iwe kama tunavyopima watoto bloo grouping

  akina mama ni wakali mno ukileta DNA testing discussions
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii kitu inafanywaga kwa siri bila mama kujua, na ukikuta wote sio wako taratibu unaondoka unamwachia mama nyumba.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Shukrani mkuu, sasa kwa hapa bongo unafanyaje kimyakimya?

  je huoni kwamba kwa kufanya kimyakimya manake wanawake wako right kwamba ni kitu kibaya?
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ukiona mtu anakuwa mkali hapo basi kuna tatizo. Kama najiamini kuwa mimi ni mwaminifu kwa mume wangu wala suala la DNA halinipi tabu.

  lakini pia MTM mpaka muamue kupima DNA kuna kuwa na kitu kimesukuma kufikia hapo....
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Wakatoliki wana kitu wanaita "Kanuni ya imani", kwa ufupi kwamba unatikuwa kuamini kuwa kuna kuna Mungu baba, mwana na roho mtakatifu. Kama huamini hivyo basi kibilia kwingine. Kama na wewe unataka amani kwenye hiyo ndoa yako achana DNA tests unazoziwaza. Unachokaribisha ni kuzimia ghafla (na usirudi tena) kwa pressure. Wazee waliosema kuwa kitanda hakizai haramu hawakuwa wajinga. Jitahidi kumwamini mwenzio vinginevyo umuache. Kwani ikitokea errors kwenye test mtoto tena unayefanana naye akawa siyo wako utakimbilia wapi?
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unajua akina mama walio wengi hasa wale wanaopenda mafiga ma3 iwa wanakuwa wasahaulifu sana na hawana uhakika pindi wakidungwa mimba ni baba yupi ndo ishu hapo.
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii ni ulimwengu ya funika kombe mwanaharamu apite, ukilifunua imejitafutia balaa. bora tuuchune ziendelee. tukichimbua dna nazani enitaimu unaweza ukagundua umekaowa kastepu sista ka nyumba ndogo ya huyo anaejifikiria ndio baiolojikali faza wako (rola kosta hapo ukigundua na yeye pia sie babaako). hapa ndio utajua tafauti ya shule na sekondari.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  msukumo wangu ni kupima kila mtoto kwa sababu ya kujiridhisha ila naona wamama wamekuwa wakali sana
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,879
  Likes Received: 23,504
  Trophy Points: 280
  Duh! Kuna kabinti nilikapata enzi za sekondari skuli sikaelewielewi! Ngoja nifanye mpango wa kucheki vina7.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  lakini mkuu huoni kwamba tuko kwenye era ya sayansi na teknolojia, kwanini iwe DNA adui badala ya confirmation ya bond kati ya baba na watoto?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukiwa unaenda kufanya hakikisha unafanya kwa siri kali alafu hakikisha upo bwiiiiii na serengeti.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Mkuu, nakimbia home ila kama nikipata nafasi kesho naweza kuongea kidogo. Kuna watu wanafanya genetic studies na kuna matatizo makubwa sana ya kimaadili (ethical issues). Kama unataka kuangalia kwa kiasi gani watoto wengi wanaishi na non-biological fathers, basi inabidi ufanye utafiti na kuna tararibu zake. Ila kama unataka kuhakikisha kama watoto wako hakuna uliyebambikizwa, nadhani unatangaza vita na mkeo. Hata ukikuta watoto wote ni wako, hilo doa hutaweza kulitoa. Hata mimi nisingependa wife anisingizie kuwa natembea na wasichana au wanawake kibao wakati najibana sana na kula kwa macho. Kuna matatizo makubwa sana, ya kisaikolojia katika hili suala. Siyo rahisi ki hivyo!
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,879
  Likes Received: 23,504
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Adhawais yanaweza tokea mashambulio katika moyo nikaresti in piis?
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo kuna kutoaminiana hapo?? well kama huamini kuwa mtoto ni damu yako na mimi najiamini wewe ndo the only man niliyehusiana naye wakati wa zile siku.... ntaenda tena kifua mbele!!!!

  wanaokataa/kuwa wakali wanakuwa hawana uhakika pia mtoto ni wa nani!!!
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  MTM kuna rafiki yangu wa karibu sana hata kama anasoma hapa atagonga thanks. Alimgusia mkewe wakafanye DNA kwa vile mtoto katoka very black na the head is too big, na masikio makubwa wakati jamaa ni mweupee na mke wake mweupe, alimnunia kama siku 2 analia tu na hata hakula mchungaji ndio aliyemaliza ugomvi kwa kumwaambia "AMINI TU NI WAKO"

  Usifanye DNA kama yafuatayo yamewahi kutokea kwako.

  1. Kusafiri hata kwa wiki 1
  2. Kama una house boy
  3. Kama mkeo yuko serikalini/bandarini na amewahi kusafiri/kufanya kazi za shifti.
  4. kama ni mwanakwaya(hapa ndio kuna utata na kuna hitaji thread)
  5.................
  6..................
   
 18. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Kimya kimya yawezekana... wala hata watoto wenyewe hawatajua.... unywele unatosha...ama kama ni wadogo swab ya mdomoni inatosha!!!

  kuna rafiki yangu mmoja his son had made a 17 yr old pregnant , si unajua mambo ya marekani tena hiyo ni case ya sex with a minor...baba mtu akawa hapati usingizi...luckily wazazi wa msichaan wakawa hawana hizo,.... mtoto akazaliwa....kijana akajizatiti kufanya vibarua hapa na pale kumlea mwanae....after abt 6 months wakaamua kumfanyia DNA...mamake akaja kumwacha pale kwao wakachukua mouth swab an kuituma LAb...duh Results zikirudi yaani 0.00009% chance that he is the father.... we kazi hapo sasa....
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,879
  Likes Received: 23,504
  Trophy Points: 280
  Mpwa nimegonga senksi kwa utirio kwenye red uliomwaga na sio kwasababu umesema yaliyomkumba ndio agonge senksi! Hiyo namba nne inahitaji seksi zaidi. Naiogongea kwa hapa. SENKSI!
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Nguli namba 4 sijaipata vizuri....kama hutojali nifafanulie kiduchu
   
Loading...