Kuwaengua Wastaafu kutoka kwenye vikao vya maamuzi vya CCM, ni ushindi wa mafisadi?

STRATON MZEE

Member
Jan 4, 2012
59
17
Wajameni kuna hili jambo ambalo limetokea kwa hawa jamaa wanaojiita CCM kuwaengua wazee waastaafu kutoka katika NEC yao, na kuwaundia baraza lisilo na meno, yaani baraza la washauri. Mi nionavyo, hii ni ushindi kwa mafisadi wanaoutaka urais 2015, hasa ukizingatia kuwa wazee hawa wakianzia na Nyerere mwenyewe, ndo waliokuwa wanaongoza harakati za kuamua nani awe rais na nani asiwe rais. Kama tutakumbuka, Mwl. aliwahi kumwambia mmoja wa makada wa CCM ambaye anatajwa kwenye harakati za kuwania urais 2015 kuwa hafai kuwa kiongozi hapa duniani. Hivyo, ili harakati zao za kuingia ikulu zitimie, ilikuwa ni lazima hawa wazee waliokuwa wanaweka kauzibe waondolewe kwenye vikao vya maamuzi. na kwa hilo wamefanikiwa. Wajameni! Kuna ahueni yoyote ambayo CCM wameipata kutokana na kuwaondoa wazee hawa?
 
Mene mene tekeli na Peres.........CCM inaelekea njia ya KANU , na ndo ukombozi wenyewe huo...JK ni agent tu wa kulisambaratisha genge la wezi la CCM akiwemo kila mtu (inclusive)....hawezi jua anachofanya mpaka hapo Mungu atakapofanikisha safari ya kuikomboa Tanzania kutoka kwa Chama Cha Majangili!
 
Mene mene tekeli na Peres.........CCM inaelekea njia ya KANU , na ndo ukombozi wenyewe huo...JK ni agent tu wa kulisambaratisha genge la wezi la CCM akiwemo kila mtu (inclusive)....hawezi jua anachofanya mpaka hapo Mungu atakapofanikisha safari ya kuikomboa Tanzania kutoka kwa Chama Cha Majangili!
Hana uwezo wowote hata yeye ni mmoja wa walewale majangili tena ni mtu Hatari sana.
 
Kuenguliwa kwa wazee hao ndio mwisho wa ufisadi kwa kuwa baadhi ya wazee hao nndio walikuwa mabingwa wa vimemo vya mafisadi kwenye mashirika ya umma.Na baadhi yao wanajua maovu yao hivyo wanamitandao yao ya kupachika watu watu wao ambao walitalajia wataendelea kuwemo kwenye vikao na hivyo kuinfluenced maamuzi kwenye vikao hivyo vya CCM.

Kuenguliwa kwao ni mafanikio makubwa sana kuona nguvu za wale engineers wa ufisadi wanaenda chini.
 
Hili limefanyika kwa ajili ya kumbeba mtu ayetakiwa na wana CCM masilahi kugombea urais 2015. Kupitia utaratibu huu tayari CCM imejichimbi shimo lake yenyewe, kwani wazee waliotengwa watakuwa nao na mtu wao na kwa kutumia ushawishi wao CCM itafarakana na hapo ndipo itaelekea kule KANU ilipo sasa.
 
kama kuna kosa kubwa kwa ccm chni ya jk ili ni namba moja na litamgharimu sana,hapa amechemka,kuwatoa wazee kama MKAPA unategemea nn,kuna nec ilyopita sikumbuk mwez gan pale lowasa alipoweka waz suala la richmond,asingekuwa mkapa kuingilia kati tngejua mengi ya jk wetu,hakka ccm yetu hii....,haya
 
Yaani badala ya kujipanga namna ya kukuiimarisha chama, wao wanahangaika kuhakikisha EL, EC na wenzao kama wabunge wasiwepo kwenye vikao vya maamuzi ili wapate nafasi ya kuwatosa. Si mnajua tena ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni?

Ila hao wazee wastaafu, hapo ndo wamekwenda mchomo tena kwa sana!
 
Back
Top Bottom