Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,770
Ikitokea kwamba mwendesha mashitaka anamfutia mtu kesi baada ya kupewa fedha na mtuhumiwa, hiyo ni rushwa. Na inakuwa rushwa si kwa kuwa mwendesha mashitaka kafaidika na ile fedha kibinafsi badala ya serikali ili kumwachia huru mtuhumiwa, inakuwa ni rushwa kwa kuwa haki (justice) imepindishwa kwa mtuhumiwa kununua uhuru kinyume na sheria. LInakuwa kosa hata kama mwendesha mashitaka atasema nilitumia zile hela kuchangia mradi wa maji kijijini kwangu.
Sasa hebu tubadili picha, badala ya mwendesha mashitaka, tuiweke serikali. Je inakuwa halali kwa serikali kuomba "hongo" kwa watuhumiwa ili waachiwe huru? Kanuni ni zile zile, tatizo hapa ni kwamba hii "hongo" inahalalishwa na serikali. Huo ndio ukweli, mpende msipende.
Hakuna tofauti na trafiki kukukama kwa makosa barabarani, ukampa hela ili akuachie yaishe. Huyo trafiki ni mpokea rushwa. Sasa hapa serikali imekuwa kama trafiki mpokea rushwa, hata kama hiyo hela ni kwa ajili ya mboga nyumbani!
Na mbaya zaidi kuna kipengele cha haki katika sheria. Hawa ni watuhumiwa. Serikali inajuaje kama wasingeshinda kesi zao? Kuwaambia watoe "hongo" ni namna fulani ya kitu kinaitwa "blackmail". Ni wazi kwamba hata kama wanajua wangeweza kushinda kesi zao wataomba msamaha yaishe na kutoa hiyo "hongo" kwa serikali.
Hii serikali ina mambo ya ajabu sana.
Update:
Zaidi ya suala la serikali kuhalalisha kupewa rushwa katika kesi za namna hii, suala jipya lililojitokeza ni serikali kuwaonea watu na kuwafanya wanunue uhuru wao kwa lazima, wapende wasipende, hata kama hawana kosa na serikali inajua kwamba uwezekano wa kuwatia hatiani ni mdogo sana. Serikali inachofanya ni kuchelewesha makusudi kesi za namna hii, hasa kwa wale wanaobambikiwa haya mashitaka, kwa namna tu ya kuwakomoa kutokana na sababu za kisiasa.
Na mbaya zaidi wigo wa kesi za uhujumu uchumi unapanuliwa kisiasa hadi kufikia vitu kama kupiga picha ya barabara mbovu. Sasa nikipiga picha ya barabara mbovu sijui serikali itanitoza shilingi ngapi ili niachiwe huru "kwa makubaliano".
Kitu cha aibu sana ni kuona mhimili wa mahakama unashiriki katika ubakaji huu wa haki za raia na kutumiwa kuuhalalisha.