hesbone
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 239
- 568
Usibadilike TEMPORARILY kwasababu unataka uonekane wife/husband material ili umu-impress mtu halafu mkifika ndani unarudia rangi-rangi zako zilezile ambazo ndio NATURAL YOU.
Muache akupende kwa ulevi wako, kwa umbea wako, Kwa Kutoa kwako udenda ukilala,Kwa kuwa mchafu na kutofua Boxer, kwa kunuka kikwapa cha njano, kwa umaharage ya Mbeya wako kwa sababu kama akikupenda KAMA ULIVYO LEO hata mkiingia ndani ATAKUPENDA TU.
Kwa sababu alijua aina ya mtu anayeingia naye ndoani na ameshajipanga kisaikolojia kuvumilia harufu ha boxer zako ukimuimpress kwamba hunywi kwa miezi mi3 akakuoa halafu hamad anakuta chupa za ndovu stoo patachimbika.
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, muonyeshe rangi zako halisi akupende kwa Uhalisi wako lasivyo utaolewa leo sawa na bajeti ya milioni 96 lakini Jiandae kuwa mjane baada ya miezi 6 kwa karatasi ya talaka ya Sh 50 Steshenari.
BE YOURSELF...