Kuwa ugenini mateso

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Imekuwa ikisemwa hivyo mara kwa mara. Mimi niliamini huu usemi mwaka 2002., nakumbuka nilikuja Dar kufatilia uhamisho wangu wa shule, nilikaa kwa baba yangu mdogo kwa takribani wiki moja. Huyo mama niliyemkuta hapo alikuwa hapiki mpaka mumewe awepo. Wiki niliiona kama mwaka, hata nilipoaga nilipewa nauli kimanati.

Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?
 
Mbona we una afadhali me niliwahi kupelekwa kwa mama mdogo,yule alikuwa kiboko akipika msosi ile saa ya kula natumwa sehemu ya mbali,ili nikirudi nikute wameshakula na kama ntajitahidi kuwahi kurudi,lazima nikute mlango umefungwa kwa ndani inabidi niwe mpole,kwa hiyo kula nilikuwa nakula usiku tu napo nilikuwa napigwa finga kwenye sahani na vifinyinyo juu,siku moja nilikuta wamefunga halafu hawapo,MUNGU saidia niliipata funguo walipokuwa wanaweka alooo niliingia kwa hasira nikala msosi na mwingine nikabeba,nikasepa moja kwa moja.
 
Mi ilinibidi niwe napiga kazi ile mbaya kutoka kutopendwa hadi kupendwa. Ila ni nouma jamani, usiruhusu mwanao akaishi uhamishoni wakati wewe dingi/maza yake upo.
 
Poleni jamani mliokutwa na mambo haya. Bahati nzuri mimi hayajanitokea ila nilishashuhudia mtu akinyanyaswa kwa kaka yake wa tumbo moja na mke wa kaka yake. Inauma sana
 
Yaani nikikumbuka basi tu.MUNGU nilinde.wanangu wasipate mateso niliyoyapitia kwa ndugu
 
omba Mungu msioe wake wachoyo yaani huwa wanakonda wakiona wageni wakati wa chakula
upo Gaga?
acha kabisa hasahasa wakiona wakwe zao huwa ndo wanaisha kabisa................
na midomo hukauka mithili ya mlamba chumvi.............
 
ni bora kila likizo umpeleke mtoto kwa ndugu ili akajifunze maisha, ukimuacha wiki mbili au tatu akirudi kanyookaaaaaaa. lazima appreciate unachompa. kila akikuangalia anaomba mungu usife leo.

hakikisha unampeleka mbali kidogo ili asiweze hata kudandia gari kurudi home.
 
Mbona we una afadhali me niliwahi kupelekwa kwa mama mdogo,yule alikuwa kiboko akipika msosi ile saa ya kula natumwa sehemu ya mbali,ili nikirudi nikute wameshakula na kama ntajitahidi kuwahi kurudi,lazima nikute mlango umefungwa kwa ndani inabidi niwe mpole,kwa hiyo kula nilikuwa nakula usiku tu napo nilikuwa napigwa finga kwenye sahani na vifinyinyo juu,siku moja nilikuta wamefunga halafu hawapo,MUNGU saidia niliipata funguo walipokuwa wanaweka alooo niliingia kwa hasira nikala msosi na mwingine nikabeba,nikasepa moja kwa moja.
Pole sana mkuu, ila ninachoshukuru ile situation ilinifundisha kujitegemea.
 
Nilikuwa nakaa kwa mamamdogo wakati na soma o-level day! Baada ya kugundua weakness yangu kwamba siwezi kula chakula chenye pilipili ilikuwa inasagwa kwa wingi na wakati wa kula inamwagwa kwenye mboga! Nilishindwa kuishi nikapata msamalia mwema mama mshiriki wa kanisa nilipokuwa nasali alinihost mpaka nikamaliza shule! MUNGU AMBARIKI TENA NA TENA na AMWONGEZEE UHAI MARADUFU NA MAFANIKIO ZAIDI
 
Mama mdogo au msamalia mwema
 
halafu hv ni kwanini wanawake ndo huwa na roho mbaya sana kwenye hz ishu?
Kwa maisha niliyoishi drs la 5 hadi 7 mungu ndo anajua.
Leo hii mama yule akiniangalia usoni anainamisha kichwa,haamini kama ndo namalizia malizia university.
Nakumbuka mama mzazi alinishauri enzi zile alipopewa ful stor na majiran kwa vile me nilikuwa sio muongeaji,"mwanangu wala usimchukie,soma hvyo hivyo tu,siku ukipata kazi mnunulie zawadi nzuri sana umpelekee"
na nitalitimiza hilo!
Khaaah! Hii thread imenikumbusha mbali sana,eeh mungu msamehe mama yule!
 
Nafasi haitoshi hapa kutoa ushuhudia wangu. Zaidi sijuwi nianze na kisa kipi na nimalize na kipi? Itoshe tu kusema kwamba kati ya watu walionyanyasika mi ni mmoja wao tena kwa kiwango cha kutisha kabisa. Hadi kufikia leo namiliki japo hiki kimeo cha tochi na leo napita hapa JF kweli MUNGU ndiye MUNGU.
Mtu kwao jamani!
 
omba Mungu msioe wake wachoyo yaani huwa wanakonda wakiona wageni wakati wa chakula

gaga umepotelea wapi? Kuna vitu vya kuwa wachoyo kama vile ambavyo ni vya mzee anapaswa kula yeye tu bila ya kuchangia au wasemaje?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom