tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Imekuwa ikisemwa hivyo mara kwa mara. Mimi niliamini huu usemi mwaka 2002., nakumbuka nilikuja Dar kufatilia uhamisho wangu wa shule, nilikaa kwa baba yangu mdogo kwa takribani wiki moja. Huyo mama niliyemkuta hapo alikuwa hapiki mpaka mumewe awepo. Wiki niliiona kama mwaka, hata nilipoaga nilipewa nauli kimanati.
Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?
Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?