Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Utekelezaji sasa ndio mtihani kwa wengi, tunapenda stori tu na kuishia kutamani.
 
Yaani huu mchanganuo nauona hapa ni kama mara ya 88 toka nimeanza kuuona sehemu mbalimbali miaka kibao iliyopita but ukweli ni kuwa theoretical expectations km hizi kamwe hazitatuacha salama,just simple like that mtu awe milionea pasipo kwanza kuwafundisha watu changamoto kuu zinazoukabili mfugo huo.

Issue sio kwamba watu hawana huo mtaji but changamoto kuu inayokwambisha watu ni hayo magonjwa yasiyoelezeka na bahati mbaya wataalamu wengi hawana uwezo wa kukabiliana nayo na mwishowe wafugaji wengi kuishia kuangukia pua.

Leteni kwanza elimu ya kutokomeza magonjwa ya kuku ndio mtuletee mchanganuo wa faida ama sivyo tutakuwa tunapiga story tu za KIBANGA AMPIGA MKOLONI.
 
HABARI,
"Kibanga Ampiga Mkoloni,
Hongera kwa habari nzuri ila pale mwanzo uliposema kuku 11 baada ya miezi mitatu utakuwa na kuku 300 au zaidi hiyo inawezekanaje kibanga?

LUMUMBA
 
Nimejitahidi saana kufuga lakini nikifanikiwa kupiga hatua kidogo unakuja ugonjwa unaondoka na kuku woote. Na hii ndio changamoto kubwa kwenye huu mradi.
 
Nimejitahidi saana kufuga lakini nikifanikiwa kupiga hatua kidogo unakuja ugonjwa unaondoka na kuku woote. Na hii ndio changamoto kubwa kwenye huu mradi.
Ukizingatia chanjo pamoja na kufugia kwenye eneo ambalo liko controlled hiyo ndio itakuwa salama yako.
 
Biashara ya ufugaji sio rahisi kama una moyo mdogo wa kukata tamaa.

Kuku anaweza kutotoa vifaranga woote wakafa
 
Ufugaji wa namna hii unawezekana kabisa lakini itategemea upo eneo gani, mjini au kijijini na kama ni mjini basi iwe angalao ni maeneo ya nje ya mji kidogo ambapo kuna nafasi ya kutosha kwani kuku zaidi ya 300 kuwafungulia eneo dogo utagombana na majirani kila upande.

Kwa kijijini inawezekana na hii ndiyo husaidia ufugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na faida huko ijapokuwa kinachowaangusha watu sana ni magonjwa. Ikiwa utafanya hivyo na kuongeza mbinu nyingine mbalimbali unaweza ukafikia lengo hilo japo uchambuzi wa gharama mleta uzi hajafafanua kwa kina sana.

Kuku wa kienyeji wana faida kubwa sana ukiweza kuthibiti suala la magojwa na kutumia vyema sayansi ya kutengenez vyakula kwa gharama ya chini.
 
Wazo zuri na mada kama ni muhimu kwa afya ya wanajukwaa na taifa kwa ujumla wake.

ANGALIZO: Tufanye tathimini kwa kungalia soko kwanza isije tukazalisha kwa wingi "kama nyanya" kipindi kile. chunguza ktk eneo lako ka kuna wafugaji wengi na soko pia
 
Ha ha ha...
Hivi nani alitunga hii hadithi aiseeh?
Kwanza, Kuku wa kienyeji huwa hawatagi kwa pamoja, na hawatagi mfululizo... Ukianza na Kuku 11 na ukienda vizuri inaweza fikisha Kuku 100 ndani ya mwaka mmoja ukijitahidi na uwe na Bahati kweli kweli...
Utajiri sio kama kucheza draft kwamba unaweka hapa na kupata pale...
Naongea kama mfugaji mzoefu na mbobevu, hii hesabu ya mada hii field HAIWEZEKANI
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
Mimi nafuga kuku wa kienyeji kwa matumizi yangu na familia (nyama na Mayai) na kuuza pale wanapokuwa wengi na pia kununulia chakula na dawa. Anachosema mleta mada si sahihi kwa kipindi kifupi hivyo.
 
Kuku 11 (wa kienyeji)wazalishe kuku 300 in 3 months ni impossible labda uwe unafuga panya. Kifaranga kinachukuwa miezi 3 hadi miezi 6 kukuwa na kuanza kutaga mayai. Tuwe tunaandika vitu vya ukweli sio kudanganyana kama wanasiasa wa hiki chama wanavyofanya
 
Back
Top Bottom