Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,698
8,843
Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Kuku-kupatana.jpg

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
 
nyumba za kupanga mtihani kweli kweli, shamba kuku ni elfu 6 tu
Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
Wakuu fursa kama hizi inahitaji kujiongeza kidogo,hapo unapotafutia ridhiki tafuta wenzako mmoja au wawili mtafute kiwanja kikubwa kidogo nje ya mji mchangishane kisha mkinunue mgawane.

Let's say kipo sehemu kina miguu 50×50 kinauzwa mill5 na wewe hunayo hiyo pesa yote,mkiwa wawili mkakinunua mkagawana pasu utaweza kutekeleza azma yako.

Muhimu we jichangishe tu na uzima uwepo.
 
Uzuri mada imekopiwa toka mtandaoni na sijui uzoefu wa mtoa na huko mada alikoitoa kwenye ufugaji wa kuku, inahitaji ujipange kuanzia ufugaji wenyewe + magonjwa ya kuku na baada ya hapo ulishafikiria kuhusu soko la kuku na changamoto zake? yote yanawezekana ila si kwa kirahisi kihivyo.
 
Hapa ndio watu hufikia tunaanguka katika mambo mengi. Badala ya kufanya jambo kwa moyo mmoja eti unajaribu. Ufanye kwa kupenda kabisa sio eti nitajaribu.

Mkuu nia ya kujenga ilikuwa kufuga kuku, lakini siyo kwa namna hii aliyosema mdau, hivyo nitajaribu kufanya namna yake
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
 
Hii michanganua kwa kuisoma hivi tu inaonekana ni simple ila ukienda field sasa.
Mkuu kuna uzi kama huu niliupitiaga nikakaa chini nikaufanyia kazi mkuu umelipa sana.Kuliko kujenga nyumba ambayo utapangisha watu chumba elfu 30-60 chumba kwa mwezi ni bora kufuga kuku mia kwenye hicho chumba nikiwa na maana kuwa ukiwa na ukuku mia una uhakika wa mayai 20 kila siku sasa yai moja la kienyeji ni 500 * 20= 10,000 so kwa mwezi una uhakika wa laki tatu ukitoa matunzo na usimamizi unabakiwa na 150,000( makadirio ya juu sana) sasa hapa hujapigiana kelele na mtu kachafua nyumba kabomoa mlango sijui umeme sijui kuvuta uchafu NK.Hii salio linatosha kabisa kwa familia ya kawaida kulipia bili ya umeme na maji kwa mwezi na kusukuma angalau kwa mboga kwa siku mbili tatu huku pia cku moja moja na wewe mfugaji kula mayai mara moja moja.

Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds!
 
76 Reactions
Reply
Back
Top Bottom