Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, May 21, 2018.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
  [​IMG]
  LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

  Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
  Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

  Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

  Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
  Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

  Mchanganuo Wa 69500 ni:-
  Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

  Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
  Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
  layer's consetraite

  Kilo 25 kifuko. = 21500.

  Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

  Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

  Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
  Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
  Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

  TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
  Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

  Jogoo 1 = 20000
  Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
  Itakuwa imebaki shs. 60500

  -Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

  Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
  Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

  Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

  Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

  Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
   
 2. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #61
  May 30, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Unaishi wapi ambapo huna sehemu ya kufugia? sehemu ya mita za mraba 6 panatosha kufuga hadi kuku 120.
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #62
  May 30, 2018
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,728
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Liwezekanao leo lisingoje kesho
   
 4. usiambini

  usiambini JF-Expert Member

  #63
  May 30, 2018
  Joined: Jan 12, 2013
  Messages: 507
  Likes Received: 412
  Trophy Points: 80
  Hakuna utajiri wa laki 3.Nyoneza huenda kwenye fungu.
   
 5. stragic

  stragic Member

  #64
  May 30, 2018
  Joined: Apr 25, 2018
  Messages: 29
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  Izi mkuu apa dar zinapatikna wap??
   
 6. 42_007

  42_007 JF-Expert Member

  #65
  May 30, 2018
  Joined: Mar 10, 2015
  Messages: 1,561
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Ufugaji wa motiveshen spikaz ni mwepesi mno
   
 7. dingimtoto

  dingimtoto JF-Expert Member

  #66
  May 30, 2018
  Joined: Jan 9, 2016
  Messages: 4,022
  Likes Received: 8,304
  Trophy Points: 280
  Nipo kwenye harakat za hiyo project lakin nimeona,kuna sehemu comrade amekosea mfano kwenye bajeti ya banda
   
 8. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #67
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  huo ndo mpango wa biashara ni makadirio au makisio inahitaji utafuti wa kutosha kikubwa ni chanjo, na kujitahidi kukumbuka vitu vidogo dogo ka gharama za usafiri wa kuku hasa huko ununuliako, gharama za kusafirisha material, gharama za kuparaza hayo maisndi na vitu vingine vidogo ambavyo ni muhimu, ukiangalia vikubwa tuu utakwama ka utakuwa huna hela ya ziada mfukoni
   
 9. tzhello

  tzhello Member

  #68
  May 30, 2018
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Hii kitu sio lahisi kama wengi wanavyofikiria,ukizingatia makadirio yamewekwa juu sana.mimi nilianza hivyo mwaka jana lakini mpaka leo nina kuku kama ishirini tu maana niliamua kuwala baadhi.changamoto kubwa nilioiona ni kutunza vifaranga ili waongezeke hao kuku,hapo ndo kimbembe:confused:
   
 10. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #69
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mchanganuo wa biashara unahitaji umakini sana pia wakati mwingine unagoma ka usipokuwa realistic hasa ka hapo ulipoona gharama za banda, banda unatakiwa ujenge la kudumu ili usije ingia mfukoni tena ambako kutaharibu mipango ya pesa kwahiyo lazima ujenge zuri na imara
   
 11. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #70
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mkuu inawezekana japo kuku wa kienyeji ukuwaji wake ni wa taratibu kingine usipende fuga ka huna elimu ya kutosha kuhusiana na ufugaji wa hicho kitu maana unawezakuta unapga mieleka bure
   
 12. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #71
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  uwezo huo hana labda kwa wale wanaofuga machotara ama wale kuku wanaita wa malawi japo si wa kienyeji ila wanawafuga kienyeji,
   
 13. Tajiri mpole

  Tajiri mpole Senior Member

  #72
  May 30, 2018
  Joined: Apr 15, 2018
  Messages: 109
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  Mchanganuo mzuri.. Vijana wapate fursa
   
 14. tzhello

  tzhello Member

  #73
  May 30, 2018
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Sijasema haiwezekani mkuu ila nimesema sio lahisi kiasi hicho tunachoaminishwa,na kingine ni kweli kama ulivyosema hawa kuku hasa pure wa kienyeji wanakawia sana kukua na wakati mwingine usipokuwa makini wanadumaa,bora kulima mboga mboga kuliko kufuga pure kienyeji (mimi binafsi);)
   
 15. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #74
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  hizi gharama si fixed kutokana na mazingira kutofautiana, mfano mie wa kijijini ntajenga banda kwa bei nafuu maana miti ntakata msituni ila wee wa mjini utanunua mbao au mabanzi,mie nitatumia kamba kujenga banda we utatumia misumari, pia ntakandika banda na kuezeka kwa nyasi, hiyo ni tofauti kubwa. pia gharama nyingine ni kujitafutia zitakuwaje kulingana na mazingira tutokayo natumai mkuu alitoa gharama za jumla na zile gharama common kwa wengi.
   
 16. Uchira 1

  Uchira 1 JF-Expert Member

  #75
  May 30, 2018
  Joined: Oct 9, 2017
  Messages: 388
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  nakubaliana nawewe mkuu mie nimefuga toka mdogo na mpaka mkubwa na nimefanya ufugaji wa kawaida mpaka wa kisasa so naelewa mfugo ukizingua hutatamani hata kusikia habari za ufugaji tena
   
 17. cephalocaudo

  cephalocaudo JF-Expert Member

  #76
  May 30, 2018
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 10,558
  Likes Received: 13,155
  Trophy Points: 280
  Business is timing.
   
 18. tzhello

  tzhello Member

  #77
  May 30, 2018
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Pamoja!:D
   
 19. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #78
  May 31, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Kuna mdau humu anaweza kukuagizia mtafute nadhani ni Mwalimu CRT km SIJAKOSEA.
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #79
  May 31, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Ndio mkuu, kuku kutaga ni lishe tu.
  na sio kutaga tu, hata kumuuz akutokas kifaranga mpaka kilo Moja kwa Miezi miwili kama wakizungu inawzekana ni lishe tu .
   
 21. zeshchriss

  zeshchriss JF-Expert Member

  #80
  May 31, 2018
  Joined: Apr 27, 2017
  Messages: 2,817
  Likes Received: 3,350
  Trophy Points: 280
  Naomba kujua bei ya hii mashine
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...