Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

mkuu kuna uzi kama huu niliupitiaga nikakaa chini nikaufanyia kazi mkuu umelipa sana.Kuliko kujenga nyumba ambayo utapangisha watu chumba elfu 30-60 chumba kwa mwezi ni bora kufuga kuku mia kwenye hicho chumba nikiwa na maana kuwa ukiwa na ukuku mia una uhakika wa mayai 20 kila siku sasa yai moja la kienyeji ni 500 * 20= 10,000 so kwa mwezi una uhakika wa laki tatu ukitoa matunzo na usimamizi unabakiwa na 150,000( makadirio ya juu sana) sasa hapa hujapigiana kelele na mtu kachafua nyumba kabomoa mlango sijui umeme sijui kuvuta uchafu NK.Hii salio linatosha kabisa kwa familia ya kawaida kulipia bili ya umeme na maji kwa mwezi na kusukuma angalau kwa mboga kwa siku mbili tatu huku pia cku moja moja na wewe mfugaji kula mayai mara moja moja.

Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds!
Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds!-Bob

I like it
 
Hiv kuku wa kienyej unaweza uka wafuga kwa Ku wafungia ndan kama hawa kuku wa kizungu" maana Nina vyumba viwili dabo vipo tupu
Yes u can, ili ni lazima liwe na hewa ya kutosha. Lakini pia utakuwa na kazi ya kuwaletea majani mabichi kila siku pamoja na wadudu.
 
umenena ukweli mtupu
Nimeanza mwezi March na kuku 35 tu
Leo ninao kuku 120 (110 ni vifaranga na mayai tunaokota karibu 5 kila siku)
Ninaona taa ya kijani mbele maana soko ni uhakika kabisa
Mkuu upo mkoa gani??
 
Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
Maeneo ya Dar es salaam Tanzania ukifugia kwa sasa kisheria hairuhusiwi kufuga kuku kwa sababu ya uchafuzi wa hewa na kinyesi chake labda nje ya DSM
 
hapo kwangu mimi vitu viwili ni kikwazo:
1. mashine ya kukodi ya kutotolea mayai.
2. mashudu ya alizeti
 
Jamani nikweli kwamba kuku wa kienyeji anatanga siku 30 mfululizo? mbona tuliokijijini tungekuwa matajili sana. acheni fix watoto wa mjini.
Wewe hujawahi kufuga mkuu,labda unafuga ilimradi umefuga tu...
 
hapo kwangu mimi vitu viwili ni kikwazo:
1. mashine ya kukodi ya kutotolea mayai.
2. mashudu ya alizeti

Mbona vinapatikana vyote ?
Ona hii Incubator ya mayai SABA.
haifiki hata 100,000/=

HTB1GtF_ldbJ8KJjy1zjq6yqapXab.jpg
 
Hivi incubator kama hiyo ya mayai saba nitaipata kwa bei gani ?
 
Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
Unaishi wapi ambapo huna sehemu ya kufugia? sehemu ya mita za mraba 6 panatosha kufuga hadi kuku 120.
 
76 Reactions
Reply
Back
Top Bottom